Achukue uamuzi gani baada ya kujua haya?

situmai

Member
Jun 29, 2012
85
18
kuna mdada mmoja yeye aliolewa miaka miwili niliyopita akaja kugundua mume wake alikuwa na mahusiano wakati wako katika uchumba na mpaka siku chache za harusi alikuwa bado wanawasiliana,je afanyaje?
 
Kuna watu kweli wafukunyuzi na wapenda makuu, mmesha kaa miaka miwili mnatafuta uamuzi wa kuchukua kwa issue ilofanyika nyumba kabla hata ya kufunga ndoa?

Ladies wake up!! Unapokuwa ni mke au mchumba haina maana upo peke yako, ina maana tu kuwa wewe ndio una qualify kuwa nae katika kila hatua ya maisha... wa kushare LAZIMA wapo. Ni rare unapokuwa kweli uko peke yako. Njema inaoa kesho usiku wake kalala na mwanamke... Inaboa ila hio ndio ukweli whether you like it or not.
 
Chochote atakachofanya ni sawa tu...sipendi kumwambia mtu cha kufanya katika mahusiano na ndoa.
 
Unapofukunyua mambo na mipango uwe nayo sio unafukunyua halafu unakuja kuuliza watu.
 
Kuna watu kweli wafukunyuzi
na wapenda makuu, mmesha kaa miaka miwili mnatafuta uamuzi wa kuchukua
kwa issue ilofanyika nyumba kabla hata ya kufunga ndoa?

Ladies wake up!! Unapokuwa ni mke au mchumba haina maana upo peke yako,
ina maana tu kuwa wewe ndio una qualify kuwa nae katika kila hatua ya
maisha... wa kushare LAZIMA wapo. Ni rare unapokuwa kweli uko peke yako.
Njema inaoa kesho usiku wake kalala na mwanamke... Inaboa ila hio ndio
ukweli whether you like it or not.

Mh! Bitter truth.
 
Wewe stumai kama sio umbea ni nini?..kwann huyo mwanamke yalomkuta ya kuchimbua makaburi asije yeye kutuuliza sie tumshauri cha kufanya...acha umbea na kuyakuza ya majumbani mwa watu..sawa??

Kuhusu ushauri afanyeje baada ya kugundua kuwa hukoooooo nyuma zamani za kale kabla hajaolewa mmewe alikuwa na demu ni haya.

1- kila mwanaume kabla hajawowa alikuwa na mahusiano..kama anabisha akkamuulize babake na mamake

2- kila mwanamke na kwa asilimia 100 nyie wa sikuhizi kabla hamjapata waume zenu wa ndoa wote huwa hamna u-bikira wenu sema sie tunawavumilia na kuwawoweni tuu ilhali tukijuwa kuwa nyie ni used

3- kabla hajatoa kibanzi kwenye jicho lake aangalie asijekuwa na boriti jichoni mwake

4- kula ni kula kibaya kukomba mboga..je mumewe baada ya kumuoa anawanawake wengine?..hata kama anao ajue ndio hukooo anaenda kufanya mazoezi na kuimarisha ndoa yake kwa kuleta ubunifu na style na mitindo mipya kitandani

5- namshauri kama dadangu..asome na alama za nyaqkati..wanawake ni wengi kuliko wanaume kwa hiyo asithubutu kumuachia aendezake atajajutia maamuzi yake maana sahivi sie ni bidhaa hadimu na tunatafutwa sana na wanawake wasio na waume.

6- kwa mujibu wa bibilia mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ..naamini huyu dadangu sio mbumbavu.
 
Yeye anataka wa kwake peke yake??atamtoa wapi??
mapadre wenyewe na wachungaji watu tunashare, budget imepanda bora na kipato cha sadaka kitusaidie, itakuwa huyo kondoo! dada kwa kifupi hakuna chako peke yako, ukijenga hiyo dhana utaishi maisha ya bila stress, kama unataka wako peke yako finyanga uweke ndani ebo!
 
Mwa,mbie haache utoto atulie!
Alaf asipende chokochoko mwanaume hachungwi.
 
hivi kweli huyu mdada yuko serious ama? alipokuwa ana mchumba hakuyachunuza hayo anakuja kuyachunguza makosa ya uchumba akiwa ndani?

FYI past experiences not always works sometimes wapaswa kuipotezea tu
 
aachane na mumewe wa ndoa halafu akaolewe tena na mwanaume ambaye hatokuwa na mwanamke mwingine, sawa eee!
 
duh nashushukaje jamani? najuta kuomba ushauri.... well let me stop umbea who cares
 
Jambo la kufuatilia ni kwamba bado mume wake yupo kwenye mahusiano na huyo kimada baada ya kuolewa? Kama bado wapo kwenye mahusiano sasa hapo hipo shida, ila kama ulikufa, waendelee tu na ndoa yao.
 
kuna mdada mmoja yeye aliolewa miaka miwili niliyopita akaja kugundua mume wake alikuwa na mahusiano wakati wako katika uchumba na mpaka siku chache za harusi alikuwa bado wanawasiliana,je afanyaje?

Aendelee na ndowa yake kwani si unasema ilikuwa...? Hizi ilikuwa tukizifatilia tutashindwa kuwa na ilivyo.... na itakavyo...!
Ndowa ni sasa kwenda mbele tu!
 
Back
Top Bottom