Solomon David
JF-Expert Member
- Mar 1, 2009
- 1,148
- 16
Katika hili ni vema kujua jamii hiyo ina viupa mbele vipi? Pengine hilo la kukaa chini sio kero kwao. Kwani sehemu nyingine wazazi na wafanyabiashara wamekuwa wakisaidiana na serikali zao za mitaa kuondoa tatizo la madawati.
Pengine BUK anaweza kutuambia kama jamaa wa Vingunguti wanaona ni kero kwa watoto wao kukaa chini madarasani. Au wana kero kubwa zaidi ya hiyo kama ya kukosekana kwa mfumo wa maji safi na maji taka, tatizo la takakata, tatizo la vyoo, tatizo la umeme, ujenzi holela n.k
Jamaa wa vingunguti wanatoa kodi kwa serikali. Kazi ya hiyo kodi ni nini kama sio pamoja na kutengeneza madawati?