Achimba Kaburi Amzike Baba Yake Akiwa Hai

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
Achimba Kaburi Amzike Baba Yake Akiwa Hai
5524686.jpg

Wednesday, March 16, 2011 11:08 AM
KIJANA aliyetambulika kwa jina la Kizito Mwashala (29), mkazi wa Mbagala Kilungulile, ametoa mpya ya mwaka kwa kuchimba makaburi ili amzike baba yake ambaye yu hai kwa kile kilichodaiwa kumchelewesha kurithi mali zake.Katika hali ambayo haikuweza kuaminiwa na walio wengi, kijana huyo aliamua kuchimba makaburi matano ndani ya nyumba yao ili aweze kumzika baba yake kwa siri aliyetambulika kwa jina la John Mwashala(87).

Ilidaiwa kuwa wakati kijana huyo alipokuwa akiandaa makaburi hayo alionekana na baadhi ya majirani na walimuibia siri hiyo baba yake ndipo ripoti ikatolewa ofisi za serikali za mtaa.

Baada ya kuona siri hiyo imetolewa alianza kumpiga baba yake huyo kwa vitu mbalimbali kwa lengo la kummaliza na majirani walikusanyika kumkamata na kumfunga kamba kisha kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi cha maturubai.

Ilidaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akimpa mateso baba yake huyo kwa kumnyima chakula huku akivuta bangi akiwa ndani humo na kumpulizia moshi wa bangi na ndugu zake walikuwa wakihofia kufika hapo kutokana na ubabe wa kijana huyo, ukatili, utukutu na hata kuwatishia kuwaua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa atafikishwa mahakamani siku yoyote.
 
Apelekwe hospital akapimwa akili kwanza.
Huyo atakuwa amezidiwa na mabangi na bongo imekuwa mbofu kabisa.
So ni bora akatibiwa kwanza kutoa sumu ya bange
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom