Naomba maoni yenu na ushauri.
Je ni vizuri au vibaya kumchapa mtoto anapokosea? kwa nini?
je ni vizuri au vibaya kumpa adhabu mtoto anapokosea?
je kuelimisha na kueleza madhara ya kosa kunatosha?
Mimi nilikuwa nachapwa na kupewa adhabu nyumbani na shuleni kadiri wazazi na walimu walivyoona inafaa.
Sasa hivi imeonekana si vyema kuwaumiza watoto na ni budi waelimishwe.
Baada ya kusoma taarifa moja ya mfungwa aliyehukumiwa kifungo, kazi na viboko ilibidi nijiulize, mara kadhaa na kuanza kuwa na mashaka na uamuzi wa kuacha kuwafanyia hivyo watoto wakiwa bado wadogo.
Je, 'mkunje samaki angali mbichi' bado ni msemo unaofaa kwa sasa?
Je kama mtoto anapokuwa mkubwa atapewa adhabu hizohizo kutoka kwa jamii, je mimi kama mzazi, au mwalimu, nikianza kumwonyesha kwa upendo na kumkosoa na kumwelekeza kukiwa kumeandamana na kiboko na adhabu si nitakuwa nimemjenga mapema?
Mzazi au mwalimu anatakiwa amjue mtoto tabia udhaifu na afya yake kwa hiyo adhabu ni rahisi kuipangilia kwa makini zaidi kuliko mahakama ambayo hakuangalii ulikotoka, wanchoangalia ni kosa tu.
Naomba ushauri.