Adai Mbegu za Kiume Kwenye Swimming Pool Zimesababisha Apate Mimba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Mwanamke mmoja raia wa Poland ameifungulia mashtaka hoteli moja ya nchini Misri kwa kusababisha binti yake mwenye umri wa miaka 13 kupata ujauzito kutokana na mbegu za kiume alizokumbana nazo wakati akiogelea kwenye bwawa la kuogelea la hoteli hiyo.

Mama wa binti huyo aliyejulikana kwa jina la Magdalena Kwiatkowska alirudi Poland na binti yake huyo mwenye umri wa miaka 13 kutoka vakesheni nchini Misri binti yake huyo akiwa tayari ameishapata ujauzito.

Magdalena alidai kuwa binti yake alipata ujauzito baada ya kujitosa kuogelea kwenye bwawa la kuogolea la hoteli hiyo ambalo wanawake na wanaume walikuwa wakichanganyika.

Magdalena alisisitiza kuwa binti yake alipata ujauzito baada ya kukumbana na mbegu za kiume wakati akiogelea kwenye bwawa la kuogelea la hoteli hiyo.

Magdalena ameifungulia kesi hoteli hiyo akidai alipwe fidia.

Chanzo kimoja cha habari kilisema kuwa mama huyo anasisitiza kuwa ana uhakika wa asilimia mia moja kuwa binti yake hakufanya mapenzi na mvulana yoyote wakati alipokuwa hotelini hapo.

"Magdalena amedhamiria kuendelea na kesi yake ya kudai fidia" kilisema chanzo hicho.

Mamlaka ya utalii ya Poland jijini Warsaw ilithibitisha kwamba imepokea taarifa ya kesi hiyo ambayo haijawahi kutokea duniani.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2463986&&Cat=2
 
Hamna lolote hapa. Haka ka-binti panga pangua kalichora 7.

Wanataka tu kuwasumbua Matajiri wa Misri. Yaani bwawa halina Chlorine za kuuwa wadudu?
 
Ni kweli kitu hicho kinawezekana kabisa, mbegu za kiume zina nguvu ya ajabu sana zina uwezo wa kuishi siku mbili mpaka tatu zikishatoka kwa mwanaume, na mwanamke sio lazima kufanya tendo la ndoa ndio mimba itunge, siku zikiwa ni za kupata minda mbegu za kiume zikigusa na kufanikiwa kupata njia ya kufika kwanye uke anapata mimba, imeshatokea mwanamke alijifutia taulo liliokuwa na mbegu akapata mimba, na kuna binti hapa bongo alipata tena ilikuwa nyumbani kwao kwenye choo cha kukaa kumbe wavulanda ndani ya nyumba walikuwa wanajichua wakienda kujisaidia siku ya siku wakabakisha mbegu juu mdada alipokwenda kujisaidia akazibeba ikawa mtafaluku ndani ya nyumba wakati binti alikuwa bikira. kwahiyo amini inawezekana
 
Mama amekosea binti alitumia taulo la pale hotelini amabalo njama jana yake alitumia baada ya self service! Mabinti wengi wamepata mimba kwa mtindo huo.
 
CAN YOU CONVICE ME!
Bt may be kama hakuvaa swimming cost bt also its alive if there is'nt chemical so................????!!!!............what abt health of the users if water does'nt purefied.
 
Sometimes vitu hivi ni vigumu sana kung'amua... Only God knows ndio maana ni vigumu sana kukataa theory hiyo, hata mimi sina comment, inawezekana. Kuna wengine si eti kugusa tu mbegu ila kupata kwa sexual int. lakini unaambiwa mbegu zilikuwa kidogo hazikuweza kuswim mpaka kunako... iweje kwa taulo? I cant prove though...
 
karibu jkwaani ndugu
 
Ni kweli kitu hicho kinawezekana kabisa, mbegu za kiume zina nguvu ya ajabu sana zina uwezo wa kuishi siku mbili mpaka tatu zikishatoka kwa mwanaume, na mwanamke sio lazima kufanya tendo la ndoa ndio mimba itunge, siku zikiwa ni za kupata minda mbegu za kiume zikigusa na kufanikiwa kupata njia ya kufika kwanye uke anapata mimba, imeshatokea mwanamke alijifutia taulo liliokuwa na mbegu akapata mimba, na kuna binti hapa bongo alipata tena ilikuwa nyumbani kwao kwenye choo cha kukaa kumbe wavulanda ndani ya nyumba walikuwa wanajichua wakienda kujisaidia siku ya siku wakabakisha mbegu juu mdada alipokwenda kujisaidia akazibeba ikawa mtafaluku ndani ya nyumba wakati binti alikuwa bikira. kwahiyo amini inawezekana

No No No... Sio katika swimming pool. Zinaweza kuishi katika mazingira maalumu ya kuhifadhia. Kitendo cha mbegu hizo kuwa ndani ya swimming pool, ingesababisha zife au zipoteze uwezo wa kuogelea baada ya sekunde chache. Chance kuwa mtoto huyo alikuwa anaogelea, eti mbegu zijipenyeze hadi apate mimba is practically impossible... Huyo alichakachuliwa...
 
Hamna lolote hapa. Haka ka-binti panga pangua kalichora 7.

Wanataka tu kuwasumbua Matajiri wa Misri. Yaani bwawa halina Chlorine za kuuwa wadudu?

kwani mbegu ni wadudu?. Mi nadhani ni protein zaidi na hazidhuriwi na disinfectants
 
Inawezekana. Izo zinaitwa mimba za chooni kama mdau mmoja alivosema km zimeachwa kwenye choo mwanamke akikalia anaweza kupata ujauzito.
 
Back
Top Bottom