Adui wa mwanamke ni mwanamke

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Habari,

Nakumbuka sana wadada wengi niliosoma nao shule ya msingi na hawakufanikiwa kuchaguliwa na wengi wana watoto wameolewa wengine hawana mbele wala nyuma. Walikuwa na akili za wastani na watiifu kweli mbele ya walimu , walikuwa wasafi wanapendeza na waliwahi sana shule kuliko hata mimi.

Tatizo ni kwamba walimu wa kike waliutumia utiifu wao vibaya wakawafanya hawa watoto wa watu masikini kama ma agent wao wa kuuza ubuyu, pipi, visheti, banzoka nk ndio walimu wa kike hao , je wakikutana na hawa watoto ambao "wamewalostisha' leo hii watawaambiaje?

Walimu wa kike ni asilimia kubwa zaidi kuliko wanaume pengine hata 70% wao wangekuwa mstari wa mbele kumpa mwanamke maendeleo hakika wanawake wangefika mbali.
 
Unatafuta ugomvi na walimu wa kike waliomo humu
Ngoja waje
Na hii hata kule MMU ingefaa zaidi sio huku jukwaa la elimu
 
Back
Top Bottom