Abiria watakaosimama Kwenye Ndege Kusafiri Bure

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Wednesday, July 08, 2009 5:23 AM Abiria wa shirika la ndege la Ryanair la Ireland ambalo linasifika kwa tiketi za bei rahisi duniani watakuwa wakisafiri bure kwenye ndege za shirika hilo iwapo watakubali kusimama wakati wa safari zao. Bosi wa Ryanair Michael O'Leary aliiambia televisheni ya Sky News ya Uingereza kuwa shirika hilo lina mpango wa kuondoa siti za nyuma kwenye ndege zake ili kuwezesha abiria kusimama wakati wa safari zao. Abiria watakuwa wakisimama kama vile wanavyosimama kwenye daladala katika safari ambazo hazitachukua muda wa zaidi ya lisaa limoja na nusu. "Tutazitoa siti zote kwenye mistari mitano au sita ya nyuma na kuwaauliza abiria wetu 'Unataka kusimama kwenye ndege? kama utakubali kusimama basi utasafiri bure' " alisema O'Leary. Kampuni hiyo imeongea na Boeing kuangalia uwezekano wa kuzibadilisha ndege zao ziweze kubeba abiria wa kusimama au kama itashindikana basi watengeneze ndege mpya zenye uwezo huo. Hata hivyo shirika la ndege la Ryanair ambalo lina makazi yake makuu nchini Ireland litabidi lisubirie ruhusa kutoka kwa mamlaka ya usafiri wa anga ya Ireland. Hivi karibuni shirika moja la ndege nchini China liliomba ruhusa toka serikali ya China kuanzisha safari za abiria wa kusimama kama kwenye daladala nchini humo. Tofauti na Ryanair shirika hilo halikusema kama litaondoa baadhi ya siti kwenye ndege zao ili kupisha abiria watakaopenda kusimama.

nifahamishe.com
 
Last edited by a moderator:
Lol! Hii nayo mpya. Ila tu kwa taarifa ni kuwa, hawa RyanAir ni wanjanja sana. Si kweli abiria atasafiri bure kabisa bali kuna pesa lazima alipe indirectly. Kwa mfano sasa hivi utakuta safari ya kutoka London kwenda Copenhagen, Denmark ni Paundi 5 (paundi tano tu). Ila kuna charges zingine kibao mfano lazima mabegi yako ulipie, checking in fees, taxes etc. japo bado wako rahisi ukilinganisha na mashirika mengine ya ndege.
 
Duh!!!!! hii naona ni kamba style. Hivi kweli kuna kitu kama hicho au ni porojo tu?
 
Back
Top Bottom