Aden Rage aomba radhi; hakujua kama silaha iko kiunoni!

Huyu jamaa ana asili ya Somalia aka Al Shabab kwahiyo hayo ndo mambo yao
 
Ndiyo siasa ya kibongo, ukifanya kitu unakikataa. Lakini kile ambacho hutakifanya unasema nitafanya hiki na kile, wizi mtupu jamaa anataka kutufumba macho hapa.
 
Haya ndio maajabu mengine ya Igunga! Mtu hajui kama aliweka silaha kiunoni wakati ukitembea unaisikia ukikaa chini unaisikia sasa iweje yeye asijue kama amebeba silaha ama iliingia kiunoni kwa njia za kishirikina!! Kwanza mikutano yao huwa inajaa wana usalama paoja na hao police ccmC maana ccmB ni CUF nao hawakuiona au kwasababu ni mwana ccm wakaona ni sawa kuonyesha hadharani kana ispekta wa police.

Tujiulize hiyo silaha angepanda nayo jukwani Mbowe,Zitto,Dr.Slaa si wangeletewa hadi ndege za kivita kuwasindikiza police kutoa maelezo!

Serikali na chama chake isiwafanye WATANZANIA wote ni wajinga sasa hivi wana mwamko mkubwa wa uelewa wanatambua kila kitu. Rage amechemka achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi na taratibu za umilikaji wa silaha hakuna cha lelemama sheria ifuate mkondo wake.
 
Hahahah....ile ni chiboko aiseee, alafu meneja wa kampeni anatoa utangulizi, vinjwaji vipo ila unajinunulia, soda, bia, pia chips zinapatikana...hahahah.....wenzao waliweka masinia ya ubwabwa, kweli Igunga kuna mambo!
.

kweli kuna mambo, huo uzinduzi wa kampeni,
nilipoangalia niliishia kucheka tu.
 
Njia ya mwongo ni fupi, anadai eti yeye alikuwa yuko jukwaani anhutubia wananchi, shati likapulizwa na upepo ndo sijui mwenyekiti gani wa magamba yao akaja akamfunika! Ile picha inazungumza yenyewe, hakuwa anahutubia wala nini ila alikuwa amweka mapozi ili bastola ionekane! Isitoshe baada ya gazeti kutoa picha yake, alipofuatwa na waandisha wa habari kuhusu hilo alijibu kwa ngebe kuwa 'mbona hawashangai wamasai kutembea na sime" kwa maana nyingine kwa vile yeye ni msomali ni kawaida kwa Mogadishu kuringishiana silaha! Nyambaf! asidhani kila mtu ana magamba ya ubongo kama magamba yao wanaotaka kuvua!
 
KWa maelezo hayo maana yake
  • Polisi inatakiwa wamuite wamuhoji kwa ufafanuzi zaidi
  • Ikiwezekana anatakiwa apimwe akili na msomgo wa mawazo na mengineyo.......
  • Anatakiwa asiwe na sifa tena ya kumiliki silaha ( kuna sababu zaidi ya tatu )
So kama Polisi hawajamuita kufafanua maelezo, Na aelze kwa nini sifa ya umiliki silaha isifutwe kwake then wasihstuke kusikia miaka ya mbele hiyo silaha imeshaua "viumbe" visivyo na na hatia kama tembo bila sababbu teh teh teh

Good comments inabidi Poilce wafanye kazi yao.
 
anadai upepe ulipeperusha shati hana lolote ukiangalia ile picha inaonyesha alidhamiria kabisa na wala si vinginevyo ameona kimenuka anatafuta sababu tu
 
"Ni bora ukiri tu kuwa mimi ni MSOMALI kwa hiyo nilijisahau nikadhani niko Mogadishu..at least nitakuelewa.."


Mkuu hapo umenena !
 
inaonyesha jinsi gani chama cha magambo kilivyojaa vihiyo ndani yake!!!!!, nnamshangaa hata yule aliyempa kura mtu kama huyu awe kiongozi wake??? kama anasahau silaha iliyopo kiunoni itakuwaje matatizo ya waliomchagua yanayohitaji utashi wa akili???? amakweli kesi ya ngedere kapewa nyani!!! watu kama hawa ndo waleeee wanaonunuliwa suti na kuuza nchi?????, Ila kwa upande wangu sishangai maana kila wa "magamba" akivunja sheria hudai ama hakujua, alisahau, ama huita tume uchwara zichunguze
 
Nadhani ni Tanzania pekeyake ndio unaweza kuomba radhi namna hiyo ukaelewa otherwise yetu macho!!!
 
Pole rage, umejibu vibaya wakati wa kuomba radhi.
  • ooohh upepo ulikua mkali sana
  • oooooh sikujua kama nina silaha
  • oooh sina rekodi mbaya
  • ooooh sasa hivi igunga imechafuka .
mimi majibu yako sioni kama yanaendana na maana ya kuomba radhi
 
Aache mambo ya ajabu yaani kumbe hajui chochote kuhusu silaha ambayo anaitumia kila siku.
 
huyu naye ni mtunga sheria?
hata ajijui kabeba nini? je anaweza kuzijua hoja zake ?
kuna mwingine naye kasema uongo .... yule mgombea wa ccm IGUNGA
KISHA ANASEMA ULIMI ULIMTELEZA
NCHI HII BANA
 
Hii bastola ya Rage ina sifa kama zile za "Always Ultra Thin Pan" maana kwenye adverts promo zake wanasema kuwa wavaaji wanaweza kusahau kuwa wameivaa. Tah teh te
 
Nkikumbukaga huyu mshika bastola Rage alivoimalizaga FAT yeye na swahiba wake Ndolanga...ivi huko kwenye JIMBO lake kuna maendeleo kweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom