Adha za daladala

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Nimeapa kwa mwendo huu lazima nami nitungue kausafiri kangu soon, by any means necessary. Nimefika Posta saa 12 jioni kufuatilia dili zangu. Nimemaliza narudi kituoni nasubiri gari ya 'kwetu' wala sioni hata moja. Naona tu za Mwenge, Buguruni, G/mboto (nyingi sana), kigogo, n.k. Nasubiri kwa saa zima kituoni. Gari za kwetu zinakuja ila kwa kusuasua tu, na zikija zimejaa. Bahati mbaya siendi 'kwetu' moja kwa moja. Nataka kupitia kwanza Tabata nikamilishe ishu ya leo. Tabata imelaaniwa kwa kukosa gari za Posta. Nasubiri wee....

Kuna kitu kingine nikagundua. %95 ya daladala zinazofika Posta jioni ni za Kivukoni. Ukitaka kwenda kwenu inakubidi kulipa mia 2 hadi Feri ndipo ulipe tena nauli halali ya kwenda kwenu. Konda anakuuliza wakati unatoa nauli, 'unarudi?' u just nod, nae anakata chake.

Nikaona isiwe tabu. Giza limeingia, nami lazima nifike Tabata kukamilisha mzunguko wa siku ndipo niende 'kwetu'. Nikaona gari ya Buguruni nikapanda kuelekea Kivukoni. Kwa kuwa miguu ilikuwa inawaka moto na gari imejaa, nikapata nafasi karibu na dereva, pale inapokaa injiini. Pana joto ila si sana. Nikakaa kutazamana na abiria wenzangu. Konda akadai chake akakata mia 5.

Gari ya kivukoni utaitambua tu kwa shombo la samaki. Basi tukafika Kivukoni na abiria wakashuka tukabaki wa kugeuza na gari. Nikasema sasa nijinafasi. Ile nakaa sawa kwenye kiti ikaja harufu kali ya pombe juu yangu. Nikasema nitazame chanzo. Nikagongana uso na jamaa aliyeonekana kuutwika vyema. Nikajisemea, huyu ndio nitakaa nae hadi Buguruni? Nikamhama kukwepa harufu ya pombe nikahamia siti nyingine ya katikati. Ile nakaa tu magoti yakakwama kukaa sawa. Siti fupi. Nikaona isiwe tabu, nikatoka hapo hadi nyuma ya yule mlei karibu na mlangoni nikakaa dirishani ili nitulie vizuri. Siti hii ikawa sawa na magoti yangu. Urefu wakati mwingine kero. Abiria wakaanza kupanda. Nje nikamwona jamaa mmoja analijia gari letu. Ni kijana tu na anachechemea akijisapoti na fimbo. Akawa anapanda mlango wa daladala kwa shida. Nikajisemea huyu atakaa na mimi tu! Kweli akaja akakaa pale kando yangu. Hakuna hata salamu. Nikaanza kusikia harufu ya nyama ya bucha! Kha! Nikajisemea, hapa hadi Buguruni. Nimemkimbia mwenye harufu ya pombe nikakumbana na mwenye harufu ya nyama. Nikavumilia hadi Buguruni nikashuka nikatafuta usafiri wa Tabata. Nitanunua gari yangu tu!
 
Hahahaha. . . pole bana.
Ila angalau umekua motivated kutafuta usafiri binafsi.Ufanikiwe.
 
hii ndo bongo dukinaa unamwopa anaenuka nyama vp hujawahi kupanda magali yanayotoka feri yamewapakiza wale akina mama na vindoo vyao vya samaki?
 
hii ndo bongo dukinaa unamwopa anaenuka nyama vp hujawahi kupanda magali yanayotoka feri yamewapakiza wale akina mama na vindoo vyao vya samaki?

ningekuwa mwendaji wa feri sana ningeshazoea hali, ila ndo hivyo tena
 
Ndo maisha bora kwa kila mtanganyika hayo..wenzako tushazoea hizo kero..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom