Adui yetu Namba Moja ni Umasikini!!

Naweza kukubali ni one way kwamba 'Tumeishi kwenye Umaskini mno kiasi cha kuamini kuwa kiongozi mzuri lazima naye awe maskini'..Na hili tatizo litatugharimu sana huko mbeleni!..Hii ni kwa sababu akili zetu hazijafunguka kuukubali mfumo wa Kibepali ambao ndio unaotawala dunia kwa sasa!..Mawazo yetu yamekuwa ya kimaskinimaskini sana..Lazima tufike wakati tukubali kuwa kuishi kimaskini na kifisadi yote ni makosa!!

Kinachotakiwa ni kubadili 'mentality' kwanza!..Hata kama tutabadili vyama kwa akili hii lazima tushikane uchawi kwa muda mfupi ujao!..Kama alivyosema Mh.Mbatia 'Let us think globally and act locally'..

Chifu kwani ubepari ndiyo mfumo unaotumika na Tanzania?! Imeandikwa wapi? Kwenye katiba ya CCM au JMT?!
 
@ W'S EXPERIENCE: Tatizo moja kubwa Tanzania ni UMASIKINI, we are too poor kuweza ku-deal seriously na matatizo mengine, Umasikini huanzia kwenye mali na ukiwa un checked huamia kwenye akili, masikini mmoja hawezi kumsaidia masikini mwingine kutoka kwenye umasikini waliomo, na kama Serikali haikuwasaidia kutoka kwenye ule umasikini, watailazimisha Serikali nayo kuwa masikini kama wao, so serikali yetu masikini hatukuipata kwa bahati mbaya!!

Willie! @ Facebook!!!

Adui wetu wa kwanza ni CCM ndio aliyeuleta umaskini kwa walalahoi.
 
Chifu kwani ubepari ndiyo mfumo unaotumika na Tanzania?! Imeandikwa wapi? Kwenye katiba ya CCM au JMT?!
Pia sijui nani kasema ubepari ndo mfumo mzuri?watu hawafuatilii halafu mnasema mna exposure na ubepari,mnayafuatilia vyema ya wakongwe wa ubepari SnowBall et al?Hata wenyewe wako kwenye struggles za ku go through changes.Kuna watu waliozaliwa na kuishi ndani ya ubepari vizazi vyao vyote na sasa wana uquestion,kuna waliodai Obama alikuwa socialist,na kila wakisema hivyo ndo kwenye polls anaenda juu, sasa jiulize.Hao 99% wanaupigia mfumo upi kelele?kila mara kwenye mataifa hayo,wakati mabepari wakubwa wanaufanya huo ubepari wao,wakikwama,uchumi wa dunia unayumba na pia wa mataifa hayo,na anayewakomboa ni bailout ya walalahoi ama taxpayers kwa ujumla.Na nina uhakika kama si hizo ninazoziita socialistic programs ambazo kwa wenzetu zinapungunza unyama wa matokeo ya ubepari,basi kungekuwa na revolution...
 
Last edited by a moderator:
Chifu kwani ubepari ndiyo mfumo unaotumika na Tanzania?! Imeandikwa wapi? Kwenye katiba ya CCM au JMT?!

Sijui kama unaishi Tanzania..unajua kitu inaitwa 'cost sharing'?..Sidhani kama unahitaji kuona kwenye Katiba za vyama au ile ya JMT ndio ujue mfumo tunaoenda nao hapa Tanzania ni Ubepali. Kama unayajua mambo ya 'soko huria' a.k.a 'utandawazi' huwezi kuuliza swali kama hili!..Ndio tunachoongelea hapa kwamba hata hawa 'viongozi' wanaoziandika hizi katiba wanajaribu ku'reason' kimaskinimaskini'..yaani hawataki kuwa 'realistic'. Wanaweka vifungu kwenye katiba ambavyo wanajua havina maana but kwa sababu wanajua mtanzania maskini akikisoma atafurahi basi wanakiacha..Hivi kwa akili yako unaamini maisha tunayoishi ni ya siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA????
 
Pia sijui nani kasema ubepari ndo mfumo mzuri?watu hawafuatilii halafu mnasema mna exposure na ubepari,mnayafuatilia vyema ya wakongwe wa ubepari SnowBall et al?Hata wenyewe wako kwenye struggles za ku go through changes.Kuna watu waliozaliwa na kuishi ndani ya ubepari vizazi vyao vyote na sasa wana uquestion,kuna waliodai Obama alikuwa socialist,na kila wakisema hivyo ndo kwenye polls anaenda juu, sasa jiulize.Hao 99% wanaupigia mfumo upi kelele?kila mara kwenye mataifa hayo,wakati mabepari wakubwa wanaufanya huo ubepari wao,wakikwama,uchumi wa dunia unayumba na pia wa mataifa hayo,na anayewakomboa ni bailout ya walalahoi ama taxpayers kwa ujumla.Na nina uhakika kama si hizo ninazoziita socialistic programs ambazo kwa wenzetu zinapungunza unyama wa matokeo ya ubepari,basi kungekuwa na revolution...

Chifu umeongea kitu cha maana sana hapo mwisho.
Hawa wanaopigia chapua ubepari hapa kwetu,wanaamini kwamba kuna nchi ambayo inafuata mfumo wa ubepari kwa asilimia 100.
Nchi kama Marekani na nyingi za Ulaya (ambazo zipo chini ya 'ubepari) zenyewe hazina ubepari wa asilimia 100. Nchi hizo zina mifumo kama Medical Care, Medicaid (Health Care), unemployment benefits, agro subsidies, social security, public transport systems (ambazo zinakuwa subsidised na serikali kwa kiwango kikubwa ili kutoa huduma nzuri ya usafiri kwa umma) n.k. Hii yote ni mifumo yenye chembechembe za kijamaa wa kiwango kikubwa, na inafanya kazi katika nchi za kibepari.

Ndiyo maana uwa naamini ili kuwa na mfumo mzuri wa kuendesha serikali ni vyema ukawepo mchanganyiko wa ujamaa na ubepari - kutumia mazuri ya ujamaa na ubepari katika kupunguza madhaifu ya kila mfumo ili mwisho wa siku mchanganyiko huo uweze kuleta faida kwa taifa.

Lakini kwa namna serikali hii ya CCM inavyoparamia ubepari kwa asilimia 100 na kuacha jukumu la maendeleo na ustawi wa jamii na wananchi liwe la sekta binafsi na soko huria; hakika haifahamu ilitendalo!
 
Naweza kukubali ni one way kwamba 'Tumeishi kwenye Umaskini mno kiasi cha kuamini kuwa kiongozi mzuri lazima naye awe maskini'..Na hili tatizo litatugharimu sana huko mbeleni!..Hii ni kwa sababu akili zetu hazijafunguka kuukubali mfumo wa Kibepali ambao ndio unaotawala dunia kwa sasa!..Mawazo yetu yamekuwa ya kimaskinimaskini sana..Lazima tufike wakati tukubali kuwa kuishi kimaskini na kifisadi yote ni makosa!!

Kinachotakiwa ni kubadili 'mentality' kwanza!..Hata kama tutabadili vyama kwa akili hii lazima tushikane uchawi kwa muda mfupi ujao!..Kama alivyosema Mh.Mbatia 'Let us think globally and act locally'..

Snowball, inawezekena hatujafunguka kimawazo na kukubali mfumo wa kibepari, lakini bado hii inarudi pale pale kwenye visionary leadership na governance system. Tanzania haijawahi kuwa chini ya uongozi wa chama kingine tofauti na TANU/CCM. Hivyo taifa limejengwa na kuongozwa kwa misingi ya chama tawala. Hadi sasa hivi angalia katiba ya CCM na ideology yake. It is full of contraditions.

Kama dunia imebadilika na uongozi wa nchi ukaona mabadiliko hayo yanagusa 'socio-economic fabric yetu' kwa nini wasi-reflect kwenye mfumo mzima wa uongozi including katiba ya chama (sio ya nchi) ambayo ndiyo technically ndiyo inaegemewa sana kwenye utaratabu wa uongozi?

Hili swali la ideology liliibuka wakati wa uchaguzi mkuu 2010 na hizi contradictions zilijitokeza lakini bado hakujafanyika jitahada za makusudi kuuondoa huu utata. Kuna relationship ya karibu sana kati ya ideology na behaviour upande wa umma.

Kwa hiyo tukisema wananchi wanaamini kuwa kiongozi anatakiwa awe mtu masikini mimi noana (under current conditions) wako sawa kwa sababu waliopo wanaaminisha watu hivyo. Pia sikumbuke ule mkakati wa rais wa kuweka sheria inayotenganisha uongozi na biashara uko vipi? Nadhani kukiwa na clear guidelines/principles za uongozi pengine watu wanaweza kuwa na mjadala tofauti. Kwa sasa wanajadili based on what they have been made to believe!
 
Sijui kama unaishi Tanzania..unajua kitu inaitwa 'cost sharing'?..Sidhani kama unahitaji kuona kwenye Katiba za vyama au ile ya JMT ndio ujue mfumo tunaoenda nao hapa Tanzania ni Ubepari. Kama unayajua mambo ya 'soko huria' a.k.a 'utandawazi' huwezi kuuliza swali kama hili!..Ndio tunachoongelea hapa kwamba hata hawa 'viongozi' wanaoziandika hizi katiba wanajaribu ku'reason' kimaskinimaskini'..yaani hawataki kuwa 'realistic'. Wanaweka vifungu kwenye katiba ambavyo wanajua havina maana but kwa sababu wanajua mtanzania maskini akikisoma atafurahi basi wanakiacha..Hivi kwa akili yako unaamini maisha tunayoishi ni ya siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA????

Chifu hapo ndipo penye shida. Kama taifa lazima mfumo unaotumika katika kusukuma maendeleo ya nchi utambulike wazi. Na chombo pekee cha kutoa utambulisho huo ni katiba - kwani kwa kuwa imetambulika kwenye katiba, hata sera na sheria nazo zitatungwa na kutekelezwa kwa kuzingatia msingi mkuu uliowekwa wazi kwenye katiba.

Hatuwezi kuwa na taifa liloendeshwa kwa hisia na kuiga mambo bila kurasimishwa kikatiba na kisheria. Kwani kwa namna hiyo itakuwa ni vigumu kufanikisha uwajibikaji kwa wananchi kwa ujumla.

Chifu unataka wawe 'realistic' kwa kufanya nini? Kwa kuparamia ubepari?
Hivi katika dunia ya sasa unaweza kunitajia taifa ambalo linaamini katika ubepari kwa asimilia 100?!

Ebu viandike hapa hivyo vifungu vya kwenye katiba ambavyo havina maana!

Chifu narudia tena katika suala la mfumo wa kuendesha nchi, ondoa suala la kuishi kwa imani; kwani tuna katiba na sheria ambazo ndizo zinapaswa kutuongoza - hivyo ukiona vyote hivyo havitoi miongozo inayoendana na hali halisi ujue hapo kuna shida, tena kubwa sana.
 
- Unajua through my research nimegundua kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani, ambayo wananchi wake wana majumba makubwa ya kifahari lakini hayakujengwa kwa mikopo toka benki, ha! ha! ha! ha! yaani it is incredible!!Willie!
aliyekwambia kukopa lazima nani?kama unaweza kulipa cash haina haja kukopa.kukopa ni mfumo uliotengenezwa ili uhisi unamiliki kitu wakati sio chako.ulikuepo Marekani umeona mortgage ilivyozingua watu.usiige kila mfumo.ndo maana serikali ya chama chenu mnaambiwa mpaka mfanikishe jinsia moja waoane kwa sababu ya mikopo.nakuhakikishia litafanikiwa.SHIDA NI CCM WANANCHI TUNAHANGAIKA KUTAFUTA NA KULIINGIZIA TAIFA KIPATO WATU WANAIBA,SHERIA ZINAZINGUA.KAIBIWA MALIMA LAPTOP HOTELINI IMEPATIKANA KAPIGWA ULIMBOKA KAKAMATWA CHIZI.WHERE U R TAKING THIS COUNTRY TUTAFIKA INSHAALAH.
 
snowball, inawezekena hatujafunguka kimawazo na kukubali mfumo wa kibepari, lakini bado hii inarudi pale pale kwenye visionary leadership na governance system. Tanzania haijawahi kuwa chini ya uongozi wa chama kingine tofauti na tanu/ccm. Hivyo taifa limejengwa na kuongozwa kwa misingi ya chama tawala. Hadi sasa hivi angalia katiba ya ccm na ideology yake. It is full of contraditions.

kama dunia imebadilika na uongozi wa nchi ukaona mabadiliko hayo yanagusa 'socio-economic fabric yetu' kwa nini wasi-reflect kwenye mfumo mzima wa uongozi including katiba ya chama (sio ya nchi) ambayo ndiyo technically ndiyo inaegemewa sana kwenye utaratabu wa uongozi?

Hili swali la ideology liliibuka wakati wa uchaguzi mkuu 2010 na hizi contradictions zilijitokeza lakini bado hakujafanyika jitahada za makusudi kuuondoa huu utata. Kuna relationship ya karibu sana kati ya ideology na behaviour upande wa umma.

