Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS)ni mzungu?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Naibu Waziri Wa Uchukuzi Dr. Athuman Mfutakamba (mwenye suti) akipata maelezo ya utendaji wa shughuli za upakuaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam jana jijini kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS) Neville Bissett.
ina maana hata hii kazi hakuna mtanzania anayeweza kuifanya? give ma a break: au mimi ndio kihiyo? kwani huyu afisa anatakiwa afanye nini kitu ambacho hakuna mtanzania anayekiweza?
03.jpg
01.jpg
 
Sijui una maana gani? Hakuna mtu anaeweza kuwekeza mabilioni ya pesa kiasi kikubwa halafu nafasi ya utendaji mkuu ikaanda kwa mtu asiekua upande wake eti kisa utanzania. Kampuni ya TICTS inamilikiwa na kampuni ya HPH kwa asilimia 70 na asilimia 30 ndio inayomilikiwa na mtanzania(Karamagi). Mwenye hisa nyingi ndio mwenye maamuzi na nafasi ya Mtendaji Mkuu ni nafasi nyeti sana huwezi kuijaza kwa kutumia vigezo vya utaifa wakati watu wamewekeza mtaji mkubwa. Zingekua nafasi nyingne sawa lakini hii nafasi hakuna popote inapowekewa kigezo cha utaifa labda kama ingekua ni shilika la umma.
 
Wabongo kwakutaka kupekenyua mambo ya watu kikubwa tutafute pesa tu ndugu zanguni
 
Hivi hakuna Watanzania wanafanya kazi nje, mfano Uk,USA n.k?Na je huko hawana wataalam wa kariba hizo?
 
Licha ya uteuzi wake nahisi kuna hisa zake hapo, hizo ndio fursa ambazo watanzania badala ya kuziwania mnabaki kupiga siasa tu.
 
Kwenye kampuni yangu nitaweka afisa mtendaji mzungu...
Watanzania wanawaza kuiba wanapoanza kazi...
 
Mr Clean (BWM) alisha sema rangi ya paka si hoja mradi akamate panya tu.
 
mbona huulizi kwa nini NMB ceo wake ni mzungu,, au NBC, Vodacom, Airtel, Tigo etc kote mabosi ni wazungu na wageni weusi..

Watanzania mnawaza kuiba tu.

Watu wamewekeza hela zao nyingi kama mtaji.. wakubebe kisa Mtanzania

kuongoza nchi yetu tu yenye rasilimali kibao Tumeshindwa.. Tutaweza kampuni za watu
 
Sijaelewa unamaanisha nini

Rais mstaafu Benjamin William Mkapa (BWM) a.k.a Mr Clean aliwahi kutoa hiyo kauli mwaka 1996 wakati wa ubinafsishaji/uuzaji wa NBC kwa makaburu akimaanisha rangi ya ngozi ya mwekezaji siyo muhimu hata kidogo kikubwa aweze kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kama taifa juu ya uwepo wake mfano.ajira,kodi nk.
 
No kweli unachosema.wabongo wapo wengi tu wanaweza ila most of them ni wezi.so ni ngumu.kumpa kwa sababu anaweza kuamishia ukoo wote hapo
 
Back
Top Bottom