Adhabu ya viboko 12, kwa kosa hili; Hakimu ana wazimu au sheria?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Last Updated on: 15.10.2008 0519 EAT (1205 GMT) (Dar Leo)
•
Achapwa viboko kwa kuchezea nyeti za watoto


Na Rehema Maigala, Kinondoni
MSHITAKIWA Rahimu Issa (22), mkazi wa Sinza amehukumiwa adhabu ya viboko 12 kwa kosa la kuwatia vidole watoto wa kike wawili wenye umri wa miaka ( 8) na (10), bila ya ridhaa yao.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Stahimili Ngwaisya baada ya kuona mshitakiwa anashahili adhabu ya viboko. Mshitakiwa huyo alichapwa viboko vyake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na askari wa Magereza kama ilivyo sheria.

Hapo awali walalamikaji hao walitoa ushahidi wao walidai kuwa, mshitakiwa ilikuwa ni kawaida yake kuwaita nyumbani kwake na kuwachezea sehemu zao za siri na baada ya hapo anawapa sh. 50 kwa ajili ya kununulia pipi.
Walidai kuwa si kwao tu bali ilikuwa hata kwa watoto wengine ambao wao walikuwa hawajaenda kusema kwa wazazi wao.

Kabla ya Hakimu kutoa adhabu hiyo kali alimuamuru mshitakiwa ajitetee ili mahakama impunguzie adhabu itakayotolewa.
Mshitakiwa alidai kuwa yeye ni mtoto yatima hivyo anaomba apunguziwe adhabu itakayotolewa na mahakama hiyo.
''Mheshimiwa Hakimu naomba unipunguzie adhabu kwani hili ndilo kosa langu la kwanza, "alidai mshitakiwa huyo .
Hapo awali imedaiwa kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 4 mwaka huu, Sinza, mshitakiwa aliwachezea watoto wawili wa kike ambao wana umri wa miaka ( 8) na (10).

Swali:
Kama unajua adhabu ya kuwatia vidole watoto ni viboko 12 tu... kuna tishio la kuto kufanya hivyo? Na utetezi wa "mimi mtoto yatima" unatosha kupunguza uzito wa kosa?
 
Kuwaingizia vidole sehemu za siri watoto wadogo(bila ridhaa yao ukilinganisha na umri wao)....lada hivi ndio inaonekana imekaa kiandishi?
 
Hivi kubaka ni pale unapotumia Abdallah bin Kichwa wazi tu? Ukitumia vidole au Ulimi haiwi kubaka? Je ukitumia vibrator? Au Wahaya na yale mapigo yao ya Kater...?? Na kama huo wote ni UBAKAJI, na mtoto mmoja ana miaka chini ya 10, sheria inasemaje? Tuliambiwa kuwa Nguza kwa kosa hili, yeye na wanae wanalilamba kifungo cha maisha. Mie hapa sielewi kabisaaaaaaa. Ngoja nisubiri wana sheria.
 
MKJJ,

Hakimu yawezekana alikula mlungula haiwezekani kuwatia kidole hao watoto wadogo adhabu ikawa viboko 12....Sijui mtuhumiwa lishafikisha kidole cha ngapi katika mkono wake wangemeza dole gumba ingefatiwa kuwanajisi na wanadai ni mchezo wake huyo jamaa tangu siku nyingi...Jamhuri haiwezi kukata rufaa hapa??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom