Adha ya usafiri wa daladala

Kelema

Member
Jun 2, 2011
37
8
Hamjambo wana JF?
Naomba tukumbuke ustaarabu wa daladala, miaka ya zamani kulikuwa na UDA-(Shirika la Usafiri Dar). Ukienda kituoni, unapanga mstari. Ustaarabu ulikuwa mkubwa!!!! Mtu aliyetangulia kufik kufika kituoni alipanda kwanza. Sasaa hali ni tofauti, na kikumbo unapigwa. Je, tufanyeje turudie ustaarabu huo???? Mfikirie mama mjamzito, mzee, mgonjwa, mtoto, n.k.
Tujiulize, chimbuko la hali hii hasa ni nini? Kwa mfano unatumia masaa mawili au matatu kutoka Mbezi ya Morogoro road kwenda posta. Ili uwahi kazini, inabidi uamke saa 10 au 10:30 alfajiri. Je, unalala masaa yasiyopungua 8 kwa siku kama inavyotakiwa kiafya? Kama si kufupisha umri wa kuishi ni nini?
Halafu ukiwa katika daladala, ukiangalia pembeni unawaona watanzania wenzio wanakula kiyoyozi kwenye magari yao ya kifahari. Kwa nini daladala zisiboreshwe kama za Ulaya?
Uarabuni wanapandaje daladala kistaarabu, na wameweka upande wa kuketi wanaume na wa wanawake?? Abiria wa Kenya wakizidi wanalipa faini. Huku kwetu kunani? SEMENI JAMANI, TUNAUMIA.
 
Back
Top Bottom