Africa ikiwemo Tanzania kwisha kazi, cheki hiki kipande ujionee africa inavyo gawanywa

Tumekwisha wakuu, do, kuna watabili waliwahi kutabili kutakuwa na utumwaw wa pili na huu utakuwa mbaya kuliko ile wa kwanza ndo haya

Tatizo waafrika tunafuga manyigu, halafu tunataka kupata asali, ulishawahi kuona wapi nyigu akatoa asali?
Huo ndio ubepari unaohubiriwa na wanasiasa wenu sijui ccm, chadema, cuf nk. wote ni ushenzi tu! Ukihoji eti "we have to undergo with the world situation" nani kasema ni lazima? PUMBAVU! Inakera sana! Unadhani tungekuwa tunajitegemea katika mifumo yetu, hawa wangeingia kihole hole tu humu? PUMBAVU TENA! Kwanini tunaacha wazungu kuturoga?
Ukihoji tu juu ya uhalali wao wa kuhodhi aridhi kwetu, watakufungulia ma-documents yenye sahihi zetu wenyewe kwenye UN Declaration of HR, Free Market Policy, Privatization Policy, Democratization, Foreign Investiment, nk. kote huko sahihi zetu zinatufunga wenyewe. Sasa kunatofauti gani kati yetu na wale wa kipindi cha Karl Peterz? Upuuzi mtupu!
Mungu wetu anaita!
 
Jana nlimsikia waziri ardhi Tibaijuka bbc akifoka mpaka povu linatoka mdomoni, anasena kuna hekta 22,000 wanawapa wawekezaji Pwani.
 
ardhi kubwa sana imechukuliwa na wawekezaji wa nje kule Kilwa, Lindi, Mpanda kwa ajili ya bio-fuel. serikali hutumia nguvu kubwa kuwalinda wageni hao.

Ukiangalia hizo takwimu ni kweli kabisa hawa jamaa mpango wa kujimilikisha ardhi na hasa ktk hili bara la Afrika upo na ni mkubwa sana. Na hili suala la umilikaji wa ardhi pamoja na mambo mengine ni suala ambalo ktk huu mchakato wa uandikaji wa katiba mpya tunahitajika kulijadili kwa mapana na kwa kina ili kuliweka bayana!
 
Hii yote ni kwa sababu ya viongozi wetu vilaza. Bado wanashadidia shanga kama kina mtemi mangungo na kuweka saini kuuza ardhi yetu. Mungu tusaidie ili tuwe huru kweli kweli. ardhi pekee ndio msingi mkuu wa uchumi. Ikibahatika kupata mtaji wa msuli na ubongo ulio fresh huzaa sana! Lakini ipo siku mambo hayatakuwa kam hivi. Let's wait and see!!!
 
Nakasirika sana na hulka yetu watanzania kulalama tu bila kutoa suluhisho....haya wameshagawana land so???toeni suluhisho!!!!ila pia wako wapi vijana wanaoweza aimamua haki na kujituma???na nnakasirika zaidi na hiyo serikali yetu ya majambazi na wanyanganyi wanaoshindwa hata kusupport sera zao wajinga kweli hapo kwenye bio fuel ningesema wananchi wangewezeshwa walime mtama wauze na sio kuwapa hao wazungu ardhi!!inasikitisha kwa nchi Kama Tanzania kuongelea kilimo cha biofuel wakati njaa kila mwaka.......
 
Suala la kutoa ardhi kwa ajiri ya uwekezaji lina manufaa sana kwa nchi endapo serikali itakuwa makini. Ardhi haiwezi kuwa na manufaa kwa mtanzania kama haijatumiwa kwa kilimo chenye tija. Tutaendelea kuwa maskini kama tutahold vitu ambavyo hatuwezi kuvibadilisha into money value. Suala hapa ni serikali iwe karibu nao kuhakikisha kile kilicholengwa kwenye lease agreement ndicho kinafanyika. Mfano hivi sasa kuna tafiti kuhusu mafuta maeneo mbali mbali isije muwekezaji kakodi ardhi kwa ajiri ya kilimo baadae eneo hilo anagundua kuwepo mafuta anaanza kuchimba kimya kimya hii haitakubalika. Ikumbukwe huwezi kusema nina utajiri wa madini kama hujaweza kuyachimba.
 
Bunge sio sehemu ya kutangaza jinsi ardhi inavyogawiwa! Hivi sasa kuna ardhi kubwa sana imechukuliwa na wawekezaji wa nje kule Kilwa, Lindi, Mpanda kwa ajili ya bio-fuel. Mambo haya hufanyika kimya kimya hadi hapo wananchi watakaposhtuka ndipo ukweli hufahamika, lakini huwa haisaidii badala yake serikali hutumia nguvu kubwa kuwalinda wageni hao.

Ndio maana tunapambana kuiondoa madarakani serikali hii ya CCM inayouza ardhi yetu kwa wazungu na waarabu tuliowaondoa mwaka 1961. Mk..we...re anachekacheka tu.. kumbe anauza nchi yetu!
 
Namshangaa huyu jamaa yetu alietuasa kuwa kama mbayuwayu yaani akili za kuambiwa changanya na zako mwenyewe lakini yeye anashindwa kufanya hivyo, yaani yeye akisifiwa au kualikwa na mzungu anavimba kichwa badala ya kudadisi why is this happening to him, ooh what a gullible person he is!!!!
 
Can it be stoped?
Or is it to happen and accepted as like otherr systems which were allowed to exist and live untill its senility!
I mean waafrica na wastaarabu wengi hawakupenda maazimio ya mkutano wa Berlin lakini yalitekelezwa, vivyo hivyo kwa utumwa.

Jambo moja naweza fikiri na pengine kuatarajia, vita kuu ya tatu itakuwa vita ambayo pengine itakuwa kubwa kuliko zote zilizopata kutokea, vita kati ya wenye silaha zote na wasio na silaha wala jeshi, vita kati ya wanyonge na wasio na matumaini kabisa dhidi ya wakubwa na mawakala wao!

Nadhani kuna wakati viongozi wanahitaji kuelewa kuwa unaweza kutofautiana na Dunia-IMF,world bank,nk- kwa maslahi mapana ya wananchi wako na ukabaki salama.

Kuna wakati huwa natafakari sana kiini cha ugomvi kati ya 'wakubwa ' na Mugabe.
 
Can it be stoped?
Or is it to happen and accepted as like otherr systems which were allowed to exist and live untill its senility!
I mean waafrica na wastaarabu wengi hawakupenda maazimio ya mkutano wa Berlin lakini yalitekelezwa, vivyo hivyo kwa utumwa.

Jambo moja naweza fikiri na pengine kuatarajia, vita kuu ya tatu itakuwa vita ambayo pengine itakuwa kubwa kuliko zote zilizopata kutokea, vita kati ya wenye silaha zote na wasio na silaha wala jeshi, vita kati ya wanyonge na wasio na matumaini kabisa dhidi ya wakubwa na mawakala wao!

Nadhani kuna wakati viongozi wanahitaji kuelewa kuwa unaweza kutofautiana na Dunia-IMF,world bank,nk- kwa maslahi mapana ya wananchi wako na ukabaki salama.

Kuna wakati huwa natafakari sana kiini cha ugomvi kati ya 'wakubwa ' na Mugabe.

Tatizo la watawala wa nchi kama Tanzania wanafikiria kushiba leo wakati viongozi wa G8 wanafikiria miaka 100 ijayo. U Mangungo mtupu.
 
Wanasema hakuna utumwa mbaya zaidi uliowai kutokea dunia hii kama huu unaofanyika karne hii.
 
Msiogope ni wawewkezaji tu.Chamsingi tuingie nao mikataba kwa maslahi ya taifa

Tumbaf! Uingie nao mikataba wakati wenzio tayari wameshamilkishwa ardhi kwa miaka 99!? Hapa tujipange kupigania ardhi yetu. Hapo tunajipanga na kuvamia mashamba kama walivofanya kule bonde la Kiru Babati. Hivi kwa nini Serikali isiwe inapugawia kwanza hiyo ardhi ili sisi Wananchi ndo tuingie na hiyo mikataba hao wawekezaji? Tz viongozi Hakunaga!
 
Back
Top Bottom