Afghanstan mambo bado ni moto!

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,518
1,086
Kwa hali kama hii si rahisi vita kuisha mapema

afghanistan.jpg
 
hii ni mithiri ya mbeya, ni nzuri kwasababu inapelekea watu kuheshimiana, tz nasi tunaelekea huko, better tujiandae.
 
attachment.php



Na bado... hesabu ni billion ngapi kwa siku zinapotea huko, sasa jiulize kwanini zisilipwe na Libya, Iraq na kwingineko? kwani hamjuwi uchumi wa dunia unayumba kwanini?
 
Kwa wale ambao tumebahatika kupita katika maeno yaliyopitiwa na vita hasa za wenyewe kwa wenyewe katu hatuwezi kushabikia vita kama njia ya kuleta heshima. Nenda Kongo kaskazini na Kongo mashariki kama Goma na Bukavu, tembelea Rwanda tena usikose kufika Gisozi kwenye jumba la makumbusho la kumbukumbu ya mauaji ya halaiki, tembelea Burundi hasa vijijini ambako walichinjana kama mbwa, fika Siera Leon na Liberia. Kisha jiulize hiyo "heshima" imepatikana? Huko kote kuna watu wanaitwa "Dogs of war" wananchi ambao vita kwao ni fursa ya kujipatia kipato, na wala hawataki iishe. Na kuna "third parts" hawa si wananchi, ni watu wa nje ambao watataka muendelee kuchinjana ili waweze kuwauzia silaha zao, tena wanuza kwa pande zote mbili. Najiuliza tukianza kuchapana ili kujenga "heshima" wakazi wa mikoa kama Dar, Pwani, Moro, Dodoma, Singida kwa kutaja michache watakimbilia wapi kama wakimbizi. Heri yao waishio mipakani itakuwa rahisi kwao kuvuka mipaka. Kumbuka tutakapokuwa tunakimbia vita hatutapanda magari! ni kwa miguu. Sasa fikiria unafyatua mbio tena peke yako ukiwa peku maana hutakumbuka familia kama ambavyo ilivyokuwa wakati wa mabomu ya Mbagala na Gongolamboto. Unatoka Dar mpaka Mombasa kupitia Bagamoyo, Pangani, Tanga hadi unafika kwenye kambi ya wakimbizi ndani ya ardhi ya Kenya.
 
Tusipokuwa makini haya mambo ya kulipua mabomu kwenye magari na hata katika taasisi nyeti yatatokea hapa nchini kwet maana tumekwishaanza kuona mifano,Mungu atuepushe na janga kama hili.
 
Back
Top Bottom