Ada ya mtoto kwa dola, hoteli kwa dola, mbona mshahara wangu kwa shilingi?

Nyambala,

Hiyo sheria bado ipo (legal tender is still a Tanzanian Shilling - TZS!). Cha msingi watu kujua ni kwamba, wafanyabiashara wanaweza kuweka bei in any currency provided the TZS equivalent is also provided/declared. Zaidi ya hapo wafanyabiashara kisheria hawatakiwi 'kumlazimisha' mteja kufanya malipo kwa currency tofauti na TZS (i.e. ukitoa/lipa TZS na muuzaji akikataa kupokea anavunja sheria). Hayo yote ni kwa biashara au mauzo yanayofanyika ndani ya Tanzania.
Sasa mkuu mwenye habari anakwambia bei mashuleni au mahotelini yameandikwa interms of dola na siyo TZs. Sasa kwa mtanzania unapesa zako mfukoni za TZS umefika hotelini usiku hizo dola unazipata wapi au ndo kugongwa bei yoyote. Mambo mengine serikali yetu inaexpose tu their inferiolity. Na hapo wanakwambia tanzania ni soveiregnity lakini ni kwenye mipaka tu na madaraka mambo mengine wanaamuliwa tu na ngozi nyeupe. It sucks!.
 
Kwa kiwango changu kidogo cha uelewa, Ilitakiwa mtu aweke bei yake kulingana na gharama zake kwa shiling kwani ndiyo currency ya nchi. Ukijenga hoja ya importation maana yake hata waalimu na wafanyakazi wa mahotelini wanakuwa imported? mbona wao wanalipwa kwa shiling.

Tatizo la huu mchezo ni kutokuwa na bei maalumu kila kunapokucha, so inflation haipimiki sawasawa. ukiangalia takwimu za BOT zinakuambia inflation ni 12% lakini kivitendo mtaani ni zaidi ya hapo. Angalia mfano huu. January ada ya mtoto ni dola 550 amabazo ni sawa na shilingi 720,000/=. ikifika April ada ya mtoto ni dola 550 ambazo ni sawa na shilingi 770,000/= tayari ni kitu tofauti kati ya january na april. Mimi nayepokea mshahara kwa shilingi nitapata wapi hilo ongezeko??
 
Kinacho fanya serikali isijali kuhusu hili swala ni wengi wa vigogo wa serikalini ndio wahusika/wamiliki wa hizi sehemu zinazotaka malipo kwa njia ya dollar.watanzania tungekuwa na ushikiriano haya yote yasingetokea sema kuna kundi letu wanaona sifa kulipa kwa dollar na hii inaonesha kuwaunga mkono hawa wafanya biashara.pesa chafu zinazoibiwa hovyo hovyo serikalini ndio zinasababisha vitu kama hivi.
 
Kwa hiyo mmeamuaje? Twendeni kwa Ndulu au Kikwete? Au hii ni another fruitless discussion?
 
Ndugu zangu wana JF nisaidieni, nilalamike wapi?

Narudisha watoto wangu shule na mwingine mmoja anaanza shule, kufika tu shuleni naambiwa ada ni dola za kimarekani kadhaaa, nashangaa, anayenihudumia ananiambia lakini unaweza kulipa kwa shilingi ila utabadilisha kwa kiwango cha 1,400/= kwa dola moja, naendelea kushangaaaa.

Naenda hotelini bagamoyo, nimeamua kupunguza uchovu wa pilika za Dar, nafika naambiwa bia dola mbili, chumba dola kadhaa, nashangaa, nauliza kwani hapa ni marekani? naambiwa shilingi haina msimamo. Nashangaaaaa

Napewa safari ya kikazi kwenda Afrika Kusini, najua niko kwa watu na pesa inayoweza kunisaidia ni Dola au Randi. Nikiwa hotelini nataka kulipa nilichotumia kwa dola, mhudumu ananiambia hapana nenda pale badilisha halafu nipe randi. nashangaaaaaaa.

Who is suppose to manage this in our country? Mr Ndulu? Mr Mkullo? au Mh Raisi? Naamini mtanisaidia. Hili jambo linanikera sana na sielewi ni nani sahihi wa kumlalamikia.

Respct.
Hapa Tanzania hilo jambo limepigiwa kelele wee mpaka kuna wakati lilifikishwa bungeni lakini wapi,hapa jirani yetu Kenya huwezi ukaenda dukani eti kitu kinauzwa kwa dola ,hakuna hata nchi masikini kama Malawi hakuna eti kulipa kwa dola ,lakini tusilaumu tu serikali huu ndio mfumo ambao sisi wananchi tumeulea angalia hata humu JF kwenye matangazo members wanauza vi laptop vyao eti kwa dola,hata magari wanauza kwa dola.
Huu ni wazi wa mchana kweupe ,lakini mimi naamini serikali makini haiwezi kuruhusu huu wizi,bahati mbaya viongozi wetu vision yao ni mambo ya kupata kura tu na kutawala.Pia haya mambo ya kulipia kwa dola inawasaidia sana wafanyabiashara wakubwa ,mafisadi na wanasiasa ambao wamejiwekea vitega uchumi vingi kwenye majumba na mahoteli,narudia tena kama serikali ikitaka kukomesha hili jambo inaweza kabisa ,mbona liliweza kwenye mambo ya Vocha,si hapo mwanzo vocha zilikuwa zinauzwa eti kwa rate ya dola?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom