Adam Malima avuruga Maisha Plus.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Jioni hii Adam Malima ameharibu kabisa ufunguzi rasmi wa shindano la Maisha Plus baada ya kutaja wazi eneo kilipo kijiji cha Maisha Plus kuwa ni Bagamoyo na kwamba si mbali kutoka Unguja...,.,gooosh!

Wasemaji wengine wote waliotangulia walikwepa kabisa kusema eneo hilo, nadhani hii ikiwa ni maelekezo ya waandaaji.
Ameshituka baada ya kugundua kosa, lakini ilikuwa too late.
Kwangu mimi amenipunguzia utamu wa zoezi hilo, ambapo huwa ni pamoja na anonimity ya mahala wanapokuwa.

Ufunguzi unaonyeshwa Live na TBC1.
 
Hawa makada wa CCM huwa wanakurupuka sana kwenye kila jambo.

Ona sasa keshavuruga mwenendo mzima wa shindano la watu.

Nawashauri waandaji wa shindano hilo wamdai fidia kwa kuharibu shindano lao.
 
Hakutangaza kugombea Urais? mimi nawashangaa sana watu badala ya kuwaomba watu kama kina Kimey au Manji au Mengi ndio wawazindulie hizi project wao wameng'ang'ana na wanasiasa!! usikute macho yake yalikuwa kwa warembo tu.
 
Hata mimi nimesikitika sn kwa watu makini km Masoud Kipanya kumwita Adam Malima ambapo anjmjua in and out kuwa ni scandalous.
Amezidiwa kwa mbali sn kwenye speech na mwanadada Ummy, yule naibu waziri wa jinsia!
 
Hili shindano naona halina maana yoyote wala mafunzo ningewaona wa maana km shindano lao lingelenga mambo muhim km afya, elim na namna ya kuinua uchumi wa nchi ila naliona limekaa ki ccm zaidi
 
Sisi bado tunaishi ki communist kwa kweli
waziri wa nini kwenye entertainment?
uliwahi sikia Obama kualikwa american idol awe mgeni rasmi?
 
aaaaaaaaah.......sasa ameharibu utamu wote.........kwanza si hata washiriki huwa wanapelekwa wakiwa wamefunikwa macho...?
amesema ya nini....aliombwa....?
 
Hili shindano naona halina maana yoyote wala mafunzo ningewaona wa maana km shindano lao lingelenga mambo muhim km afya, elim na namna ya kuinua uchumi wa nchi ila naliona limekaa ki ccm zaidi
Mkuu, utakuwa hujaliangalia kabisa. dSafari hii wameliandaa kwa busara na umkini sn baada ya kuweka theme ya "Mama Shujaa Wa Chakula"!
Kimsingi washiriki ni akina mama walioenda 'mileage' ya kutosha.
 
Hili shindano naona halina maana yoyote wala mafunzo ningewaona wa maana km shindano lao lingelenga mambo muhim km afya, elim na namna ya kuinua uchumi wa nchi ila naliona limekaa ki ccm zaidi
wewe kumbe unaona mbali kuliko wengine.
 
Mkuu, utakuwa hujaliangalia kabisa. dSafari hii wameliandaa kwa busara na umkini sn baada ya kuweka theme ya "Mama Shujaa Wa Chakula"!
Kimsingi washiriki ni akina mama walioenda 'mileage' ya kutosha.
Kwa hiyo hao akina mama wazee wameliongezea maana ipi?
 
Kwa hiyo hao akina mama wazee wameliongezea maana ipi?
Lengo kuu ni hatimaye kumzawadia mama shujaa atakayeonekana kuwa mbunifu na mzalishaji bora wa kijasiriamali wa chakula...thats what i perceive.
 
kosa lake lipi watu wengine bana mnaona doongeeee mtajibeba

Usikurupuke ndugu,
Umeshasikia kuwa wageni waalikwa wote walipewa angalizo kutoweka wazi Mahala shindano hilo linafanyoka ikiwa ni sharti mojawapo la shindano hilo.
sasa donge unalozungumzia hapo ni lipi, ni huo ujuha wake?
 
Juha kama huyu eti hapa bongo ni naibu waziri wa nishati na madini! halafu anandaliwa kuja kuwa raisi wetu mwaka 2020!!!!!
 
Back
Top Bottom