Aenda Kwa Daktari wa Meno, Apoteza Jicho Lake

mtwana

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
428
140
Mtoto wa miaka 7 wa nchini Cyprus aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya meno amepoteza jicho lake baada ya daktari wa meno kumdondoshea dawa ya ganzi kwenye jicho lake.
Kwa mujibu wa magazeti ya Cyprus, mtoto huyo alipelekwa na wazazi wake hospitali alipokuwa akisumbuliwa na maumivu ya jino.

Wakati akiwa hospitali, daktari wa meno alitoa dawa ya ganzi na kumuonyesha mtoto huyo na wazazi wake dawa ya ganzi atakayotumia.

Wakati akifanya hivyo kwa bahati mbaya matone ya dawa hiyo yalidondokea kwenye jicho la mtoto huyo na kupelekea mtoto huyo apoteze nuru ya macho yake.

Mtoto huyo aliwahishwa kwenye kitengo maalumu cha macho kwenye hospitali hiyo hiyo ya serikali lakini juhudi zao za kuliokoa jicho la mtoto huyo zilipokuwa zinafeli mtoto huyo aliwahishwa kwenye hospitali binafsi ambako huko pia madakatari walishindwa kuliokoa jicho la mtoto huyo wakisema kuwa amecheleweshwa sana kupewa tiba hivyo hakuna kinachoweza kufanyika kulikoa jicho lake.

Kwa mujibu wa magazeti ya Cyprus, wazazi wa mtoto huyo wamemfungulia mashtaka daktari wa meno na daktari wa macho kwenye hospitali hiyo.


Napenda kuuliza wanaJF hivi ingekua kwetu ingekuaje au ndio watasema ni kosa la kibinaadamu?
 
Mtwana thread yako ilifaa uweke kwenye hoja mchanganyiko na siyo hapa.ninapita tu tutaonana baadaye.
 
So sad!
Mods peleka hii thread kunakohusika. Hapa ni mambo ya vitu vizito vyenye ncha kali tu
 
Back
Top Bottom