Adha hii itaisha lini!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
ADHA HII ITAISHA LINI! http://majira.co.tz/index.php?view=...bali&id=1731:adha-hii-itaisha-lini&format=pdf http://majira.co.tz/index.php?view=...hii-itaisha-lini&tmpl=component&print=1&page= http://majira.co.tz/index.php?optio...pY2xlJmlkPTE3MzE6YWRoYS1oaWktaXRhaXNoYS1saW5p Wednesday, 21 October 2009 08:02
mtihani%20wa%20mock.jpg

Wanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Vingunguti katika Manispaa ya Ilala, Dar es salaam wakifanya mitihani ya "mock" wakiwa wameketi sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati unaoikabili shule hiyo. (Picha na Gladness Theonest)
 
ADHA HII ITAISHA LINI! Wednesday, 21 October 2009 08:02
mtihani%20wa%20mock.jpg

Wanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Vingunguti katika Manispaa ya Ilala, Dar es salaam wakifanya mitihani ya "mock" wakiwa wameketi sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati unaoikabili shule hiyo. (Picha na Gladness Theonest)
Na hii ipo Dar, kuna ngapi kama hizi zipo Ludewa, Tunduru, Kakola, Rwamisheni, na pengine popote..???
 
Wadangayika wa nchi hii, embu jioneeni hali hiyo,kwa kweli inasikitisha sana na haya yote ni kwasababu ya wenzetu wachache waliokabidhiwa dhamana ya kulinda raslimali zetu wao wanatafuna tu.Angalia watoto wasio na hatia wanavyo sota sakafuni wakati mitoto yao imepelekwa ughaibuni kula raha!walah, kama moto upo no escaping at all!!inatia uchungu sana kwa nchi yenye rasilimali lukuki kama tanzania.
 
Wakati adha inaendelea kuna watu kama watatu hapa nchi wanachotewa bilioni 40 kila mmoja kutoka BoT!!
 
Na hii ipo Dar, kuna ngapi kama hizi zipo Ludewa, Tunduru, Kakola, Rwamisheni, na pengine popote..???
Nilienda Kilindi na Mkinga wilaya za Mkoani Tanga kuna matatizo kama haya tena makubwa saana. Si kukaa chini tu bali hakuna madarasa kabisa hata ya wanafunzi kukaa na kusoma. Wakati wa mvua wanaondoka na kurudi nyumbani hakuna shule siku hiyo na kipindi chote cha masika. Just imagine halafu tunakaa tunajidanganya kuwa hii nchi kuna amani na usawa wakati rasilimali za muhimu hazigawanywi sawasawa miongoni mwetu. Ni tatizo halafu bado serikali inakaa na kusema imeongeza idadi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi na sekondari. LOL!:(
 
Eee Mungu uturehemu!
Na mtihani huo huo wanafanya st mary's, eden garden etc halafu matokeo yakija hawa wataambiwa wamefeli. Inasikitisha kuuona hali kama hii ndo maana kwenye thread yangu nemesema wanaohusika siku moja watatoa hesabu ya mambo haya.

Adha hii inaweza kuisha pale ambapo wananchi tutaamua kwa dhati sasa kwamba tunataka mabadiliko. Wanaopata nafasi wajue ni kwa ajili ya wengi na si kwa matumbo yao. wananchi tutakapoamua kutumia rasilimali zetu kwa faida yetu. Pale nchi itakapamua kusema madini, wanyamapori, misitu nk ni mali ya watanzania kwa mafaida ya watanzania, pale ambapo watu tutaamua kuacha mabaya na kutenda mema. Hapo, Tanzania yenye neema, maziwa na asali itapatikana na si hizi ndoto za mchana za maisha bora kwa kila mtanzania zilizopambwa kwa maneno matamu pazipo utekelezaji. Mungu utusaidie
 
Mpaka CCM itakapoenguliwa tumepewa mifano mbalimbali hapa shule za nyasi,udongo maboksi matope nakadhalika nakadhalika baada ya miaka 49 haya yote yanatokea ,ni kwa sababu ya uvivu wa ubunifu wa viongozi wetu
 
Kwani hii adha imeanza lini? Ukipata jibu lake ndo unaweza kukisia itaisha lini....
 
Nyie Mtapiga kelele weeeeeeeeeeeeeeeeeeee lakini hizo kelele ni za Chura kwani haziwanyimi usingizi

Angali barabarani Wanatembelea Toyota VX V8 New Module, Thamani yake ni zaidi ya Tshs 100 million.

100milion inaweza kununua madawati mangapi?

