Adamu Malima aonja zomea zomea Sumbawanga

Leo watakua hapa Mpanda; nawasubiria kwa hamu,
Namwona DC anahaha kuhakikisha mahudhurio yanakuwa sawa; Nitawapatia updates
 
Vipi mbunge wao Aisha Hirari aliyepigwa chini alikuwepo?????

ha ha ha Aishi hakuwepo alishakimbia mji, aibu aloipata hatajaisahau kamwe tatizo yule jamaa hata ccm hawampendi kabisa angekuwa na umhimu wangeongelea lolote kuhusu yeye hiyo jana!
 
siku nyingine mkuu ptz uwe unatupia mapicha,by the way pipooooooooooooooooooooooooozzzz
 
Sina shaka na taarifa ya Ptz, nimewasiliana na jamaa zangu pale swanga na kusema kweli ni kwamba ccm ina wakati mgumu sana jimboni-sumbawanga. Wanasema pamoja na ugeni mkubwa pale mjini, bado wakazi wa swanga hawakujali hilo na wameendelea na mambo yao. CCM taa nyekundu inawaka swanga.:israel:
 
karibu cdm ndugu yangu,acha porojo za ukanda na udini ambazo ni bora kuliko Ufisadi,Rushwa na ufedhuli ndani ya ccm.
 
Ungeweka picha, Nape asingebisha!

Leo mjini Sumbawanga kulikuwa na mkutano wa hadhara uliotishwa na ccm! Mkutano huu uliongozwa na Nape katibu itikadi na uenezi ccm Taifa, pamoja naye aliongozana na na Mwigulu Nchemba aliyekuwa kinara wa mipasho na matusi kwa viongozi wa Chadema akiwaita wanafiki wakubwa huku akitolea mfano wa Mbowe kukataa gari then baadaye anachukua kimya kimya.

Alikuwepo pia Naibu waziri mawasiliano Charles Tizeba aliyetoa ahadi za ujenzi viwanja vya ndege Sumbawanga na kuwakejeli viongozi wa CHADEM kuwa wana njaa kali kwani ndo wanaokuwa wa wakanza kuchukua posho bungeni, alihutubia pia Prof Jumanne Maghembe waziri wa maji, akafuatia naibu waziri wa Mifugo Benedict Ole Nangolo, wengine waliokuwepo ni Aggry mwanry naibu waziri TAMISEM, Adamu Malima naibu waziri kilimo, na Ezekiel Lwenje naibu waziri ujenzi.

Kali iliyonishangaza kwa wanasumbawanga ni pale walipomzomea Adam malima alipoanza kuwashambulia wale waliomgomea kuitikia wimbo wa alambe kwa kuwanyoshea kidole wote waliomkatalia na kuwaita wachawi ndipo walipoanza kumzomea hatimaye alipanic na kuanza kuelezea megawati za umeme wa Sumbawanga kwa kusema kuwa yeye ndo aliyetatua tatizo la umeme wa Sumbawanga.

Ukiachana na Mh Mwanry aliyewavuta wengi kwa kutoa maagizo kwa kero zilizoibuliwa na Nape huku wakisimamishwa RAS, DC na mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga, wahutubiaji wengine waliotajwa walijaa kutoa ahadi kana kwamba hawako madarakani, maneno kama upembuzi yakinifu, mchakato, wakandarasi na megawati yalitawala.

Mkutano huo ulikwenda hadi saa moja na nusu jioni hii. Ukiachilia mbali ushabiki, nilifurahishwa sana na hotuba aliyoitoa mh Aggrey Mwanry kwani, sauti yake ilipanda na kushuka ghafla huku akichomoa macho kama Kingwendu, ukweli aligusa sana hisia za watu wengi waliokuwepo ingawa wahudhuriaji walikuwa wachache kuliko ilivyotegemewa pamoja na kusomba watu kutoka nje ya mji. Mwisho kabisa wahudhuriaji waliruhusiwa kuulizwa maswali yaliyojibiwa papo kwa papo na mawaziri husika.

Uchache wa wahudhuriaji katika mkutano wa leo ni dalili tosha kuwa Sumbawanga si ya CCM tena hili liko wazi na kama vipi Nape akanushe kwani alikuwepo huku akiwa busy na kamera lake akiigeuza geuza kamera akihangaika kupiga picha ili angalau ionekane kuna uwingi watu.

Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Rukwa ndiyo ulikuwa mtaji mkubwa wa CCM kwa kutumia umasikini na ujinga “kutosoma” kwa wanarukwa wengi hususani wilaya ya Sumbawanga.

Hii ya leo ni tisa ya , kumi ni pale filimbi itakapopigwa ya mchakato wa uchaguzi mdogo wa mbunge wa Sumbawanga mjini sipati picha ccm itaambulia nini. Kimchina changu hakikuwa na chaji nilitamani kuwaleta live!
 
Wakuu mojawapo ya mambo yanayonikera ni pale Mwigulu na wenzake kina Lusinde wanaposema cdm wasitumie magari mazuri au wasipokee posho, je wao ccm kama wanaona ni kosa nao pia si wazifute? Maana ndo imekuwa mashiko ya kusemea, iko siku na inakuja..
 
Hawa jamaa wamebanwa, baraza la mawaziri linapohamia Sumbawanga. Ndio maana magamb
a huwa sibishani nao, their death is imminent.

Hizi huwa ndo dalili za binadamu anayekaribu kufa.Anajaribu kuvuta pumzi ya mwisho,lakini wapi.2015 pamoja
 
Lengo la mkutano huo ni nini? Au ndio jitihada mfu za kuzuia upepo kwa kiganja cha mkono?
 
Campaign manager eeh! Na wewe ujipange kuchukua jimbo siyo kutanguliza wenzio tumb..f! Wasomi wakwepa majukumu huwa siwapendi! LIWALO NA LIWE!

Mkuu hatuwezi kugombea wote kwa pamoja. Lazima wengine wagombee na sisi wengine tuwape support. Swala la Mimi kugombea Ubunge ni swala ambalo lipo kwenye Plan yangu ya maisha toka nikiwa shule ya msingi. Na nimekuwa na record ya kuwa Kaka Mkuu (Mugabe Primary School), Normal Prefect (Pugu High School), Head Prefect (Mzumbe High School), Mbunge wa bunge la Wanafunzi (USRC Member - UDSM) na Chairman wa Faculty of Commerce and Management (UDSM).


TUMBIRI (PhD, Hull University - Hull City, United Kingdom)

tumbiri@jamiiforums.com
 
Wakuu ni kweli kabisa,boda boda zilikuwa 20 hivi na baadae lile jengo alilouziwa aziz mwarabu eti ni kitega uchumi cha chama bila kutaja ni miaka mingapi limemilikishwa lilizinduliwa na wakasema wanashukuru kwa mzindakaya kujenga kiwanda.for sure wana rukwa leo wameonyesha maajabu zile picha za umati wa watu napendekeza ziingizwe kwenye maajabu 7 ya dunia.Tuwapongeze hawa ndugu zetu wa pembezoni kuamka.Yaani wa ujenzi kasema viwanja viwili vya ndege vinajengwa lkn kwa mwana rukwa vina tija gani?wananchi waliuliza.zaidi ya yote kuna msomali mmoja kalalamika kuchukuliwa mke wa ndoa,nae mkuu mpya wa wilaya bwana sedoyeka kaingia king eti aliyegongewa wife aende juma 3 asubuhi ofisini watafute suluhisho yaani mgongaji na mgongewa.look at this mufilisiko wa politics
Mh! hapo kwenye red Muuliza swali lengo lake ilikuwa kumpa dongo Mwigulu sasa wao kwa uelewa mdogo na ukilaza walionao wakafikiri ni swali la kujibu.
 
Mkuu hatuwezi kugombea wote kwa pamoja. Lazima wengine wagombee na sisi wengine tuwape support. Swala la Mimi kugombea Ubunge ni swala ambalo lipo kwenye Plan yangu ya maisha toka nikiwa shule ya msingi. Na nimekuwa na record ya kuwa Kaka Mkuu (Mugabe Primary School), Normal Prefect (Pugu High School), Head Prefect (Mzumbe High School), Mbunge wa bunge la Wanafunzi (USRC Member - UDSM) na Chairman wa Faculty of Commerce and Management (UDSM).


TUMBIRI (PhD, Hull University - Hull City, United Kingdom)

tumbiri@jamiiforums.com

Sawa Mkuu nimekuelewa! Lakini usije kutuangusha hapo baadaye tukaishia kusikia ulisharudi Chama cha Mabwepande!! Maana nyie hamchelewi!!
 
Sawa Mkuu nimekuelewa! Lakini usije kutuangusha hapo baadaye tukaishia kusikia ulisharudi Chama cha Mabwepande!! Maana nyie hamchelewi!!

Mkuu nimepita katika majaribu sana hadi hapa nilipofika. Nakambuka wakati nikiwa UDSM Yusuph Makamba (Katibu Mkuu wa CCM aliyepita) alikuwa anatuma vijana wake watushawishi kujiunga na chama chake. Walileta hadi fedha tukawa tunazikataa. Na kibaya zaidi tulikataa fedha huku mifukoni mwetu hatuna kitu. Baada ya kuoana njia ya kuturubuni kwa fedha imeshindikana walianza kututisha kwamba tutafukuzwa chuo kwa kusimamia migomo iliyokuwa inatetea haki za wanafunzi.

Hata leo nipo hapa HULL lakini nimekuwa nikifuatwa fuatwa kuachana na msimamo wangu na hatimae nijiunge na CCM. Ninawaambia kila siku Am Price less (Sina bei ya kuninunua)!

TUMBIRI (PhD, HULL University, HULL City - United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom