Afisa Magereza aacha kazi aolewa na mfungwa mbakaji

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Afisa Magereza aacha kazi aolewe na mfungwa mbakaji

Alison kushoto na Royston Wednesday, February 04, 2009 6:01 AM

Afisa magereza wa gereza moja nchini Uingereza ameacha kazi yake ili aolewe na mwanaume ambaye alifungwa katika gereza alilokuwa akifanya kazi kwa makosa ya ubakaji.

Afisa magereza huyo aliacha kazi yake na kununua nyumba ili waishi pamoja na mpenzi wake ambaye alifungwa kwa makosa ya ubakaji.

Alison Uyanik alinunua nyumba pamoja na Royston Wells baada ya kuangukia kwenye mapenzi wakati Royston alipokuwa akitumikia kifungo chake jela.

Alison mwenye umri wa miaka 41 ambaye aliachika na mumewe miaka kadhaa iliyopita, aliangukia katika mapenzi ya mbakaji huyo wakati akitumikia kifungo katika jela ya Whatton iliyopo Nottinghamshire, Uingereza ambayo wafungwa wanaume wa makosa ya ubakaji hufungwa jela hiyo.

Wapenzi hao walinunua nyumba katika mji anaokaa Alison na walihamia kwenye nyumba hiyo muda mfupi baada ya Royston kuachiwa huru kuendelea na kifungo cha nje mwaka jana.

Marafiki wa Alison walipigwa na butwaa na kusema kwamba Alison ameitupa kazi nzuri yenye mshahara mzuri na marupurupu kibao.

"Royston amekuwa akijitetea kwamba hakutenda kosa la kubaka, lakini hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kujua ni nini hasa Alison alikigundua kwa Roy mpaka kuamua kuolewa naye" walisema rafiki zake.

Chanzo cha magereza kilisema kwamba uchunguzi uliofanyika haukugundua wapenzi hao kufanya mapenzi ndani ya gereza hilo.

Wazazi wa Alison walikuwa hawajui kwamba Royston mwenye umri wa miaka 37 aliwahi kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kubaka kwakuwa Alison aliwaongopea wazazi wake kwamba alikutana na Royston katika sherehe moja mjini humo.


SRC-NIFAHAMISHE.COM
 
Penzi ni kikohozi, kulificha huliwezi. Kama wamependana ni haki yao kuoana.
 
Last edited:
Inzi kufia ndani ya kidonda jamani!!! Acha wapendane. Sasa sielewi ni upendo wa kweli au ni mazingira yaliwafanya waanguke katika penzi maana jamaa alikuwa amefungwa na hakuwa na choice kwani ukiwa mfungwa unasahau kabisa ile habari. Kwa mantiki hiyo kila demu anaonekana fresh. Tuwape muda tuone yatakayojiri katika mahusiano hayo, maana huenda pia bibie alikuwa desparate baada ya kuachika. Pia yawezekana kuna ka upendo ndani mwao, who knows???? Fall falll faaaaaaall in loooooooove.
 
Je yafaa kukaa hapa kwenye jukwaa la siasa?????
Hapana, kuna ukumbi wa Mapenzi ambako ndiko inafaa kukaa huko ili iweze kujadiliwa kwa kina. Hata hivyo tatizo la uvivu la wajumbe wengi kutembelea sehemu nyingine humu ndani ya JF linazidi kuwa kubwa.
 
Duuh!! Kweli JF inakokwenda siko! Sioni mantiki ya thread kuwa hapa kwenye jukwaa la siasa! Let's try and be more serious on issues that matter the most.
 
Back
Top Bottom