Advocate Maira is no more!

Astaghfirullah, astaghfirullah, astaghfirullah, mswalie mtume.

Namkumbuka wakili Maira alijitolea bila malipo kuichukua kesi ya vijana wa Sekondari ya Tambaza waliokumbwa na tafrani ya fujo za mpirani mwaka 1993.

La ilaha illallah.


unaongela wale vijana waliosababisha O level ikafutwa tambaza ..Kina ...komando PUZZA..., muro,,..,mtoto wa KIARO[jenerali]....

walikuwa balaa wale
 
mwenyezi Mungu amjalie makazi ya milele!
Duh, eti wataalam wa milingotini wanasema amelogwa na mtuhumiwa Zombe! msiniulize source wakuu!
 
Mwili wa Wakili Maira kurejeshwa Aprili 30

Wednesday, 22 April 2009 16:07

Na Makumba Mwemezi
MWILI wa aliyekuwa wakili katika kesi ya Abdallah Zombe, marehemu Moses Maira (66) aliyefariki dunia juzi nchini Marekani alikokuwa kwa matibabu unatarajiwa kuwasili nchini Aprili 30 kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu Dar es Salaam jana, Msemaji wa familia Bw. Semba Wilson alisema awali walitarajia kusafirisha mwili wa marehemu kesho ambapo ungefika Jumapili lakini kutokana na ndege kujaa wamepangiwa Aprili 28 ambapo ndege itafika nchini Aprili 30.

Alisema taratibu za mazishi zinaendelea vizuri na kuwa Marehemu anatarajiwa kuzikwa Dar es Salaam mara baada ya mwili kuwasili.

Marehemu Maira ndiye aliyekuwa wakili katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam ambapo anatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro pamoja na dereva teksi wa Dar es Salaam.

Kifo cha wakili wa Zombe kimekuja siku chache baada ya kifo cha aliyekuwa mshitakiwa na shahidi muhimu katika kesi hiyo ya mauaji marehemu Koplo Rashid Lema aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani.

Akimzungumzia wakili Maira, mkwe wa marehemu ambaye pia ni Wakili katika kampuni ya Membar Law Attorneys, Bw. Yassin Membar alisema alikuwa mchapakazi mwenye upendo na moyo wa kusaidia.

Source:Gazeti la Majira.
 
Kwa sababu mtoto wake alikuwa anasoma Tambaza pia. Alikuwa na sababu binafsi za kutetea ile kesi. Lingine?

Mzee Maira alishindwa kuwa mfano wa maadili kama wakili mwandamizi pale alipolegalega kimwenendo mpaka kukanywa na Tanganyika Bar Society akibishana na Nimrod Mkono magazetini ni yupi mwenye akili zaidi, na nani anamzidi mwenzake hela. Baadhi ya tuliotafuta mwongozo kwa hawa Wakubwa wetu tuliangushwa.

This is what i call cheap arguments. whto is parfect? We all make mistakes once, twice or more in our life time. I don't think at this moment it's matter if he was weaker or stronger, rich or poor. What matters is condolences to the family of advocate Maira.

Please spear your argument for the next topic.
 
Update toward Msiba.
The body of marehemu Moses Maira utaondoka Bush Intercontinental Airport siku ya Jumanne kwa ndege ya KLM na kufika Dar siku ya Alhamisi.
 
Mwili wa Wakili Moses Maira wasafirishwa leo kutoka Houston Texas kuelekea dar kwa mazishi, hii nimeipata kwa ndugu wakaribu wa Maira. Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi na awape wafiwa utulivu wa roho.
 
Moses Maira was one of the most courageous lawyers to grace the Tanzania landscape. It reminds me of how he locked horns against the government in the VAllambia case in which he won but the govt.refused to pay the late Vallambia!! RIP advocate Maira. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom