abiria

Badu

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
407
106
Hii imetokea juzi ruti ya kutoka
Sinza kuelekea Posta mishale ya
saa 3 asubuhi. Kulikua na daladala imekula nyomi
kama kawaida asubuhi kwenda
town watu wanajaa tangu
mwanzo wa basi kwa hiyo njiani
kunakua hakuna haja ya kupakia
tena…… Madereva wengi huamua
kuchepuka na kupita vichochorni
watokee magomeni kasha
washushe jangwani, faya waingia
mjini mapema waende na kugeuka
fasta. Juzi dereva mmoja akafanya
hivyo ili apite kama tandale uku
aibuke magomeni kisha aenda
town… kwa bahati mbaya Trafiki
walikuwepo alikopita
akasimamishwa.. TRAFIKI: nyie ndio tunawatafuta
siku zoote DEREVA: kwanini muheshimiwa TRAFIKI: mnajifanya mna haraka
humu duniani kuliko watu wote
sio?? DEREVA: hapana muheshimiwa ila
hii gari imekodishwa kwa ajili ya
harusi. (abiria kwa nyuma wanasikilizia
kinachoendelea) TRAFIKI: (Aking’aka) aaah
unanifanya mi zumbukuku sio…
yani ndio wajizidishia makosa sasa
gari linawekwa ndani na we
mwenyewe dereva unaenda ndani
(selo). Abiria kusikia ivo, mmoja kwa
nyuma akaanzisha, …dada huyoo anaolewa…. Dada
huyoo anaolewa.. (abiria wote wakaanza kuitikia) Mahariiiii..... ishatolewaaa... Dada
huyooo anaolewa….dada
huyooooo anaolewa….!!! (trafiki akaona apo ameshindwa
akaruhusu gari
liendeleee…)
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom