Adhabu ya kifo ifutwe TZ?

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Wadau, nilikuwa nasikiliza BBC Swahili leo asubuhi na ndipo ilipokuja habari kuhusu adhabu ya kifo kwa upande wa nchi yetu. Takwimu zinaonesha kuwa kipindi cha awamu ya kwanza na ya pili walinyongwa wafungwa 204. Ripoti ikaendelea kusema kuwa awamu ya tatu mheshimiwa Mkapa alitoa msamaha wa wafungwa 101 wa kunyongwa na mheshimiwa Kikwete mpaka sasa 73...

Jeh! Kuna haja ya sheria hii kuendelea? maana ni kama inakiuka HAKI ZA BINADAMU...
 
Hili la adhabu ya kunyonga ni dilema kubwa. Kwa maoni yangu si vema kuifuta. Kuifuta kunaweza kuongeza watu kujichukulia sheria mikononi na kulipiza visasi kwa watuhumiwa wa mauwaji.

Hivi, jaribu kufikiria una bunduki/bastola halafu unamkuta mtu amemchinja mkeo na anamalizia kumchinja mtoto wako kipenzi....unafanya nini hasa ukijua kuwa hata muuwaji huyo akipelekwa mahakamani atafungwa maisha tu na si zaidi ya hapo?
 
Back
Top Bottom