Abiria zaidi ya 60 wanusurika kufa baada ya basi kupinduka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
ABIRIA zaidi ya 60 waliokuwa wakisafiri katika basi la abiria linalotambulika kwa jina la Harambee Bus linalofanya safari zake kati ya Dar Arusha walinusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka huko Msata Wilayani Bagamoyo Tukio hilo lilitokea jana ambapo basi la abiria lililokuwa na namba za usajili T362 AFN na lori lililokuwa na namba za usajili T714 ALM kutaka kuvaana na kupelekea basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa lori hilo.

Eneo lililotokea ajali hiyo Msata kuna kona kali ambapo lori hilo lilikuwa likitokea Arusha kuja jijini Dar es Salaam.

Lori hilo bila kuonyesha ishara yoyote kama linataka kuingia kwenye kituo cha mafuta lilikata kona kuingia kituoni hapo na kusababisha dereva wa basi ambaye alikuwa anaendelea kunyoosha barabara bila kutambua kuwa lori hilo litaingia kituoni hapo kuwa katika wakati mgumu wa kulikwepa lori hilo.

Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu hao na kukwepa wasivaane na lori hilo basi hilo lilipinduka pembezoni mwa barabara.

Hata hivyo katika tukio hilo hakuna abiria aliyepoteza maisha bali kulipatikana na majeruhi kadhaa ambapo walikimbizwa katika hospitali ya Msata Wilayani Bagamoyo kwa matibabu.

nifahamishe.com
 
Last edited by a moderator:
Mungu ashukuriwe kwa kunusuru ajali hiyo ambayo ingeleta maafa. Madreva wengine wanavuta sigara kubwa hivyo sheria zingine za barabarani hawazijali.
 
Mungu ashukuriwe kwa kunusuru ajali hiyo ambayo ingeleta maafa. Madreva wengine wanavuta sigara kubwa hivyo sheria zingine za barabarani hawazijali.

kwa kweli kuna haki ya kumshukuru Mungu, lakini kwa asilimia kubwa ajali nyingi ni uzembe wa madereva, hivi huyo dereva wa basi alikuwa umbali gani kutoka kwa mwenye Lori, na kama hilo eneo lina Petrol station ni obvious lilikuwa karibu na ka-center sasa alikuwa na speed gani ya kuweza kupindua gari kama sio over speeding hiyo,
hata kama huyo dereva wa lori akuonyesha hiyo ishara lakini principle zipo palepale kwamba dereva uwa anaendesha magari matatu, lake analoendesha, lililo mbeleyake na lililo nyuma yake, kwa mtazamo wa hiyo ajali huyo dereva alikuwa anaendesha gari lake tu,
 
Back
Top Bottom