Accidents at Kibaha: A Scientific Reason?

Mimi nadhani kuna matatizo ya aina mbili. kwanza udogo wa barabara, na pili uzembe wa madereva. tuchukue mfano wa daraja la wami, kabla ya hatua zilizochukuliwa pale, wengi wetu tuna kumbukumbu jinsi roho za watu zilivyoishia pale. sasa hivi matukio ya ajali pale ni kama hakuna.
Chalinze - Dar, Serikali ichukue hatua kama ilivyofanya Wami. itafute solution, zaidi ni kupanua barabara si kuongeza matuta. Hatua kali zichukuliwe dhidi ya madereva wazembe, nadhani tutaweza kupunguza ajali.
 
Hakuna sayansi wala nini ni uzembe tu...lile lori ni zee sana na halistahili kuwa barabarani....magari yote makubwa unayoyaona barabarani 99% ni mitumba na hayakaguliwi...mimi naishi Tegeta na almost kila siku tunapamabana na yale ya cement toka Wazo...mazee kwelikweli na yanapita mbele ya trafiki huku wakipungiana...pita wewe na saloon yako unapigwa mkono..triangle,fire extinguisher leseni ya mkeo....lakini haya madude hayakaguliwi hata kidogo...mengine ni models za 1970s
 
HADI LEO HII dar hakuna fy-over hata moja....!na kila siku watu wanalia foleni.

WAKATI HUO HUO....!jiji kama BERLIN lina fly-overs,na foleni zipo.sasa hebu angalia huu mlinganyo halafu uniambie DAR ES SALAAM KUNA MAGARI MENGI!kuna magari mengi kama london?berlin?paris?

kinachotumaliza sisi ni ''SIASA''!....hata researsch za bongo zimegubikwa na siasa
 
Nakubaliana na Safari ni Safari na wale wanosema uzembe wa dereva (au kwa asilimia kubwa Konda ambae hakuwa na leseni). Hivi kwa nini kila siku sababu inakuwa ni "kufeli kwa breki" tuu? Hili ni changa la macho.

Kwa upande mwengine na sisi abiria tunachangia kwa kiwango kikubwa kwenye haya magari yanayosafiri long distance. Kwa mfano munamwona dereva anaendesha kama kichaa na mumenyamaza tuu mpaka itokee ajali ndio munaanza kukurupuka "oooooh akiendesha kwa kasi sana" - mulikuwa wapi?

Au unamwona Konda amepewa gari akiliangusha ndio munaanza kulalamika.

UMEFIKA WAKATI WA KUCHUKUA HATUA KUZUIA UZEMBE WA MADEREVA
 
sehemu nyingi Tanzania magari yanapishana, milimani, mabondeni, kwenye kona n.k lakini hakuna mahali panapovutia ajali zaidi kama Kibaha why?

You are right M/Kijiji, tulitakiwa tuone ajali za kila siku Kitonga huko na siyo kibaha. Ila haya mambo huwa yapo, nafikiri ukiongea na wazee wa haya maeneo huwa maelezo makini kabisa. Similarly maeneo fulani ya Morogoro hali ni hiyo hiyo. Kuna mahali nilishawahi kuambiwa eti barabara inakuwa imejengwa juu ya makaburi ya watu. Lakini sijui kuna uhusiano gani kati ya hao wafu ambao barabara inapita juu yao na ajali zinazojitokeza. Labda huwa wana tabia ya kuwaita wenzao wengine, waungane nao katika hali ya wafu.
 
nimesikia madereva wanalalamika kuwa kuna uchawi pale......
sasa naona mchangannyiko wa sayansi ya kisayansi na sayansi y auchawi.....
 
Ni kweli siasa zinatupa tabu,wanasiasa wanaingilia hata masuala ya kitaalamu,kwa mfano mchoro wa barabara Iringa -Dodoma baadhi ya wanasiasa wanataka ianzie Manispaa ya Iringa baadhi wanapinga kwa kuwa italeta msongamano wa magari mjini Iringa na barabara ni ndogo yaani magari,basi,lori zote zitakazo toka nyanda za juu kusini zitakazo elekea Dodoma zipitie mjini kulekea Dodoma !mvutano bado unaendelea sijui wamefikia wapi!
 
wabongo.. tuna kazi!!

Kuna vitu vingi sana muhimu kujadili kama kweli tunataka ufumbuzi au at leat kujua chanzo cha matatizo kwenye eneo hili; i did put one which is the craziest, lakini kwa siku hizi ambazo tunawapa akina Yahya, Mze wa ngurumo au tunaenda kwenye mikondo ya bahari kutafuta nguvu mimi naona tusiisahau, there are alot of believers out there...

Now back to senses;
reasons ni kama zifuatazo

  1. magari yetu ni mabovu - i am sure mengi ni used befor coming, tumeyatengenezea bodies bila standards, poor maintenance nk
  2. madereva wetu bado hawana elimu na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa uwepo wao barabarani
  3. Maendeleo yasiyona mipango miji, kusababisha human settlement sehemu na kuleta stress na anxiety kwa madereve hivyo inaongeza possibility ya mistakes
  4. ubou wa barabara unaoletwa na poor procurement procedures hivyo kutuletea contractors fake!
  5. Weak enforcement of road safety lawys
  6. corruption and poverty
  7. ubutu wa wataalam wetu wa vyuo husika kujihusisha na tatizo na solutions
  8. bado tuko karne ya nane kwenye infrastructure lakini tunapokea vitu vya karne ya 19
  9. irresponsible behaviour
 
nimesikia madereva wanalalamika kuwa kuna uchawi pale......
sasa naona mchangannyiko wa sayansi ya kisayansi na sayansi y auchawi.....
na mimi nimeyakuta pale... hasa baada ya ile ajali ya jioni kwenye eneo hilohilo, thanks God hapakuwa na fatalities
 
nimesikia madereva wanalalamika kuwa kuna uchawi pale......
sasa naona mchangannyiko wa sayansi ya kisayansi na sayansi y auchawi.....

Hakuna uchawi pale wala duniani popote.....ni uzembe tu wa watendaji wetu....magari yanapaswa kukaguliwa lakini ukimpa hela yule VEKO trafiki unapata makaratasi yote gari imekaguliwa..barabara ile ni finyu kwa wingi wa magari na umuhimu wake
 
Kuna vitu vingi sana muhimu kujadili kama kweli tunataka ufumbuzi au at leat kujua chanzo cha matatizo kwenye eneo hili; i did put one which is the craziest, lakini kwa siku hizi ambazo tunawapa akina Yahya, Mze wa ngurumo au tunaenda kwenye mikondo ya bahari kutafuta nguvu mimi naona tusiisahau, there are alot of believers out there...

Now back to senses;
reasons ni kama zifuatazo

  1. magari yetu ni mabovu - i am sure mengi ni used befor coming, tumeyatengenezea bodies bila standards, poor maintenance nk
  2. madereva wetu bado hawana elimu na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa uwepo wao barabarani
  3. Maendeleo yasiyona mipango miji, kusababisha human settlement sehemu na kuleta stress na anxiety kwa madereve hivyo inaongeza possibility ya mistakes
  4. ubou wa barabara unaoletwa na poor procurement procedures hivyo kutuletea contractors fake!
  5. Weak enforcement of road safety lawys
  6. corruption and poverty
  7. ubutu wa wataalam wetu wa vyuo husika kujihusisha na tatizo na solutions
  8. bado tuko karne ya nane kwenye infrastructure lakini tunapokea vitu vya karne ya 19
  9. irresponsible behaviour
hiyo bolded part hiyo ndio tatizo kubwa la waswahili!NI TATIZO KWA MAANA YA TATIZO.we can write and write here kuhusu IRRESPONSIBLE BEHAVIOUR...!tuache tu maanake tutajaza server.
 
Kwenye road design kuna mambo mawili yanazingatiwa.

1. Engineering Design
Inahusisha aina na uwezo wa barabara kubeba idadi/uzito fulani.

Mpaka sasa hivi, hii barabara haijaonesha udhaifu katika hili.

2. Geometric Design
Inahusiana na hali nchi na usalama wa watumiaji.

Kutokana na kutotaka kufuata haya. Watumiaji wanaweza kumlaumu mhandisi (designer). Kwenye Geometric Design ndipo tunapata mahali gani alama gani itumike kumuongoza mtumiaji.

Achilia mbali vilima na mabonde yaliyopo eneo husika, pia ukizingatia kuna alama ya mstari mnyofu kwenye barabara unaoashiria kuwa eneo hilo hauruhusiwi kupita gari la mbele yako. Lakini watumiaji wanadharau.

Swala la msingi sio kumatafuta mchawi wala mlozi. Sisi watumiaji wa vyombo vya moto hatufuati taratibu ya matumizi ya vyombo hivyo.

Utaratibu mzima wa mchakato wa utoaji leseni, uandikishaji wa magari, uthibiti wa magari nk. umekaa vibaya.

Kwa ujumla swala la usafirishaji ni swala nyeti katika kukua kwa uchumi wa nchi. Cha ajabu Tanzania hatuna Wizara ya Usafirishaji. Badala yake tuna wizara ya miundombinu. Swala la Usafirishaji na Miundombinu ni mambo yanayoenda sanjari lakini ni majukumu tofauti. Ndio maana inapotokea ajali kama hii hatujui nani wa kumlaumu.

Kwanza, mtu anaagiza gari, linakaguliwa na TRA na TBS.

Mtu akitafuta leseni, anajaribiwa na polisi anainunua TRA.

Mtu akifanya kosa, anakamatwa na Polisi. Gari likikiuka taratibu linakamatwa na SUMATRA.

Hii ni full confusion na ni swala la kuendekeza ulaji na sio utaratibu muafaka.

Maoni yangu:

Tuwe na wizara ya usafirishaji, itakayokuwa inatoa mwongozo mzima wa masuala ya usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo wa mchakato mzima wa kupata aina ya watu wa kuendesha vyombo hivyo (Driving License) na kuthibiti aina ya chombo na aina ya mzigo wa kubeba.

Hili linawezekana kama watu hawataweka siasa kwenye maisha ya wenzao. Tuweni wa kweli na tuachane na mambo ya kuwa eti sisi ni taifa changa au masikini. Hizi ni fikra duni zinazoturudisha nyuma kila kuchapo.

Watu wasilete siasa katika mipango ya maendeleo. Tufanye uchunguzi wa kisayansi na watumie majibu yanayopatikana kupangia bajeti na kutekeleza. waachane na ubinafsi. Kila kipindi idara/wizara inaongezewa mafungu lakini hatuoni matokeo ya hizo pesa. Swali huwa zinatumikaje? WIZI MTUPU!

Tanzania unaweza kupiga hatua ila siasa inakushika shati. AAAAGGGHH!
 
Ndugu yangu,
Hapa umetoa ukweli haswa....shukrani.Wingereza ambao sisi hatuchoki kuiga sera zao...hasa sheria wana Ministry of Transport (MoT) amabayo husimamia mabo yoote ya usafiri toka sera mpaka utekelezaji wake.Hii SUMATRA naona si chochote zaidi ya watu kupata ajira tu...haina meno.Suala la leseni tumelisema sana lakini mpaka leo watu wanafikiri watanufaika vipi...hu mfumo wa Class A,B,C umepitwa na wakati na serikali inpoteza sana mpato kwa sababu lesseni nyingi zintengenezwa mitaani ikiratibiwa na TRAFFIC POLICE.
Mtazamo wangu:
a)Hawa trafic wanakaa sana kwenye idara hii mpaka wanataka kuchana uniform zao kwa obesity.Naamini kule CCP Moshi askari husomea sekta zote na hakuna specialization,kwa hiyo ni vema sasa tukawazungusha...leo kulinda benki,kesho mahakamani,jumatau ongoza magari au kama hili haliwezekani basi wahamishwe vituo sio askari huyohuyo miaka nenda rudi yuko mizani kibaha.
b)Mfumo wa leseni umebadilishwe mara moja kwa kuondoa hizo class A,B,C na kuleta lesseni kutokana na aina ya gari Personal,Light passenger(taxis and the like),mid passenger(hizo hiace),passenger service(mabasi makubwa),light comercial,mid commercial and heavy commercial trucks)na mtu aruhusiwe kuomba zaidi ya leseni moja na sio sasa mwenye class C anaacha kuendesha gari ya mzigo na kupewa basi ambavyo ni vitu viwili tofauti.Kama mtu ni dereva wa basi kama kazi yake na ana gari binafsi basi aombe leseni mbili-personal na heavy commercial kusudi aonyeshe leseni yake pale anapoendesha moja ya hayo magari-la kazi au binafsi.
c)Magari yakaguliwe jamani:TBS na SUMATRA na sio wale VEKO sijui wa traffic
 
