Abuse..( Dhuluma)

Mkuu CPU mlikuwa mnahadithiana haya wapi? tehetehetehetehe ila nimeona tu kwa kusoma huyo mume ana wivu sana hadi inapelekea kutokujiamini kabisa,inaonekana huyo bibie ni mrembo wa haja. Mke anatakiwa amwelewe huyo mumewe vizuri ili kuepusha mambo kma hayo, akitoka mwenyewe avae nguo ndefu akiwa nae avae hizo fupi. Mh ndoa hizi zina vijimambo haswa

My dia
Hizi sio hadithi
Ni habari ya kweli . . .
 
Hoja yako ni ndefu sana na kwa mtazamo wangu haiwezi kujibiwa kwa upana wake. nadhani inabidi kuchagua eneo la kujibu kwa sababu hizo abuse ziko tofauti na inawezekana kabisa zinakasabishwa na vitu tofauti na hata namna ya kuzitatua ni tofauti from each other. kwa upande wangu ntachangia kuhusiana na phyisical abuse i.e. kupiga/kupigwa mwili.

ntaanza na mfano wa familia yangu. sie tuko wanane kwa baba na mama. 7 wanaume. tuna dada mmoja. katika maisha yetu, mimi ni wa 6, sijawahi kumwona baba akimpiga mama hata siku moja. mama mwenyewe hulikiri hili kila cku. hali kadhalika, hatujawahi kupigwa na baba hata cku moja. ni kaka yetu mmoja ambaye aliwahi kupigwa na bb na ni kwa vile alimpiga mama! nadhani kwa malezi hayo, hata nasi hatujawahi kuwapiga spouses na watoto wetu hata siku moja! hapa nilipo kuinua mkono wangu kumpiga mtu, hata kama ni mwanaume mwenzangu, ni ngumu sana. nasikia kabisa mkono ni mzito.

nadhani hali ingekuwa tofauti kama tungekua kwenye familia ambayo kupigwa/piga ni hali ya kawaida. so kwa ufupi malezi yanaweza kusababisha abuse, walau za aina hii (physical abuse). Nadhani mchango wangu unatosha kwa sasa
Sante sana kwa mchango wako..
Naelewa topic yangu ni ndefu sana
Kabla sikuianzisha hii thread niliwaza sana
nikaona kwa hizi dhuluma kwa njia moja au nyingine zimeingiliana.. mfano huo wa physical abuse utakuta mtu anatukanwa (verbal abuse) au utakuta mtu anakuchukia(hate) ..same thing for sexual abuse... nadhani utakuwa umenielewa kidogo
kwa nini nimeziweka zote...
 
Naomba niwasilishe mada yenye aina fulani ya (Neglect)kutelekezwa)

Mariah-Carey-and-Nick-Cannon.jpg
mariah%20carey.nick%20cannon.2.thumbnail.jpg

Mwanamziki wa miondoko ya R&B nchini Marekani, Mariah Carey amejifungua mapacha wawili wa kike na kiume aliozaa na mume wake Nick Cannon.

Uhusiano wao ni kwamba, Nick na Mariah Carey walidumu ktk uhusiano wa kimapenzi kwa wiki 6 tu tangu wajuane hadi kuamua kuoana rasmi April 30, 2011.
(Angalizo hapa: Uhusiano ukae muda gani kabla ya ndoa, au kuanza mapenzi?!!! Au kwa wale wanaotaka mpaka ipite miaka kadhaa ndio ionekane wakioana watadumu ndoani)

Mahusiano yao yalijaa ukosoaji kutoka sehemu mbalimbali, wakisema Nick hakustahili kuwa na mwanamke huyo kwa kuwa alikuwa amezidiwa sana umri na Mariah Carey. Wanasema inawezekana Nick amerubuniwa na huyo mwanamke kutokana na utajiri wake. Walifunga ndoa wakati Nick ana miaka 27 na Carey 38.
(Hapa naanza kufananisha na akina Aibu-Rose Ba . . . na Jafa-Rahimuu)

Harusi yao ilihudhuriwa na wageni 24 tu wa upande wa Mariah, na hakukuwa na ndugu kutoka kwa Nick japo walipewa taarifa zote. (Huu sio utekelezwaji jamani???)
 
Wengi wetu tukibadilika watabakia wachache mwishowe wataona aibu, ila kwa kiukweli hili tatizo halitaweza potea kabisa ila tunaweza lipunguza kwa kiasi kikubwa sisi wenyewe
Sante sana Gaga
Lakini naomba ukumbuke wengi ambao
wana abuse wengine wana matatizo mengine
Mfano wengi ni addicts wa vitu kana alchohol, drugs, etc .. kweli watu kama hao itakuwa rahisi kwao kuacha hizo dhuluma kwa kuangalia mfano wa watu wengine??
 
Naomba niwasilishe mada yenye aina fulani ya (Neglect)kutelekezwa)

Mariah-Carey-and-Nick-Cannon.jpg
mariah%20carey.nick%20cannon.2.thumbnail.jpg

Mwanamziki wa miondoko ya R&B nchini Marekani, Mariah Carey amejifungua mapacha wawili wa kike na kiume aliozaa na mume wake Nick Cannon.

Uhusiano wao ni kwamba, Nick na Mariah Carey walidumu ktk uhusiano wa kimapenzi kwa wiki 6 tu tangu wajuane hadi kuamua kuoana rasmi April 30, 2011.
(Angalizo hapa: Uhusiano ukae muda gani kabla ya ndoa, au kuanza mapenzi?!!! Au kwa wale wanaotaka mpaka ipite miaka kadhaa ndio ionekane wakioana watadumu ndoani)

Mahusiano yao yalijaa ukosoaji kutoka sehemu mbalimbali, wakisema Nick hakustahili kuwa na mwanamke huyo kwa kuwa alikuwa amezidiwa sana umri na Mariah Carey. Wanasema inawezekana Nick amerubuniwa na huyo mwanamke kutokana na utajiri wake. Walifunga ndoa wakati Nick ana miaka 27 na Carey 38.
(Hapa naanza kufananisha na akina Aibu-Rose Ba . . . na Jafa-Rahimuu)

Harusi yao ilihudhuriwa na wageni 24 tu wa upande wa Mariah, na hakukuwa na ndugu kutoka kwa Nick japo walipewa taarifa zote. (Huu sio utekelezwaji jamani???)

Wakati mwingine inabidi uangalie kile kinachokufurahisha wewe zaidi ya kitakachowafurahisha wanaokuzunguka maana furaha yao inaweza isiwe yako.Hicho ndicho alichofanya Nick....na sidhani kama sasa hivi hicho kitendo cha ndugu zake kumsusia kinamuumiza kichwa maana ana furaha na anayafurahia maisha yake....wanaobaki wanang'aa macho ni hao waliomtelekeza!!

BTW kwanini umeifanya hii mada tegemezi?????
 
Ni rahisi kuacha ikiwa wataacha hivyo vianzilishi!!
At the end of the day vyote ni visingizio tu na havihalalishi kufanyia watu wengine mambo mabaya!
 
CPU mambo ya ndoa,harusi yanamatatizo yAke ...
kama ni kweli ilikuwa hivyo basii huu ni utekelezaji..lakini utekelezaji niliokuwa naugusia zaidi ni kama ule baba anamkataa mwanae au mama anamtupa mtoto .. vitu ambavyo vinazunguka jamii yetu...
 
Sijakuelewa????
 
Utekelezaji ni utekelezaji tu, tena huu wa Mariah na Nick ni mbaya zaidi coz hata wazazi wa Nick hawajagusa harusini
Utapuuzia utekelezaji wa wazazi kwa vile umekuwa mtu mzima????
Ndugu uliokuwa nao tangu unakuwa na hatimaye umekuwa mtu mzima.
Wamekufundisha mazuri na mabaya
Wamekulelea, wamekufanya ujisikie sehemu ya dunia
Huwezi dharau mchango wa ndugu bana
Uliza waliozaliwa hawajui ndugu zao ndio utajua maumivu ya utekelezaji wa ndugu.
Mpenzi akikutekeleza unaweza kupata mwingine, mzazi akikutekeleza je????
 
Ni rahisi kuacha ikiwa wataacha hivyo vianzilishi!!
At the end of the day vyote ni visingizio tu na havihalalishi kufanyia watu wengine mambo mabaya!

Lizzy nadhani unafahamu mtu
alchoholic ilivyokuwa ngumu kuacha pombe..
Au drug addict... je kweli unafikiri wanaweza kuviacha tu bila msaada wowote..?
 
Wakati mwingine inabidi uangalie kile kinachokufurahisha wewe zaidi ya kitakachowafurahisha wanaokuzunguka maana furaha yao inaweza isiwe yako.Hicho ndicho alichofanya Nick....na sidhani kama sasa hivi hicho kitendo cha ndugu zake kumsusia kinamuumiza kichwa maana ana furaha na anayafurahia maisha yake....wanaobaki wanang'aa macho ni hao waliomtelekeza!!

BTW kwanini umeifanya hii mada tegemezi?????

Isitoshe mi siwezi dharau umuhimu wa ndugu hata kidogo.
Yaani ndugu, ikiwemo wazazi na ndugu zako wa tumbo moja wanakususa unaona ni kawaida????
Yaani kwa vile umekuwa mtu mzima unaweza kujiamulia mambo yako basi unaona sawa tu???
Ukitekelezwa na ndugu (hata kama unapata furaha na ndoa yako) kwako unaona maisha yako yatakuwa na raha???
Acheni mzaha . . . .
 
Lizzy nadhani unafahamu mtu
alchoholic ilivyokuwa ngumu kuacha pombe..
Au drug addict... je kweli unafikiri wanaweza kuviacha tu bila msaada wowote..?

Akitaka anaweza sana!!
Mjomba wangu mmoja alikua anapenda gongo huyo....yani hata tukiwa sehemu tunakula na ana bia zake kadhaa mezani atajifanya anaenda chooni akirudi yuko njwiii!!Alisemwa mpaka kila mtu akachoka wakaamua wamuache siku zikimharibia mahali labda atajifunza!!Siku ya siku tulishangaa tu amebadilika kila kitu na mchumba anatambulisha!Mwenyewe aliona hazimsaidii zinmwaibisha tu na kumkosesha mapenzi ya ndugu zake maana wote wamemchoka.Hata hatujui nini kilimshawishi na vipi aliacha tunafurahia tu matokea....miaka mitatu sasa imepita ameo na mtoto juu anafurahia tu maisha yake!!!

Mtu asipoamua mwenyewe kwamba hichi kitu sikitaki tena hata ukimpa msaada hataupokea!!Kwahiyo stepu ya kwanza siku zote ni mtu kukubali kwamba ana matatizo na anataka kuondokana nayo....hapo sasa ndo kama anahitaji msaada unampa na kama anaweza kujidhibiti mwenyewe Mungu ashukuriwe!
 
Isitoshe mi siwezi dharau umuhimu wa ndugu hata kidogo.
Yaani ndugu, ikiwemo wazazi na ndugu zako wa tumbo moja wanakususa unaona ni kawaida????
Yaani kwa vile umekuwa mtu mzima unaweza kujiamulia mambo yako basi unaona sawa tu???
Ukitekelezwa na ndugu (hata kama unapata furaha na ndoa yako) kwako unaona maisha yako yatakuwa na raha???
Acheni mzaha . . . .

Kwahiyo unatakaje???Asiomuoe mwanamke anaempenda kwasababu tu ni mkubwa kuliko yeye na ndugu hawafurahii hilo???Hao watoto waliozaliwa hawatataka kuwajua kwasababu wamezali na mama mkubwa....au labda kwa vile ni mzungu???Nwy wote huo ni ubinafsi wa kibinadamu!!Yeye angeacha kumuoa yule binti hao ndugu zake wasingefaidika chochote na kuoa kwake vile vile hawajapungukiwa chochote kwahiyo wote ni ubinafsi usio na maana!!!Ila kwa upande wa muoaji kwa kuoa amefaidika kwa kumpata anaewezana nae pia famili yake mwenyewe....asingemuoa labda angekua anazunguka toka kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine...then what???

Hiyo familia kama haimheshimu yeye na maamuzi yake ukizingatia kwamba hayamuumizi yeyote sioni kwanini unasema yeye ndo mwenye dharau!
 
Utekelezaji ni utekelezaji tu, tena huu wa Mariah na Nick ni mbaya zaidi coz hata wazazi wa Nick hawajagusa harusini
Utapuuzia utekelezaji wa wazazi kwa vile umekuwa mtu mzima????
Ndugu uliokuwa nao tangu unakuwa na hatimaye umekuwa mtu mzima.
Wamekufundisha mazuri na mabaya
Wamekulelea, wamekufanya ujisikie sehemu ya dunia
Huwezi dharau mchango wa ndugu bana
Uliza waliozaliwa hawajui ndugu zao ndio utajua maumivu ya utekelezaji wa ndugu.
Mpenzi akikutekeleza unaweza kupata mwingine, mzazi akikutekeleza je????
Nimekubaliana nawe tangu mwanzo kama kweli ilitokea ni utekelezaji....

Kujibu kabisa mwisho wa sentensi yako"mzazi akikutekeleza je"? That's exactly my point..
Sasa we imagine mzazi anakuacha ukiwa mdogo unaokotwa au unatunzwa na mtu mwingine.. katika maisha yako yote unakaa na kuwaza hivi mama na baba yangu ni nina? Hivi ni raha gani kutwanzwa na mzazi wako halisi...?? Mmhh I'm just wondering do I have any siblings??? Utekezwaji wote ni mmbaya lakini kwangu binafsi naona ule wa kuachwa tangu utotoni ndo mmbaya zaidi... ni sawa na kuishi maisha yako yote gizani....
 
Akitaka anaweza sana!!
Mjomba wangu mmoja alikua anapenda gongo huyo....yani hata tukiwa sehemu tunakula na ana bia zake kadhaa mezani atajifanya anaenda chooni akirudi yuko njwiii!!Alisemwa mpaka kila mtu akachoka wakaamua wamuache siku zikimharibia mahali labda atajifunza!!Siku ya siku tulishangaa tu amebadilika kila kitu na mchumba anatambulisha!Mwenyewe aliona hazimsaidii zinmwaibisha tu na kumkosesha mapenzi ya ndugu zake maana wote wamemchoka.Hata hatujui nini kilimshawishi na vipi aliacha tunafurahia tu matokea....miaka mitatu sasa imepita ameo na mtoto juu anafurahia tu maisha yake!!!

Mtu asipoamua mwenyewe kwamba hichi kitu sikitaki tena hata ukimpa msaada hataupokea!!Kwahiyo stepu ya kwanza siku zote ni mtu kukubali kwamba ana matatizo na anataka kuondokana nayo....hapo sasa ndo kama anahitaji msaada unampa na kama anaweza kujidhibiti mwenyewe Mungu ashukuriwe!
Dahhhhh
ulichoandika hapo especially hapo mwisho
Oprah mwanafunzi hahahah lol asantesana
 
Kwahiyo unatakaje???Asiomuoe mwanamke anaempenda kwasababu tu ni mkubwa kuliko yeye na ndugu hawafurahii hilo???Hao watoto waliozaliwa hawatataka kuwajua kwasababu wamezali na mama mkubwa....au labda kwa vile ni mzungu???Nwy wote huo ni ubinafsi wa kibinadamu!!Yeye angeacha kumuoa yule binti hao ndugu zake wasingefaidika chochote na kuoa kwake vile vile hawajapungukiwa chochote kwahiyo wote ni ubinafsi usio na maana!!!Ila kwa upande wa muoaji kwa kuoa amefaidika kwa kumpata anaewezana nae pia famili yake mwenyewe....asingemuoa labda angekua anazunguka toka kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine...then what???

Hiyo familia kama haimheshimu yeye na maamuzi yake ukizingatia kwamba hayamuumizi yeyote sioni kwanini unasema yeye ndo mwenye dharau!

Pamoja na yote hayo, bado siwez kujifanya nitaishi kwa raha huku nimesusiwa na wazazi. Hata kama nimekuwa vipi.
Pamoja na kwamba unaweza kusema umekuwa na utafanya maamuzi yako mwenyewe, its fine, kususiwa na wazazi waliokuzaa ni kitu ambacho kitakuumiza maisha yako yote. Kwanza ufahamu kwamba mimi sina tatizo la mtu kuoa hata kikongwe, si kapenda bana. Na sidhani kama kwa mzazi makin anaweza kumsusa mtoto wake kwa kuoa mtu mkubwa zaidi yake tu. Hii si sababu ya maana hata kidogo.

Sijajua sababu ya kususiwa na wazazi wake ni nini, lakin naamini haiwezi kuwa ukubwa na Mariah Carey tu. Huenda kuna kitu cha ziada walitaka kumweleza mwanao ambacho aliamua kupuuzia pengine kwa sababu kapata mwanamke tajiri. Hii ni kasumba ambayo vijana wengi wadogo wanayo, haijalishi ni wa bongo au Ulaya.

Kwangu mimi, hata kama maamuzi wa kuoa nani nafanya mimi, bado nitaweka umuhimu mkubwa kwa wazazi wangu pia. Wao wameona mengi, wamepitia mengi. Labda kama ni wazazi wa ovyo.
Wamekususa ndugu zako wote, then uone ni kawaida???? Hapana aisee!!!!!!!
Labda kama nilizaliwa sijui ndugu yoyote. Otherwise, siwezi ishi kwa amani.
 
Nimekubaliana nawe tangu mwanzo kama kweli ilitokea ni utekelezaji....

Kujibu kabisa mwisho wa sentensi yako"mzazi akikutekeleza je"? That's exactly my point..
Sasa we imagine mzazi anakuacha ukiwa mdogo unaokotwa au unatunzwa na mtu mwingine.. katika maisha yako yote unakaa na kuwaza hivi mama na baba yangu ni nina? Hivi ni raha gani kutwanzwa na mzazi wako halisi...?? Mmhh I'm just wondering do I have any siblings??? Utekezwaji wote ni mmbaya lakini kwangu binafsi naona ule wa kuachwa tangu utotoni ndo mmbaya zaidi... ni sawa na kuishi maisha yako yote gizani....

Ni sawa ulichosema . . . . Nakubali 100%
Labda pengine hukutaka nilete hii habari ya utekelezwaji wa aina hii ambao unakuwa unafanyiwa ukiwa mtu mzima, hasa ktk mahusiano ya ndoa, hapo nitakuelewa. Lakin mi nilichoelewa ni kwamba hata utekelezwaji hata wa aina hii ktk mahusiano pia unaweza ukaishi maisha yako yote yaliyobakia MPWEKE
 
Pamoja na yote hayo, bado siwez kujifanya nitaishi kwa raha huku nimesusiwa na wazazi. Hata kama nimekuwa vipi.
Pamoja na kwamba unaweza kusema umekuwa na utafanya maamuzi yako mwenyewe, its fine, kususiwa na wazazi waliokuzaa ni kitu ambacho kitakuumiza maisha yako yote. Kwanza ufahamu kwamba mimi sina tatizo la mtu kuoa hata kikongwe, si kapenda bana. Na sidhani kama kwa mzazi makin anaweza kumsusa mtoto wake kwa kuoa mtu mkubwa zaidi yake tu. Hii si sababu ya maana hata kidogo.

Sijajua sababu ya kususiwa na wazazi wake ni nini, lakin naamini haiwezi kuwa ukubwa na Mariah Carey tu. Huenda kuna kitu cha ziada walitaka kumweleza mwanao ambacho aliamua kupuuzia pengine kwa sababu kapata mwanamke tajiri. Hii ni kasumba ambayo vijana wengi wadogo wanayo, haijalishi ni wa bongo au Ulaya.

Kwangu mimi, hata kama maamuzi wa kuoa nani nafanya mimi, bado nitaweka umuhimu mkubwa kwa wazazi wangu pia. Wao wameona mengi, wamepitia mengi. Labda kama ni wazazi wa ovyo.
Wamekususa ndugu zako wote, then uone ni kawaida???? Hapana aisee!!!!!!!
Labda kama nilizaliwa sijui ndugu yoyote. Otherwise, siwezi ishi kwa amani.

Swala sio kuona kawaida.....swala ni kupima uzito wa wanachokisusia na kujua je ni kwa faida ya nani????
Baada ya hapo ndo mtu unajua utakapojisikia vibaya ni kwasababu umesababisha wakususie au kwasababu hawataki kukuunga mkono??Vyovyote vile ndugu/jamaa/na marafiki wanatakiwa waondoe ubinafsi kwenye maamuzi yao.Hata kama kuna kitu hakikuwafurahisha kama hakimuumizi yeyote wangekuwepo then waondoke....kwani inawagharimu nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom