Mahmoud Qaasim
JF-Expert Member
- Nov 3, 2007
- 923
- 264
Kosa jingine kubwa ni kujenga Taifa la wananchi waoga katika kila jambo hata katika kujua haki zao za msingi, hivyo kuzalisha jamii ya watu wasiowabunifu katika kuyakabili maendeleo binafsi.
Mkuu sahiba heshima mbele.
Tuko pamoja katika hili kama kunakosa ambalo nyerere alilowatendea watanzania ni hili la kutubandikia fisadi Mkapa.Kosa lingine kubwa ambalo bado litaendelea kututesa kwa muda mrefu ni kutengeneza katiba iliyomfanya rais wa Tanzania kuwa mungu mtu.
Mwalimu alikuwa na KURA ngapi kwenye CC, NEC na Mkutano Mkuu wa CCM wakati wa uteuzi wa Mkapa? Mkapa alitubadilikia sana baada kifo cha Mwalimu.
Katika historia ya Dunia hakuna mtawala aliyewahi kufanya maamuzi yakawa sawa 100% au yakawapendezesha wote. Labda kama mnamfahamu mniambie Nkurumah vile vile alikuwa na matatizo yake...Soma Historia zaidi na utaafiki kwa maelezo hayo basi tukubali Nyerer hakuwa kamili pia ila kuna watu ambao walitaka nyerere sikosea hata kitu kimoja..sasa hiyo haiwezakani lakini katika ulinganisho wa mwisho mazuri ya nyerere yanazidi mabaya aliyotenda na ni viongozi wachache sana wa kiafrika wakati huo unaweza kuwaweka katika mizani sawa na nyerere. He was extraordinary on the other was he was not ordinary.
Kuhusu Umoja wa Afrika Nyerere pekee hawezi kulaumiwa na hapa ninamaanisha hata angekuwa upanda wa nkrumah haimaanishi umaja wa afrika ungeafikiwa. Je labda uniambie kama walipiga kura ratio ya proposing na opposing ulikuwa ngapi? sasa kwa nini kelele hizi? Nyerere ,..nyerere kila siku .Huyo Nyerere hakuwa Mungu na hata angeunga mkono kula yake ilikuwa ni moja tu na haimaanishi vilevile huo muswada ulishidwa kwa kula moja.
Nyerere asilaumiwe labda mlaumu kizazi chote cha utawala kipindi hicho. Halafu Winston Churchil alisema ' Ukianzisha ufitini kati ya wakati huu(present) na uliopita (past)uko kwenye hatari ya kushindwa wakati ujao(future). Ndugu tuangalie mbele, Tuangalie Je Gaddaffi ataweza? Kikwete atasaidiaje? na marais wengine watasaidiaje na Je itawezekana? au ni day dreaming?
Mahmoud,Kosa jingine kubwa ni kujenga Taifa la wananchi waoga katika kila jambo hata katika kujua haki zao za msingi, hivyo kuzalisha jamii ya watu wasiowabunifu katika kuyakabili maendeleo binafsi.
Sahiba,Jasusi kwa maoni yako unafikiri wakati wa Nyerere watu kama Mengi wangeexist ?
Sahiba,
For your information Mengi alikuwepo wakati wa Nyerere. Hakuwa na utajiri alionao hivi sasa lakini alikuwepo na alikuwa katika hali nzuri tu. Kamuulize!
Mahmoud,
Nifahamishe utajengaje taifa la watu waoga? Yaani Nyerere alikuwa na uwezo wa kushika akili za kila mtu? Leo karibia miaka 10 tangu Nyerere aondoke duniani mbona wajasiri sijawaona? Kiongozi yeyote hawezi kumfanya mtu awe mbunifu. Ubinifu ni hulka. Tafuta kisingizio kingine cha kumhukumu Nyerere.
Nimejaribu sana kuwa neutral ili niweze kukuweka katika mzani gani wewe SAHIBA ila nadhani kuwa fair naweza kusema una"KAUJINGA" fulani ka historia ya Africa....thts is much fair i can beMkuu sahiba heshima mbele.
Tuko pamoja katika hili kama kunakosa ambalo nyerere alilowatendea watanzania ni hili la kutubandikia fisadi Mkapa.Kosa lingine kubwa ambalo bado litaendelea kututesa kwa muda mrefu ni kutengeneza katiba iliyomfanya rais wa Tanzania kuwa mungu mtu.