Afisa Afya Mkoa wa Kagera akanusha kuingia kwa ugonjwa wa Ebola, JamiiForum yatajwa

Hivi afisa afya who is this, anajua hata kufanya diagnosis, na ndiyo maana hana taarifa coz hajui hata what is ebola, kumekuwa na outbreak za measles kibao tunawapa taarifa ili watoe health education lakini nothing they are doing. Poor them acheni kubishana naye kama mganga mkuu kaona then this guy is nothing

shughulisha kichwa jombaa, Afisa afya ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za infenctiouz disease na kuwepo kwa dalili haina maana kwamba ebola imekuwa confirmed. kilichotangazwa ni kwamba mgonjwa mwenye dalili za ebola na sio mwenye ugonjwa wa ebola, kama unaakili utakuwa umeelewa lakin kama uliiba mtihani utabisha mpaka kesho.
 
nataka WALICHOSEMA ITV usiku huu...kwani nipo mbali na TV!!

Mkuu ITV wametoa habari nzima pamoja na taarifa toka kwa daktari.. Ni kwamba kuna mgonjwa mmoja mwenye dalili zote za ebola.. Anaharisha damu.. Anatapika damu na anatokwa na damu puani.. So walichofanya wamemtenga yeye mgonjwa na nesi pamoja huyo aliekuja na mgonjwa.. Vle vle Daktari ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hao waliosafiri kwenye bus moja na mgonjwa.. Nadhani kuna haja ya Serikali kulichukulia kwa uzito wa juu hili janga..

Sent from Tora Bora..
 
Kumbe Afisa Afya wa mkoa wa Kagera naye anaisoma Jamiiforums!? Sasa ni wazi kwamba JF is rocking everywhere.

Back to ebola; mganga mkuu wa wilaya amethibitisha kuwepo mgonjwa mmoja mwenye dalili zote za ebola. Na kwamba wanasubiria wataalamu wa afya toka mpakani ili kufanya uchunguzi wa kina.

Je huyu afisa afya wa mkoa amefika karagwe kuthibitisha taarifa hiyo kabla ya kukimbilia kukanusha?

Huu upuuzi wa kukimbilia kutoa taarifa za kukanusha kila jambo bila kufanya uchunguzi ama kupata taarifa za kina ndio zitasababisha watu wengi wapoteze maisha ikiwa ugonjwa umeingia ama utaingia huko kagera.

Tunahitaji tume kuchunguza.
 
Nimemsikiliza vizuri sana kupitia habari ya tbc1 kasema yule mtoto hana ebola na anaendelea vizuri tu kwenye chumba alichofungiwa cha ajabu akusema anaumwa nini maana kakanusha hana ebola sasa swali anaumwa nini???
 
Duh kumbe JF inasomwa hadi Nyakahanga, Murongo, Bugene, Umugakorongo, Umurushaka, nk.Mimi nilikuwa nikidhani inasomwa Dar, Arusha, New York, Washington DC, London kumbe siyo huko peke yake. Hakika JF ina impact kubwa ya kijamii na kisiasa hapa nchini. Tuitumie kwa weredi na kwa manufaa ya nchi yetu kwa ujumla.
 
Umeingia umeingia umeonekana kwa nani?

another great thinker! tena kumbuka kila mtu anaiheshimu profesional yake, kwa afisa afya kutangazia taifa kwamba ugonjwa wa ebola umeingia Tanzania wakati sio kweli ni kujishushia taaluma yake ikiwa kama yeye ndio muhusika wa kwanza ktk infenctiouz diseases prevention and control.
 
mwenyewe nashangaa!hii news ilikua covered na ITV jana usiku,walisema kuna mgonjwa ana dalili za huo ugonjwa!sasa analaumu JF ya nn?au anataka naye ajadiliwe na wana JF?wataagizia CV yako sasa hv!chwzea JF ww!waulize wanasiasa wanaiogopa JF manake kwa data imeshindikanika!
 
QUOTE=Ngalikivembu;4372828]Muhtasari wa habari wa saa 10 jioni hii TBC1 imemuhoji Afisa Afya Mkoa wa kagera juu ya kuingia kwa ugonjwa wa Ebola nchini hususani mkoani humo, amekanusha. Anasema taarifa hiyo haina ukweli. Ametaja kuwa JamiiForums ndio imeandika taarifa hiyo. Hii inatoka na taarifa aliyoandika tatanyengo mchana kuwa ugonjwa huo umeingia Kagera.

Mimi ni mmoja wa walioona taarifa mpasuko ya ITV mchana, Mwandishi wake Cosmas Makongo alikuwa akiripoti taarifa ile leo. Na hata tatanyengo aliweka source kuwa ni ITV. Kwa hiyo huyu Afisa Afya alipaswa kuilaumu ITV kwanza kabla ya kuirukia JF.

Aiombe radhi JF yetu. Tusubiri taarifa za jioni ITV tena maana walituahidi kutuletea taarifa zaidi.[/QUOTE]

Watu wengine bwana, kila kitu wao kukanusha tu, huenda hata lenyewe likilazwa kwa ugonjwa wa Ebola litaendelea kukanusha tu wakati linatokwa na damu mpaka kwenye masaburi.
 
Ugonjwa wa ebola waingia nchini
• Mtoto wa miaka 6 abainika

na Andrew Chale


amka2.gif
UGONJWA hatari wa ebola ambao umeua idadi kubwa ya watu nchini Uganda umeripotiwa kuingia nchini.
Taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zilibainisha kuwa ugonjwa huo umeingia nchini katika Wilaya ya Kyerwa, Kijiji cha Bulongo, mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ugonjwa huo umegundulika kwa mtoto mmoja wa miaka sita, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alikutwa na dalili zote zinazohusiana na ugonjwa huo.
Vyanzo vya habari kutoka eneo la tukio hilo vimedokeza mtoto huyo aligundulika mapema jana baada ya kuonesha dalili za ugonjwa huo ikiwamo kutokwa na damu sehemu za puani, mdomoni na sehemu nyingine za mwili huku akiwa na homa kali muda wote.
“Mpaka sasa watu watatu akiwamo mama mtoto, mtoto na muuguzi aliyekuwa akimuuguza wamewekwa kwenye nyumba maalumu kwa uangalizi mkali ili kusubiri wataalamu wa ugonjwa huu kuja kuwatibu na kuchukuliwa vipimo zaidi,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Karagwe, kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa ndipo ilipobainika kuwa na ugonjwa huo na dalili zote ni za ebola, na kuamuliwa kuwekwa kwenye nyumba maalumu na uangalizi mkali.
Mganga Mfawidhi wa Wilaya, Dk. Charles Andrew, alisema wameamua kuchukua tahadhari kwa kuweka kambi maalumu eneo alipobainika mtoto huyo.
Alisema mtoto huyo, mzazi wake na muuguzi aliyempa matibabu ya awali wamewekwa katika nyumba moja ambapo kila mtu ametengwa katika chumba chake wakifanyiwa uchunguzi zaidi.
Alibainisha kuwa uchunguzi huo utawahusisha wataalamu waliobebea.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Masawe, amekiri kuwepo kwa taarifa za kuonekana kwa ugonjwa huo na alisema wanasubiri timu ya wataalamu kutoa ufumbuzi.
Masawe aliwataka wananchi kuwa makini na wageni wanaotoka mipakani hasa Uganda ambako ugonjwa huo umewaathiri watu wengi.
Alisema wananchi pia ni vema wakaacha kushikana mikono na watu pamoja na kuwa wangaalifu katika maeneo mbalimbali wanayokuwapo.
Hivi karibuni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa tahadhari ya ugonjwa wa ebola, kwa wananchi wote wa mikoa ya Tanzania na hasa wale waliopo mpakani na nchi jirani ya Uganda. Mikoa hiyo ni Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma na Rukwa.
Taarifa hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina Kikuli, ikiwashauri wananchi kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu, mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Wizara hiyo pia ilitoa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhusu kuwapo kwa ugonjwa huo ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda.
Ugonjwa huo umewapata watu 20 ambao wamepata maambukizo na kati yao 14 wamepoteza maisha, hadi kufikia Julai 29 mwaka huu.
Kwa upande wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imekiri kupokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kuwepo ugonjwa wa ebola ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda, hasa Kanda ya Magharibi ya nchi hiyo.
Aidha, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatoa tahadhari ya ugonjwa huu kwa wananchi wote katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale waliopo katika mikoa inayopakana na Uganda, mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma na Rukwa.
Kuhusu chanzo na dalili za ugonjwa wa ebola, husababishwa na virusi vya ebola huku dalili zake zikiwa homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa na vidonda kooni.
Aidha, mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje ya mwili. Dalili hizo zaweza kuonekana kati ya siku mbili hadi 21 baada ya kupata maambukizi. Kuenea kwake ni kwa kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo, Kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu, kugusa wanyama walioambukizwa kama vile sokwe na swala wa msitu.
Juu ya tiba, kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamnii, hadi sasa ugonjwa huo hauna tiba wala chanjo, hivyo wamechukua hatua madhubuti za kukabiliana nao.
”Tumetoa taarifa ya tahadhari kuhusu ugonjwa huu kupitia kwa waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya. Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, mwongozo kwa watumishi wa sekta ya afya wa namna ya kuchukua sampuli na vipeperushi vinavyoelezea ugonjwa huu.
”Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa wataalamu wa afya katika mikoa, wilaya na maeneo ya mipaka. Aidha, wataalamu wa afya pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu, ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema na kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya.
Sambamba na hatua hizo, wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa hapa nchini.
Aidha, wananchi wameshauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu, mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Source: Tanzania Daima 5/8/2012
 
Duh kumbe JF inasomwa hadi Nyakahanga, Murongo, Bugene, Umugakorongo, Umurushaka, nk.Mimi nilikuwa nikidhani inasomwa Dar, Arusha, New York, Washington DC, London kumbe siyo huko peke yake. Hakika JF ina impact kubwa ya kijamii na kisiasa hapa nchini. Tuitumie kwa weredi na kwa manufaa ya nchi yetu kwa ujumla.
Niko Berrien Springs, US, lakini kila siku napata mpya hapa JF. JF is more than Facebook and twitter
 
Back
Top Bottom