Adam Chagulani (Diwani aliyetimuliwa CHADEMA) aanza kufunguka...

Huyu bwana anajidanganya. Huwezi kumkataa mama mkwe halafu ukasema unampenda mwanae ukaishi salama. Hapa ni ama mwanae au wewe mmoja atakwenda chini ki ninja ninja
 
hivi huyu bwana mdogo Chagulani alifanikiwa kumaliza chuo pale Udsm? maanake alikuwa kiongozi wa vijana wafanya vurugu na wala si mpiganaji zaid ya kuwa mpenda cheap popularity
 
Ok, tumekusikia, ila nadhani bado dhambi itakuandama kama hutaki kujilekebisha
 
Dogo ni Jembe tena Sana tu. Watu ambao wamefanikiwa Kuona kash kash zake kwenye vikao vya halmashauri na Jinsi alivyo Makini huwezi thubutu kukubaliana na hii taarifa ya kumwagwa.
Mbaya ni Kuona watu wanamshitumu tu Adam kwa kosa la kubumbiwa na lenye fitna ndani yake.
Alafu watu wanakubaliana na info kutoka juu hata Kama hazina tija wala haki kwa ADam
Lazima watu wawe wanapima Kama vitu ni sawa sio kila linalotolewa na uongozi wa chadema ni sawa na watu wana buy them na kufanyia kazi. Hatuwezi kwenda popote. Kabla ya kamati kuu ilitakiwa lipitie ya wilaya kisha mkoa. Sasa hii shuttuma direct to kamati kuu na hapo hapo maamuzi kutolewa uanachama. Hakuna first warning last warning wala nini?watu wa chadema ni perfect tupu Hakuna makosa! Duuu

Kuna kipindi niliamini CHAGULANI anaweza kuivusha CDM kwenda hatua nyingine ndani ya Mwanza, lakini sikuwa sahihi hata kidogo kwani nilipoenda mwanza nilijitahidi sana kuonana nae na kuweza kuongea kuhusu siasa za mwanza na matarajio yake kisiasa.Hapa ndo nilipogundua kuwa hana Vision ya kichama na wala kijimbo zaidi alinielezea hujuma alizofanyiwa na Wenje na jinsi alivyojiandaa kupambana nae kwani wenje anaona dogo atakuwa Mwiba kwake 2015 katika nafasi ya ubunge Nyamgana.
Kwa kweli kuna mambo mengi aliyasema kwa busara sitayaweka hapa ni kweli alikuwa anania sana ya kuwa Meya kwani haamini kwa Madiwani wa CDM mwanza hakuna aliye na vigezo zaidi yake na pia anaona ana nafasi ya kuwa mbunge wa Nyamagana 2015.
Dogo yuko katika mapambano ndani ya chama kuonyesha kuwa viongozi na watu wanaomuunga Wenje hawapati nafasi ndani ya chama na kimkakati waangushwe katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama ili apange safu kuelekea 2015.

Kuna maswali mengi nilimuuliza yalikosa majibu;
1.0 kama tatizo ni wewe na Wenje hakuna njia nyingine ya kutatua zaidi ya kukigharimu chama?
2.0 hizi hujuma munazofanyiana mnajenga chama au mnabomoa?
3.0 Tangia uwe diwani umefungua matawi mangapi ya CDM nje na ndani ya kata yako?
4.0 Vipi kama mpango wako wa kumuangusha wenje utafanikiwa kabla ya 2015 huoni utaliingizia taifa hasara ya kuingia katika uchaguzi mdogo?
5.0 Vipi ukiachana na mambo haya yaliyopita ukajikita kuimalisha chama huoni 2015 utakuwa na nafasi kubwa kuliko hivi sasa mnavyonyukana wenyewe kwa wenyewe?
6.0 Kwanini ulipokosana na mkuu wa shule wa SHAMALIWA SEC ulipopata udiwani ulishughulika nae mpaka akaamua kuhama kituo cha kazi huoni unafanya kazi za kulipiza visasi?

Kuna mengine mengi siwezi kuyatupia hapa ila tu CHAGULANI anakosa uvumilivu kwa kisiasa na yuko tayari kupambana na mtu bila kujali maslahi ya umma au jumuiya.
 
Wenje ana fitina mbaya sana ugomvi wake na Chagulani kaupeleka kwa Mbowe na Dokta Slaa.
Kwa taarifa ya Bwana Adam Tanzania ya sasa haitaji kiongozi legelege kiongozi kama Dr Slaa ndiye haswa anafaa kuongoza TZ yetu, yako madudu mengi hayaitaji kufumbiwa macho, yanahitaji greda la kuyangoa na greda letu ni Dr Slaa!!!! Bwana Adama uje tena kwa staha na adabu ili viongozi waweze kukuelewa kama sio mnafiki, lazima uelewe malengo ya CDM kwa sasa!!!!

 


  • Nipenda kutumia fursa hii kuwataarifu wapenzi wa mageuzi na wakweli wote kuwa sina mpango wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi kama maadui zangu wa kisiasa wanavyozusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa nina mpango wa kujiunga na CCM ,

    niseme hivi sijawahi kuwa mwanaccm na kamwe sitakuwa mwanaccm mimi bado ni mwanachadema kindakindaki najipanga jinsi ya kuitafuta haki yangu nawaheshimu sana viongozi wangu wa chama hasa mwenyekiti F.Mbowe,Zitto kabwe Dr.Kitila; niseme binafsi nimesikitishwa na kuhusihwa na majungu kuwa nimeshiriki vitendo vya kifisadi na kukihujumu chama changu nilichokipigania siki zote tangu nikiwa chuoni hadi sasa nitaandika waraka mwingine kueleza kilichojiri na nini hatua inayofuta baadae tuko pamoja ukombozi wa taifa hili ni lazima kwa njia yeyote ile



1.Penye kijani, Kushiriki katika kuua chama siyo lazima utoke chama kingine bana aaaahg!!
2. Penye Blue, kwa kuwataja viongozi wa CDM bila kumtaja Dr Slaa umenifanya ni hisi una bifu na Katibu mkuu, leo hii baada ya kukubana wewe personally ndo unaona hafai kabisa kushika nchi hii, huu ndiyo tunaita ubinafsi ningekuona ni mpigania maslahi ya nchi wa ukweli iwapo tu ungeyasema haya kabla hajakubana wewe binafsi, huu ni ubinfsi ndugu yangu haiwezekani utoe tamko kwamba mtu hafai kushika madaraka makubwa baada ya kukubana wewe.
3. Penye red, Kwani kukipigania chama kwa mda mrefu ni justification kwamba hujanunuliwa kukihujumu chama? Umeniudhi sana kwa ubinafsi uliouonyesha kwa hili tamko lako, chonde chonde hata huo waraka mwingine unaotaka kuandika usije kuwa wa kumlenga mtu aliyegusa maslahi yako bali ulenge katika kujenga chama, na jiepushe kumkandia mtu baada ya kukubania sehemu, ikitokea kuna mtu umegundua hafai katika chama toa tamko haraka ndani ya vikao vya chama siyo usubiri yeye anapokugundua wewe hufai ndiyo useme na yeye hafai.
 
Enzi zile wakati Dr. Slaa anaiheshimu Jamiiforums angekuwa kashakuja hapa kulitolea ufafanuzi swala hili.
 
Ninaamini kwamba kama kweli anakipenda chama chake CDM, asingeleta malalamiko yake humu ndani ya JF, ambamo hayawezi kupatiwa ufumbuzi zaidi ya kujadiliwa tu.

Ashakum si matusi, lakini hii ni sawa na mtu aliyemfumania mwenzi wake, badala ya kuyamaliza kimya kimya kama bado anampenda, anaamua kuita watu waje washuhudie kisha wanaondoka wote na mwenzi wake kurudi nyumbani kulala eti wamepatana!!?? Ni aibu.
I agree, huyu dogo (Chagulani) na mwenzake Matata, kama wanafikiri wameonewa wakate rufaa kwa mujibu wa katiba ya CDM. Hapa JF ni pa kuenezea propaganda na fikra za chukii bila sababu.
 
Kimbunga mwambie rafiki yako Chagulani asipoteze muda kupiga kelele nyikani. Kwa msaada zaidi awasiliane na wale watano waliokuwa madiwani jijini Arusha wamshuhudie mbio zao zilipoishia. Nao walikuwa wanatapatapa hivihivi wakimshutumu Dr. Slaa, kitu ambacho kilikuwa ni aibu kwao wenyewe kwani kwa watu wanaojua katiba, kanuni na taratibu za Chadema walikuwa wanawahurumia tu kama si kuwacheka kutokana na madai yao ya kitoto!


Wale wa Arush nao walikua hivi hivi kisa kuona chama kama ndio kinawahitaji sana zaidi ya wao wanavyokihitaji..sasa wanasaga meno...mimi ningeshauri hawa vijana waone ccm inavyokua tofauti kwenye masuala ya nidhamu..huwezi kukuta diwani anamtusi Katibu Mkuu hata wa wilaya tu,,ila wao hawa vijna wasio na adabu wanamtusi Katibu Mkuu wao Taifa tena mtu kama Slaa...hilo ni kosa kubwa sana...kwanza kwa kusema hayo anatakiwa huyu jamaa achukuliwe hatua zingne kwa kosa la kumtusi Dr slaa..adabu hakuna kabisa na hili ni jambo la kufanyia kazi ...
 
  • Chagulani Adams


    Chagulani Adams
    Nipenda kutumia fursa hii kuwataarifu wapenzi wa mageuzi na wakweli wote kuwa sina mpango wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi kama maadui zangu wa kisiasa wanavyozusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa nina mpango wa kujiunga na CCM ,

    niseme hivi sijawahi kuwa mwanaccm na kamwe sitakuwa mwanaccm mimi bado ni mwanachadema kindakindaki najipanga jinsi ya kuitafuta haki yangu nawaheshimu sana viongozi wangu wa chama hasa mwenyekiti F.Mbowe,Zitto kabwe Dr.Kitila ,na wote wanaopenda ukweli na siyo wafanyia kazi majungu HUKU WAKITAKA NAFASI NYETI NCHINI nimuomba MUNGU KUANZIA SASA WASIPATE NAFASI HIZO MAANA kama wanayafanya haya hawajawa na uhakiki wa amri kwa vyombo vya ulinzi vipi?

    wakijua wanausalama wanawalinda sipati picha MUNGU aepushe bali na balaa hilo,niseme binafsi nimesikitishwa na kuhusihwa na majungu kuwa nimeshiriki vitendo vya kifisadi na kukihujumu chama changu nilichokipigania siki zote tangu nikiwa chuoni hadi sasa nitaandika waraka mwingine kueleza kilichojiri na nini hatua inayofuta baadae tuko pamoja ukombozi wa taifa hili ni lazima kwa njia yeyote ile



kaandika akiwa na jazba sana
 
Mimi ningempa huyu dogo ushauri wa bure. Mapambano hayawezi kukusaidia chochote, utaishia kwenda CCM tu. Uamuzi ni wa kamati kuu ya Chama, si wa Slaa wala Mbowe. Sasa wewe unapojaribu kuwagawa unakosea sana, CDM haifanyiwi hivyo hata siku moja. CDM ni wamoja sana kama ulishindwa kuwaridhisha kwa hoja ujue imetoka.

Ushauri wangu ni kuwa nenda chini omba msamaha urudishiwe uanachama, mapambano hayatakusaidia kabisa, angalia wenzenu wa Arusha walijitahidi lakini wakakwama, na mahakama ilikwishatoa jibu "Maamuzi ya Chama ni ya MWISHO" Teremka omba radhi dogo, bado tunakuhitaji, usimfuate Matata, yeye ni makapi ya CCM na si mpambanaji.

USHAURI WA BURE.
 
  • chagulani adams


    chagulani adams
    nipenda kutumia fursa hii kuwataarifu wapenzi wa mageuzi na wakweli wote kuwa sina mpango wa kujiunga na chama cha mapinduzi kama maadui zangu wa kisiasa wanavyozusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa nina mpango wa kujiunga na ccm ,

    niseme hivi sijawahi kuwa mwanaccm na kamwe sitakuwa mwanaccm mimi bado ni mwanachadema kindakindaki najipanga jinsi ya kuitafuta haki yangu nawaheshimu sana viongozi wangu wa chama hasa mwenyekiti f.mbowe,zitto kabwe dr.kitila ,na wote wanaopenda ukweli na siyo wafanyia kazi majungu huku wakitaka nafasi nyeti nchini nimuomba mungu kuanzia sasa wasipate nafasi hizo maana kama wanayafanya haya hawajawa na uhakiki wa amri kwa vyombo vya ulinzi vipi?

    Wakijua wanausalama wanawalinda sipati picha mungu aepushe bali na balaa hilo,niseme binafsi nimesikitishwa na kuhusihwa na majungu kuwa nimeshiriki vitendo vya kifisadi na kukihujumu chama changu nilichokipigania siki zote tangu nikiwa chuoni hadi sasa nitaandika waraka mwingine kueleza kilichojiri na nini hatua inayofuta baadae tuko pamoja ukombozi wa taifa hili ni lazima kwa njia yeyote ile




bannnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnned!!!!!!!!!! Ukwende hukoooooooooooooo!!!
 
HII imewekwa hapa na adam chagulani kweli? chagulani ninayemfahamu anamtukana DR basi adam its now important you need a severe counseling to maximum
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom