Kama sikosei KKKT Makao makuu chini ya Dk Alex Malasusa haijatoa tamko la Kuunga mkono au kupinga tiba itolewayo na Mchungaji Mwaisapile. Nafikiri uamuzi huu ni wa busara na hii pengine nikatika kujiridhisha kuwa jambo hili linaukweli kwa kiasi gani. Ni kweli kuwa Mungu hana mipaka na anaweza kufanya au kumtumia mtu yeyote ili kudhihirisha ukuu wake, hata hivyo nafikiri sio vibaya kuthibitisha shuhuda ambazo zinatolewa na wale ambao wameshatumia kikombe hicho. Pengine kiroho sio vizuri kupinga lakini katika uhalisia ni vizuri kujiridhisha maana uwezekano wakufanya hivyo upo.
Mimi binafsi nimekutana na watu kadhaa ambao wamekuwa wakishuhudia kuwa wamepata nafuu baada ya kunywa kikombe hicho hata hivyo nahisi moyoni mwangu bado niko na shauku ya kuthibitisha ushuhuda huo. Nafikiri sio dhambi kwani hata bwana yesu alipofufuka kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa na shaka baada ya kumuona Bwana yesu amesimama mbele yao, hili halikumfanya yesu asiwaambie waguse makovu waone alama za misumari na mkuki, alipofanya hivyo aliwatoa shaka waliokuwa nayo. Nafikiri hili ndilo linalofanywa na KKKT makao makuu maana kama sikosei waliounga mkono kwa mikono miwili dawa ya mchungaji mwaisapile ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini inayoongozwa na Askofu Laizer. KKKT makao makuu isitie neno kwenye hili mpaka itakapojiridhisha kuwa hao waliokuwa na matatizo ya kweli wamepona Hii inamaana kubwa sana mbele ya safari.