Jamani inauma inauma inauma saaaaaaaaaaaaana
 
Mkuu Kibs mimi nadhani inasababishwa na Serikali kutokuwa na vipaumbele vyake sawa sawa. Kikwete aliingia madarakani kwa kuchangiwa mabilioni na mafisadi waliombeba kuingia Ikulu. Mafisadi hao wangeamua kuchanga 20% ya kiasi walichomchangia Kikwete basi adha hii ingeweza kabisa kumalizwa Tanzania nzima.
 
ADHA HII ITAISHA LINI! http://majira.co.tz/index.php?view=...bali&id=1731:adha-hii-itaisha-lini&format=pdf http://majira.co.tz/index.php?view=...hii-itaisha-lini&tmpl=component&print=1&page= http://majira.co.tz/index.php?optio...pY2xlJmlkPTE3MzE6YWRoYS1oaWktaXRhaXNoYS1saW5p Wednesday, 21 October 2009 08:02
mtihani%20wa%20mock.jpg

Wanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Vingunguti katika Manispaa ya Ilala, Dar es salaam wakifanya mitihani ya "mock" wakiwa wameketi sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati unaoikabili shule hiyo. (Picha na Gladness Theonest)

Siku Kikwete akiacha kutumbua mabilioni ya pesa za watanzania akizunguka dunia na wapambe kibao wakifanya shoping za nguvu.
 
Yaani inasikitisha kwa kweli, hivi serikali hii ina nini? Kodi zina fanya nini?Ewe mbunge Makongoro Mahanga unaona lakini?

Wafanyabiashara wa jimbo la ukonga mbona wanatoa kodi, zinaenda wapi?Tanzania jamani kama Dar ndio hali hii, huko vijijini sipati picha. Hii serikali ni uozo na wala haifai, wako tayari kufisadi nchi na sio kuleta maendeleo katika elimu.

Hivi leo huyu mtoto akimaliza shule hapo na kufanikiwa kutoka nje ya nchi hata ukimwambia kurudi nyumbani kujenga taifa atakubali kweli? Nchi gani unatoa kodi wala huoni kazi ya hizo kodi? Ndio maana watu wengine hawataki kuja kuishii hapa bongo kwa mtindo kama huu, nafuu aishi nchi ambayo anatoa kodi na anaona kweli kodi inafanya kazi ya kuleta maendeleo.
 
Patriots wanaotusema kila siku wako wapi? Cost ya kuchonga dawati moja ni kiasi gani?

I'm serious.
 
Hapa tuache kulaumu serikali tu. Hili ni tatizo la jamii nzima. Sasa cha kujiuliza jamii inafanya nini? Kwa nini watu hatu step up to the plate kubadilisha hizi hali? Kwani wazazi wa watoto hao na watu wengine wapenda maendeleo wakikusanya nguvu zao watashindwa kweli kuchongesha madawati au kununua viti vya kukalia hao watoto?

I'm tired of people boohooing govt this govt that....why don't we all step up as a community?
 
Kwa hiyo hii adha iko "bongo" tu na mikoani haipo?

Kwani wewe shule ya msingi ulisoma wapi? Olympio? na je wewe ni mtanzania kweli ambaye hujui hii?

Hili tatizo ni sugu liko miaka kibao zaidi hata ya ishirini sehemu nyingine hii ndio kawaida kama sheria.

Kwa wale waliosoma shule za msingi TZ nadhani mmelizoea na mmetoa michaango ya madawati mara kibao halafu unashangaa linaletwa dawati moja au mawili kuwazuga.
 
Hapa tuache kulaumu serikali tu. Hili ni tatizo la jamii nzima. Sasa cha kujiuliza jamii inafanya nini? Kwa nini watu hatu step up to the plate kubadilisha hizi hali? Kwani wazazi wa watoto hao na watu wengine wapenda maendeleo wakikusanya nguvu zao watashindwa kweli kuchongesha madawati au kununua viti vya kukalia hao watoto?

I'm tired of people boohooing govt this govt that....why don't we all step up as a community?
Katika hili ni vema kujua jamii hiyo ina viupa mbele vipi? Pengine hilo la kukaa chini sio kero kwao. Kwani sehemu nyingine wazazi na wafanyabiashara wamekuwa wakisaidiana na serikali zao za mitaa kuondoa tatizo la madawati.

Pengine BUK anaweza kutuambia kama jamaa wa Vingunguti wanaona ni kero kwa watoto wao kukaa chini madarasani. Au wana kero kubwa zaidi ya hiyo kama ya kukosekana kwa mfumo wa maji safi na maji taka, tatizo la takakata, tatizo la vyoo, tatizo la umeme, ujenzi holela n.k
 
Back
Top Bottom