Barabara hii inahitaji kupanuliwa angalau iwe ya njia nne kuanzia Dar mpaka Morogoro kwa sababu asilimia kubwa ya magari yaendayo mikoani na nchi jirani yanapitia katika barabara hii, njia mbili zimepitwa na wakati hasa wakati huu na unaokuja.

Ajali nyingi zinahusisha magari wakati wa kupishana, na hasa wakati mwengine inapotokea gari kuharibika barabarani kitu ambacho kinamzuia dereva wa gari kuona mbele ya barabara.

Kitu kingine ni kuwa lazima Polisi wa usalama barabarani wafanye tathmini ya leseni zinazotolewa, kuna madereva wengi hawana uzoefu wa kuendesha magari makubwa lakini wana leseni ya class C. Bila ya kurekebisha kasoro hizo hizi ajali hazitokwisha na zitakuwa zinaangamisha maisha ya watu wetu kila siku.
 
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?

Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.

Kuna utafiti ulifanywa na wataalamu wa BICO miaka kama miwili iliyopita na wakatoa ripoti inayoelezea sababu za accidents Tanzania. Kwa ufupi takribani asilimia sabini na tano (75%) ya ajali nchini zinatokana na makosa ya kibinadamu ya madereva na watumiaji wengine wa barabara. Na asilimia zilizobaki zinatokana na mambo mengine kama hali ya barabara, ubovu wa vyombo vya usafiri na hali ya hewa.

Ukiangalia kwa makini eneo la Kibaha na maeneo yanayo karibia hapo utagundua kuwa lina vilima na mabonde mengi. Na kwa sasabu hiyo barabara iliyojengwa ina miteremko mikali, milima, kona kali na madaraja mengi ambavyo ni vyanzo vikubwa sana vya ajali kwenye eneo hilo. Hasa kwa kuzingatia Tanzania madereva halisi ni asilimia 30% tu. Asilimia 70% ya madereva nchini hawajapitia kwenye mafunzo ya udereva na wala hawana maarifa yanayowawezesha kufanya kazi ya udereva kwa ueledi unaotarajiwa.

Matokeo ya udereva duni wa madereva wetu ni kuwa wana 'overtake' kwenye milima, kona, madaraja, hata bila ya kuwa na uhakika wa nini kinakuja upande wa pili wa barabara.

Kwa mfumo ulivyo sasa hivi mtu anajifunza udereva chuo cha Veta (kama ni mtu anayejali maana wengine hata udereva hawajifunzi maana wananunua leseni kama njugu), anajaribiwa na polisi kitengo cha usalama wa barabarani, na anapewa leseni na TRA na baada ya hapo hakuna chombo chochote kinachosimamia udereva kama taaluma nyeti inayoathiri maisha na mali za watu. Hivi vyombo vitatu vinavyoshiriki katika kumuandaa dereva havina mawasiliano yoyote zaidi ya kuangalia nyaraka ambazo nyingi zinaghushiwa hapa mjini.

Kwa hiyo kwa ufupi bila kushughulikia mfumo wa uandaaji wa madereva na udhibiti wa leseni na madereva hatuwezi kuondoa tatizo la ajali. Vilevile bila ya kuondoa rushwa katika upatikanaji na ukaguzi wa leseni nchini hatuwezi kuondoa ajali.

Hivyo kwa mtazamo wangu kama hatutawekeza katika kusimamia mafunzo ya madereva, mitihani ya na majaribio ya waliohitimu udereva vyuoni na utoaji wa leseni nchini kamwe hatutaweza kushinda hii vita ya ajali nchini.
 
Back
Top Bottom