Adhabu ya viboko mashuleni - should it be abolished?

Je; adhabu ya viboko iwepo (Kwa Wanafunzi au Wasio Wanafunzi)?

Kama unaunga mkono iwepo ni kwa nini?

Na kama unapinga isiwepo ni kwa nini?
 
kiboko lazma especially kwa students,hiyo ndo adhabu rahisi isiyopoteza muda kwa wote,mwalimu na mwanagunzi,maana ukitoa adhabu nyingine,itahitaji usimamizi,kitu ambacho ni upotevu wa muda
 
Wanapaswa kuwa na kupigwa tu kama wanafunzi juu ya picha hii.
23.jpg
(Picture from here: http://tinyurl.com/6y4rohy)
 
Kuna wakati niliwahi kushiriki katika kampeni ya kitaifa ya kupinga viboko shuleni. Bado nilikuwa sina mtoto. Hivi sasa ninao watoto 2, na nimewahi kumchapa mara moja tu mkubwa wa miaka 8 alipokuwa na umri wa miaka 5. Nilifikia hatua hiyo baada ya kumaliza ushauri nasaha wote. Kosa lilikuwa kumdharau mfanyakazi wa ndani.

Kabla ya kumchapa nilimwambia, masaa 6 kabla ya kumwadhibu, kuwa saa fulani nitakuchapa idadi fulani ya viboko. Nilifikiria kwa kumpa muda angelijirekebisha na pengine kuomba radhi, kinyume chake kabla ya muda nilomwambia, akarudia kosa lile lile. Kwa sababu ninampenda sana, alihisi sitomwamdhibu. Nilimchapa, sio kwa hasira, sio sehemu zinazoweza kumweka alama, na idadi ile ile ya viboko nilivyomwahidi, bila kupunguza wala kuzidisha. Tokea wakati huo amejirekebisha na amekuwa mwalimu mzuri kwa mdogo wake. Nyumbani ipo bakora, pahala pa wazi. Wanajuwa kuwa ninaweza kuitumia wakati wowote ingawa siitumii.

Kwa ufupi, kimsingi ninapinga matumizi ya viboko, (hasa namna ambavyo wazazi na walimu wengine wanatumia, kwa hasira, bila kuweka idadi maalumu ya viboko wala kuchagua wapi pa kupiga), lakini kama mzazi mwenye jukumu la kumlea mtoto wangu, sitosita kuvitumia pale inapobidi.

Kuhusu viboko na nchi za magharibi, nafikiri sasa wanajuta. Uingereza walikuwa na msemo "Spare the rod, spoil the child", lakini kwa kuendekeza haki za binadamu na hasa haki za mtoto, bila ya kuzingatia haki za mzazi, mambo yametoka kwenye udhibiti wao. Ninakubali uwepo wa haki za watoto, ambazo zinapaswa kulindwa kwa kila hali, lakini "haki za mzazi je?". Mtoto kumtukana au hata kumpiga mzazi si kosa, haki zinamlinda, lakini mzazi akijaribu kurekebisha tabia za mwanawe, anaishia korokoroni na pengine hata kunyang'anywa mtoto.
 
Fimbo ni nzuri zikitolewa kwa kipimo na kwa malengo!Mi niliwahi kuchapwa mara moja tu nyumbani kwasababu nilidanganya tangu siku hiyo nikajifunza sio vizuri kudanganya!Ila kuna jirani yetu alikua anamchapa mjukuu wake alafu anamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha kabla hajamtundika huku chini moto unawaka!Yani moshi na joto vyote vyake!Alikua mweupe..akitoka hapo hafai kuangalia!Sasa hayo ni mateso na manyanyaso kwahiyo haki za watoto ziwepo kuwalinda watu kama hao!
 
Hivi kwani watu weusi tu ndio wasio sikia mpaka kwa viboko,mbona wenzetu hawatumii na watoto wananyooka vizuri tu,tujifunze kutumia midomo zaidi ya viboko,nakumbuka nilichukia somo la hesabu kwa sababu ya viboko kama punda kutoka kwa mwalimu wa hesabu akiitwa Njowoka,almaarufu kwa kuchapa,mpaka leo najua kuhesabu pesa tu sasa viboko vimesaidia nini!!!
 
Adhabu ya viboko inatakiwa kwani vijana weingi wasasa hawataki kusoma ila wanataka kufaulu sasa ili hwa madogo wajue kwamba elimu sio sebene lazima wanyukwe viboko ili washike adabu.
 
ADHABU ya viboko kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini inayotolewa na walimu na kuibua malalamiko miongoni mwa wazazi na walezi, haijafutwa kisheria, imeelezwa.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa, Albert Mloka kwenye mkutano wa wadau wa elimu uliondaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Matai wilayani humo.

Mloka alisema adhabu ya viboko shuleni imekuwa ikilaumiwa na wananchi wengi nchini kwa kuwa walimu katika kuadhibu, hawachapi viboko, bali wanapiga wanafunzi kwa mateke, viboko visivyo na idadi, ngumi na vichwa.

“Kinachofanyika shuleni walimu wanakiuka taratibu na sheria zilizoainishwa na Serikali ambapo mbali ya kuwapiga viboko visivyo na idadi kwa wanafunzi wakosefu, lakini pia walimu wa kiume wanawapiga wanafunzi wa kike ambapo sheria haisemi hivyo,” alifafanua Ofisa Elimu wa Mkoa.

Alisema mwanafunzi ataadhibiwa kuchapwa viboko pale itakapobainika kuwa kosa alilofanya ni ovu na adhabu yake ni viboko au kufukuzwa shule na si vinginevyo.

Kuhusu viboko kwa wasichana, alisema wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko na walimu wa kike pekee kama shule haina mwalimu wa kike, basi adhabu hiyo itatolewa na Mkuu wa Shule na Mwalimu Mkuu.

Alisema ni viboko vinne tu vilivyoruhusiwa kisheria kwa wavulana kuchapwa kwenye
makalio na wasichana mikononi na mwalimu akitoa adhabu hiyo, anaagizwa aandike kitabuni kuonesha tarehe na idadi ya viboko na aliyeadhibiwa lazima asaini kitabuni humo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay aliwavunja mbavu wajumbe alipochangia
kwa kusema kuwa “mbona sisi (wanafunzi wa kiume) tunachapwa na walimu wa kike…this is not fair, mie ni Mmasai kule umasaini mtoto wa kiume kucharazwa viboko na mwalimu wa kike looh mwalimu huyo atapewa misukosuko kwa kweli atapata shida,” alisema.

Wajumbe wengi wakichangia walidai kuwa walimu wanaotoa adhabu ya viboko visivyo na idadi shuleni hata kwa kosa la mwanafunzi kushindwa kujibu swali darasani, wengi wao hawana uwezo wa kutosha kufundisha au hawajiandai vizuri kufundisha.

“Si kweli shule zimeharibika, bali walimu baadhi yao wameharibika....viboko sio suluhisho la kumaliza utoro shuleni, walimu wanaotembea na fimbo mikononi kutwa nzima basi ujue wewe si mwalimu,” alisema mjumbe mmoja.

Wajumbe hao pia walishauri kuwa adhabu hiyo ya viboko kwa wanafunzi kamwe isitolewe na mwalimu mwenye hasira kwani atapiga badala ya kuchapa.

Baadhi ya wanafunzi ya Shule ya Sekondari ya Matai walioalikwa hapo, walikiri kuwa adhabu za viboko shuleni zimekithiri na ni mateso kwao.

“Maisha ya shule yamekuwa ni mateso kwetu kwani adhabu za viboko zimezidi baadhi yetu wamekata tamaa ya kusoma na wanahudhuria shule kwa lazima na si kwa hiyari yao wenyewe” alisema mwanafunzi wa kidato cha nne, Paulo Maembe.
 
Mnasahau kuwa fimbo ni moja vichagizo vya mwanafunzi kufaulu. Hakika unaweza kudai utakavyo kuhusu hii adhabu lakini waswahili wasema ukitakusikia utamu wa ngoma ingia ucheze. Kule university tulifundishwa mambo ya theory ya behaviourism kuwa kuna humo punishment na reinforcement. Maana yake ni kubwa sana na sie walimu ndio twajua umuhimu wake.
 
Back
Top Bottom