Achen kuchangia harusi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Thursday, 07 October 2010 08:27

WATANZANIA wametakiwa kuondokana na tabia ya kuchangia sherehe na harusi badala yake kuiga wananchi wa Kenya wanaoshirikiana katika kuchangia elimu kwa mtindo wa harambee.

Changamoto hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Shirikisho la sekta Binafsi Tanzania, Esther Mkwizu, wakati akizungumza na wanafunzi na wazazi wa Shule ya Sekondari ya Suji katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mkwizu alisema wananchi wa Kenya bila kujali ni matajiri au maskini kwa kiwango gani, kupitia harambee watoto wa familia za kipato cha chini wameweza kupata elimu ya viwango mbalimbali hata nje ya nchi.

Alisema umefika wakati sasa Watanzania kuiga mfumo huo ikiwa wanataka mabadiliko na maendeleo yenye tija katika elimu hasa katika kipindi hiki cha utandawazi na muunganiko wa mataifa ya Afrika ya Mashariki.

Aliwataka wazazi kutoona uchungu kulipia gharama za masomo kwa watoto wao kwa madai kuwa ukombozi wa Mtanzania kuondokana na umaskini utategemea kiwango gani cha elimu alichonacho.

"Ndugu wazazi najua mnalipa kiasi kikubwa cha fedha kulipia ada katika shule hii ambayo ni ya binafsi inayomilikiwa na Kanisa la Kisabato, lakini nataka mjue kuwa hata utekelezaji wa sera ya kilimo kwanza lazima kilimo kiwe cha kisasa na kifanyike na wakulima wasomi," alisisitiza Mkwizu.

Mkutano huo uliofanyikia shuleni hapo, pamoja na mambo mengine wadau walipata fursa ya kujadili na kuona changamoto zinazokabila taasisi hiyo katika kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo majengo.
 
Back
Top Bottom