Afariki Baada Ya Mahojiano Na Polisi Ukonga - Hii ni sawa?!

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Polisi wa ukonga hapa Dar, jana wamemchukua raia nyumbani kwake jioni, na kwenda naye kituoni kwa mahojiano, ndugu zake walipoenda kesho yake wakaambiwa kuwa ndugu yao, amepata homa hivyo kalazwa amana, walipoenda amana wakakuta amefariki.

Kamanda wa polisi wa Ilala alipoulizwa na redio wapo jana jioni alisema kuwa huyo raia wakati anahojiwa iligundulika kuwa ana homa hivyo akapelekwa hosp. na kufariki. Je ni sawa?
 
Last edited:
Je haya mahojiano yaliisha au hayakuisha? Na je mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi ili kubaini kama kuna unyanyasaji wowote alifaofanyiwa marehemu? na baada ya kupata majibu kwa hayo maswali nahisi tunaweza tukapata mwanga katika kuchangia mada hii,ili tusikurupuke kujibu naomba mleta habari atupe full information ili tuweze kuchangia vizuri.
 
Nafikiri madaktari wtakuwa na nafasi nzuri sana kueleza hilo baada uchunguzi wao wa kitabibu
 
Back
Top Bottom