Kwa hiyo tukisema wananchi wanaamini kuwa kiongozi anatakiwa awe mtu masikini mimi noana (under current conditions) wako sawa kwa sababu waliopo wanaaminisha watu hivyo. Pia sikumbuke ule mkakati wa rais wa kuweka sheria inayotenganisha uongozi na biashara uko vipi? Nadhani kukiwa na clear guidelines/principles za uongozi pengine watu wanaweza kuwa na mjadala tofauti. Kwa sasa wanajadili based on what they have been made to believe!

- hapa ndipo ninaposhindwa kuielewa jf, system haiwezi kuwabadili wananchi wasiotaka kubadilika badala yake wanataka majungu tu asubuhi mpaka jioni, toka tushike uhuru yamesemwa mengi sana kiongozi flani hafai flani anafaa, sasa waliowahi kufaa semeni waliweka nini cha maana kuwasiadia wananchi kuondokana na umasikini, ambalo ndilo tatizo letu namba moja?

- umasikini ukikuingia kwenye akili huwezi kufikiria sawa sawa na infact mara nyingi huwa unaishia kuukata mti ulioukalia, mimi nawajua wananchi wengi waliojaribu kushauri njia za kujitoa taifa na umasikini, wakaishia kupigwa vita na hii society wee na wengi mpaka leo wapo wakijaribu tu ni vita tuu!!

- chadema wanasema wanataka kuleta maendeleo na kuondoa umasikini, lakini matendo ya viongozi wao n i very clear kwamba ni mabepari, wapo ki-individual zaidi kuliko jumuiya, so tutaendelea kzunguka na kutafutana uchawi mpaka mwisho wa dunia, lakini until wananchi wetu wamebadilika na hasa kwenye mind-set zao ni bure tupu!

- tfuike mahali tanzania tuigeuze system ili iweze kutoa miaanya ya wananchi kuwa matajiri bila kutegemea serikali, i mean hapa mjini ni impossiblr kukuta tajiri ambaye hana connections na serikali why?

Willie!
 
aliyekwambia kukopa lazima nani?kama unaweza kulipa cash haina haja kukopa.kukopa ni mfumo uliotengenezwa ili uhisi unamiliki kitu wakati sio chako.ulikuepo marekani umeona mortgage ilivyozingua watu.usiige kila mfumo.ndo maana serikali ya chama chenu mnaambiwa mpaka mfanikishe jinsia moja waoane kwa sababu ya mikopo.nakuhakikishia litafanikiwa.shida ni ccm wananchi tunahangaika kutafuta na kuliingizia taifa kipato watu wanaiba,sheria zinazingua.kaibiwa malima laptop hotelini imepatikana kapigwa ulimboka kakamatwa chizi.where u r taking this country tutafika inshaalah.

- kama wananchi hawana access ya kukopa toka benki, basi ni wazi hakutakuwa na mzunguko mkubwa wa pesa kwenye taifa, matokeo ni wananchi waoga kutumia pesa zao, na matokeo ni kutokuwepo kwa pesa zinazonguka kila siku kwenye maisha ya kawaida ya wananchi,

- taifa ni lazima liweke njia rahisi kwa wananchi kuweza kukopa na kurudisha kwa masharti nafuu tena ka mashindano baina ya benki, ndio mambo tuliyoyaona huko majuu, kampuni za simu zinashindana mpaka kunakuwa na sim za bure usiku kuanzia saa tatu usiku, kutokuwepo kwa mikopo na masharti nafuu yake ni kosa kubwa sana la kukosa maendeleo kwa taifa!!

- huwezi kuendelea bila system ya mikopo katika taifa, nyumba za kukopa na kodi za property ni muhimu sana hasa kwa local government kuendesha shuguli zake, taifa halina tolls bridges leo 2012? Sasa una maintain vipi bara bara bila tolls? Bara bara na madaraja vinatakiwa viji-maintan vyenywe through tolls!!

Willie!1

willie!!
 
-

- chadema wanasema wanataka kuleta maendeleo na kuondoa umasikini, lakini matendo ya viongozi wao n i very clear kwamba ni mabepari, wapo ki-individual zaidi kuliko jumuiya, so tutaendelea kzunguka na kutafutana uchawi mpaka mwisho wa dunia, lakini until wananchi wetu wamebadilika na hasa kwenye mind-set zao ni bure tupu!

Willie!

Huwezi kuongoza nchi on ad-hoc basis. Niambie ni nchi gani inafuata mfumo wa kidemokrasia ambayo ina vyama visivyosikuwa na ideology? Na kwanini kwenye vyama vya siasa ideology inakuwa central?

On the red: yes, kwa sababu CHADEMA wanfuata mrengo wa kati (a mix of the two, left +right). Wakati CCM bado kwenye katiba yao wanaonekana to the far left! which is in my view a white lie. maana hakuna u-left wowote kwenye ccm but they keep on singing that old lie.
 
@ W'S EXPERIENCE: Tatizo moja kubwa Tanzania ni UMASIKINI, we are too poor kuweza ku-deal seriously na matatizo mengine, Umasikini huanzia kwenye mali na ukiwa un checked huamia kwenye akili, masikini mmoja hawezi kumsaidia masikini mwingine kutoka kwenye umasikini waliomo, na kama Serikali haikuwasaidia kutoka kwenye ule umasikini, watailazimisha Serikali nayo kuwa masikini kama wao, so serikali yetu masikini hatukuipata kwa bahati mbaya!!

Willie! @ Facebook!!!
ni vema kabla ya kumtaja adui yetu kuwa ni umasikini, tujiulize kwa mapana umasikini ni nini?.Le Mutuz, karibu tujadili hili kwanza
 
- hapa ndipo ninaposhindwa kuielewa jf, system haiwezi kuwabadili wananchi wasiotaka kubadilika badala yake wanataka majungu tu asubuhi mpaka jioni,

System inaweza kuwabadili watu kama watu wakiona kweli system inafanya kazi kisawasawa. Sasa kwa system iliyopo huwezi tegemea watu watabadilika - kwani kila mtu sasa anaweza kuiba tu katika mahala pake pa kazi - kwani hivyo ndivyo system nzima inavyo-operate chifu. Kukiwa na uwajibikaji wa kweli kuanzia kwenye ofisi ya rais hadi ya kijiji, hakika nakwambia chifu, kila mtu atakuwa mwajibikaji, kwani husipokuwa hivyo rungu la sheria linachukundua mkomndo wake. Sasa unataka tubadilike vipi wakati serikali ya CCM inalea wezi na mafisadi - inawatuhumu kwa ufisadi, halafu serikali hiyo hiyo inawapa nafasi nyeti za uongozi - halafu pia inafukuzisha kazi na kuwaacha wanadunda mitaani!! Seriosly chief?!?

chadema wanasema wanataka kuleta maendeleo na kuondoa umasikini, lakini matendo ya viongozi wao n i very clear kwamba ni mabepari, wapo ki-individual zaidi kuliko jumuiya

Chifu husiogope, taifa likiwa na katiba na sheria zinazoeleweka - katiba inatamka wazi itikadi ya taifa - ubepari, ujamaa au ubepari + ujamaa (mchanganyiko) - kunakuwa hakuna shida; kwani sheria na kanuni zake zitaweza kuwanyoosha viongozi wote wanaoenda kinyume na maslahi ya taifa.

tufike mahali Tanzania tuigeuze system ili iweze kutoa mianya ya wananchi kuwa matajiri bila kutegemea serikali, i mean hapa mjini ni impossible kukuta tajiri ambaye hana connections na serikali why?

Willie!

Kwa sababu serikali hii ya CCM ndiyo inataka utaratibu huo! Mfumo ulikuwepo ni kwamba ukiwa tajiri lazima uegemee upande wa serikali ya CCM, la sivyo utatengenezewa mizengwe ya kila aina - oh unadaiwa kodi toka ulipoanza biashara n.k. - Pia ukiwa tajiri na ukawa upande wa serikali ya CCM, dili zako nyingi zitafanikiwa - utalipa kodi inavyotakiwa n.k. Siku ukienda kinyume na serikali wanakubana na kudai ulikuwa hulipi kodi - yupo wapi Majige wa Mwanza!!!??
 
- The point ni Tanzania tunawezaje kuwa na wananchi wenye majumba mengi ya kifahari ambayo hayakujengwa kwa njia za mikopo toka benki? Sasa kama huna system ya mikopo, Serikali itapata wapi kodi za kuwaletea wananchi wake maendeleo?

- Hayo mengine sio muhimu na wewe unaweza kuyafanya sio kusubiri nikufanyie kila kitu ndio maana tunakuwa masikini bro, kutegemea kufanyiw akila kitu!!

Willie!!

Ni percent ngapi ya Watanzania katika hiyo reasearch yako wewe umeona wana majumba ya kifahari? Na kwa mtazamo wako wewe ni nyumba ya namna gani unaweza kui qualify kuwa ya kifahari?
 
The B, vipi za masiku??

Kutoka kwenye maneno yako haya nakumbuka maneno ya jamaa angu mmoja alisemaga kuwa "Hii nchi ipo perfect kabisa ila kuna kijisehemu kidogo tu mtu/watu anatakiwa akitwist, yaani kidude kidogo tu ukikisogeza tu hivi, mambo mengineee yooote yanakuwa saaafi"

Nilicheka sana na sikumuelewa, ila hapa umeiweka clear sana!

hahaha
Na mimi umenichekesha mzee!! lakini kuna ukweli kuna kakitu kadogo tu tunatakiwa kutwist halafu mambo yanakuwa swaafi!!
Lakini naona karibu tuta katwist muda si mrefu!!!
 
@ W'S EXPERIENCE: Tatizo moja kubwa Tanzania ni UMASIKINI, we are too poor kuweza ku-deal seriously na matatizo mengine, Umasikini huanzia kwenye mali na ukiwa un checked huamia kwenye akili, masikini mmoja hawezi kumsaidia masikini mwingine kutoka kwenye umasikini waliomo, na kama Serikali haikuwasaidia kutoka kwenye ule umasikini, watailazimisha Serikali nayo kuwa masikini

kama wao, so serikali
yetu masikini hatukuipata kwa bahati mbaya!!

Willie! @ Facebook!!!

Tatizo kubwa kuliko yote ni umaskini wa Akili! na hili limeletwa makusudi na watawala ili waweze kuendelea kutawala! Elimu duni kwa watoto wa familia maskini, shule za kata , watoto kukaa chini au chini ya miti wakati wanasoma ni kuwaandaa kisaikoloji wajione wao ni duni na kutazitambua haki zao za msingi hivo kuwapa rulling class( mafisadi/magamba) upenyo wa kuendelea kutawala!
Utajiri wa mali haupo Tanzania! tuna madini ya kila aina, ardhi kubwa yenye rutuba, watu wengi na utulivu wa kisiasa, maji ya maziwa,mito na bahari, mbuga za wanyama, mlima mrefu , binadamu wa kwanza aliishi hapa(kivutio cha utalii) gesi nyingi, n.k kinachokosekana ni utajiri wa akili zetu wa kutumia rasimali hizo!
 
Chifu umeongea kitu cha maana sana hapo mwisho.
Hawa wanaopigia chapua ubepari hapa kwetu,wanaamini kwamba kuna nchi ambayo inafuata mfumo wa ubepari kwa asilimia 100.
Nchi kama Marekani na nyingi za Ulaya (ambazo zipo chini ya 'ubepari) zenyewe hazina ubepari wa asilimia 100. Nchi hizo zina mifumo kama Medical Care, Medicaid (Health Care), unemployment benefits, agro subsidies, social security, public transport systems (ambazo zinakuwa subsidised na serikali kwa kiwango kikubwa ili kutoa huduma nzuri ya usafiri kwa umma) n.k. Hii yote ni mifumo yenye chembechembe za kijamaa wa kiwango kikubwa, na inafanya kazi katika nchi za kibepari.

Ndiyo maana uwa naamini ili kuwa na mfumo mzuri wa kuendesha serikali ni vyema ukawepo mchanganyiko wa ujamaa na ubepari - kutumia mazuri ya ujamaa na ubepari katika kupunguza madhaifu ya kila mfumo ili mwisho wa siku mchanganyiko huo uweze kuleta faida kwa taifa.

Lakini kwa namna serikali hii ya CCM inavyoparamia ubepari kwa asilimia 100 na kuacha jukumu la maendeleo na ustawi wa jamii na wananchi liwe la sekta binafsi na soko huria; hakika haifahamu ilitendalo!

Hawa wanaoupigia chapuo hawajui wanalofanya...kuna siku watarudi kwa aibu kule kule tulikotoka. Ujamaa ulikuwa na matatizo yake tena makubwa tu. Ila hatukutulia na kuangalia namna nzuri ya kurekebisha makosa ya ujamaa. Tukakimbilia kuvaa shati ambalo hatuna hata uwezo wa kulivaa na limewashinda walioliasisis...ubepari
 
Back
Top Bottom