Abiria wa Dar - Moshi/Arusha: Highway restaurant wanatulisha nyama mbichi

si bora miezi mitatu...huwa kuna kunguru pia wa kuchoma unaambiwa ni kuku
...teh! tehh! Preta unanikumbusha stesheni ya reli ya kati inaitwa Saranda utakutana na paja ya kuku kubwa utadhani digidigi...lakini unameza na maisha yanaendelea...
 
Nyama zingine hadi ziive ipo kazi,ulijaribu kucheki kwa makini ujue ni nyama gani?usianze kutapika, i mean ng'ombe wa aina gani asieiva?
 
Polee sana M2 wangu.
Hizi Kero zizoee tu unless uwe na private usafiri.
Hilo mbona Dogo sana.
Kuna hii barabara ya Mbeya Dar. Mkuu watu wanasukumizwa mgahawa wa aljaazira. ****** mnaingia kwa foleni coz unakuta mabasi yaendayo Dar na yatokayo Dar yanakutana pale mda mmoja. mwanangu huu mziki sii mchezo.
Tunashukuru wale wamasai pale mvemero, kwani pale mabasi yanoyotoka Dar lazima yasimame pale watu wachimbe Dawa. Basi hapa nakamata minyama ya Mbuzi kisawasawa.
Tukifika pale kwenye Hoteliu yao ya aljaziira mi mluzi mwembamba hata kwenye gari sishuki.
But hii ndo Bongo yetu bana
 
Nadhani kuna variety, if you think ya kuchoma siyo choice yako basi nenda kwenye buffet. Na mtoto unayesema hakula, kwanza nyie wakubwa ndiyo wakulaumiwa, kwanini ukamnunulie mtoto nyama choma wakati kuna chakula cha kupika kizuri tu sana na ina mboga za majani na amatunda? (balanced diet). Just take a little different from what you normally like au hiyo ndiyo outing yako?
 
Major, yaani ni afadhali hapo Highway unakula chakuala fresh kule wale jamaa zangu wa Liverpool kule Mombo yaani usafi ni zero, na chakula cha 3,500/- utadhani cha elfu mia tano.

Ingawa ukweli unabaki pale pale kuwa hizi hoteli za njiani zinatuibia sana, thamani ya vyakula wanavyotuuzia ni kubwa kulinganisha na ubora wa vyakula vyenyewe. Yaani ni vile tu wanasema MSAFIRI KAFIRI, ukweli unabaki pale pale kuwa WANATUIBIA!
 
Labda TRL ikifufuka maana njia ile sasa ni malisho ya mifugo.
 
acheni ulafi,safari ya masaa sita unataka ule minyama wee utadhani uko kwenye barbecue party,kama zimekushinda piga biscuit na soda yako poowa,kisha ukifika arusha,moshi,agiza msinia wa nyama iliyochomwa ikaiva.

nilitaka kusema hivi hio safari ni 24hrs???kunywa full breakfast nyumbani then kula chakula ukifika destination yako,tusiendekeze kula hovyo njiani,unaweza kupata magonjwa ya tumbo njiani mkaanza kusumbua madereva wasimame kila dk 10
 
Kwako Major Mkandala,

Kwanza napenda nikupe pole kwa lililokusibu. Lakini katika hayo malalamiko yako sijaweza kujua ni kwa mara ngapi yalikupata hayo. Kwani katika biashara ya kuhudumia zaidi ya watu 200 kwa kila dakika 30 si mchezo.

Pia napenda kujua msimu ambao safari yako ilikusibisha hayo maswahibu hayo. Elewa kuwa pale Highway ni moja ya sehemu bora zaidi kupata msosi. Ila inategemea unafika pale saa ngapi na ni msimu gani. Kwa mfano msimu wa sikukuu ni bora ule pale ukiwa na private transport. Mkigongana pale mabasi zaidi ya matatu, kuna hatari ya kupata nyama mbichi. Tatizo lipo kwa wateja wenyewe, kwani wengi wa maeneo ya Moshi - Arusha hawapendi nyama iliyokaushwa sana na kwa sababu mahitaji ni makubwa, na wana uchu wa nyama, wanalazimisha hata kama wakiambiwa kuwa ni bado kidogo ili mradi waende na muda.

Lakini embu fananisha Darajani, Liverpool, Transit, Bufalo na Highway. Utaona ni viwango tofauti kabisa. Enzi za pale Transit - Korogwe chakula kilikuwa ni cha ajabu ajabu sana, muhudumu anakuletea supu anatia kidole kwenye supu. Matokeo yake pamechoka pamefungwa.
 
Ndugu wapendwa kuna hii bar imefunguliwa majuzi kwa wanaopenda kusafir na dar express ,saydady,metro na mengineyo huwa wanapenda kutulazimisha kwenda kula pale...sikuwa najua ni baada ya kusikia ukipeeka gari mnapewa 20 wewe na dereva...sasa hii ni kero kwa abiria

jamani wiki iliopita napita wakatoa nyama mbichi nikawamwagia....nkaondoka majuzin narudi na metro nakumbana na same stupid nyma mbichi wanalazimisha kugawa watu wakafie mbali....chips wameanza punguza mgao huu ni uhni mwenye hotel embu lifanyie kazi wafanyakazi wako hasa dada mmoja na mwenzio mweusi wanabaki kutucheka...mbaya katoto kamoja kameshindwa kula tukaomba hata wampe ilioiva wakaakataa kabisa...hiii na laaana kama si mwisho wa dunia kumlisha mwenzio damu...

Loh11

Heshima kwako Major mkandala.

Kwanza naomba kukataa madai yako yote kwasababu zifuatazo.

[1] Binafsi nimekula nyama mara nyingi highway kwasababu aina ya usafiri nianaotumia ninalazimika kula hapo.Dar Express,kilimanjaro,Mtei na Saibaba marcopolo zote wanapumzika kwa dk 15 highway.

[2] Ninasafiri mara tatu kila mwezi hivyo nina uzoefu mkubwa sana na njia hiyo,wakati mwingine ninapokosa usafiri wa mabus niliyoyataja ninalazimika kutumia usafiri wowote unaopatikana bila kujali standard ya bus,pengine hii imenipa uzoefu mkubwa wa kubaini huduma za mahotel ya njia.

[3] Highway iko juu sana ukijaribu kulinganisha na Liverpool ambayo kwanza ni chafu,wafanyakazi wake hawana ujuzi wa kutoa huduma nzuri wakati mwingine unaweza kudhani labda hawalipwi mshahara.Vyakula sio fresh,bei zao unaweza kudhani labda uko Zimbabwe.Mbaya zaidi hakuna huduma ya vinywaji vyote eg bia na konyagi kwaajili ya kucheua.Wanatulazimisha kunywa majuice ya ukwaju ambayo maji yaliyotengeneza mtu unakuwa huna uhakika nayo.Sana sana pale Liverpool wanachokifanya ni ujenzi wa misikiti badala ya kuboresha huduma.Jaribu kufanya utafiti kidogo mabus yote yanayopita Liverpool ni yale ya kiwango cha chini kabisa kuanzia nauli na ubora wa bus vikochini ya kiwango.
 
Kwa barabara nilizopita hii ya Dar -Arusha kwa usafiri wa Dar exp mbona is the best. Ni magari ya uhakika, huduma nzuri na hiyoo hotel yao Highway ikoo std tuu.

Sipendi kukumbuka mambo ya Korogwe Transit, Liverpool, Aljazeera, Mombo exp kwani jamani kwao afya ya binadamu si mtaji zilivyookithiri kwa uchafuu na vyakula very substandard.

Kama ni nyama mbichi hiloo linarekebishikaa tuu ili mradii usafii upo.Na pale vyakula machaguoo ni mengii tuuuuuu.
 
Dear Major, mimi pia nimepita hapo mara chache nilizosafiri njia hiyo.......kwa kweli nilipapenda. Lakini kama nyama hujaipenda, kuna buffet na pia kuna snacks pale. Sambusa nzuri zinavutia machoni, sijui sandwich, baga........mbona vyote vipo mkuu. Ukipita siku nyingine hebu jaribu buffet au snaks, im sure utakuja na maelezo mengine tofauti.
 
this guy is totally misleading the public, napata filing huyu jamaa katumwa na jamaa wa restaurant ya mombo mpya kwani inashindwa kushindana na highway sasa anadhani anaweza kutujaza ujinga, nyama ya pale is the best na vyakula vingine pia, njia nzima hakuna sehem nzuri kama pale, kama hutaki kula nyama kuna bufee pale ndani nenda kajisevie, au kama ulivyoonyesha una chuki binafsi panda mabasi mengine yanayosimama mombo uko ulikotumwa kama sumry,serengeti, skline, happy nation etc pale ni mahali kwa watu classic wa mabasi ya ukwli kama dar express, kilimanjaro, mtei na ma luxury yote ya njia ii
 
this guy is totally misleading the public, napata filing huyu jamaa katumwa na jamaa wa restaurant ya mombo mpya kwani inashindwa kushindana na highway sasa anadhani anaweza kutujaza ujinga, nyama ya pale is the best na vyakula vingine pia, njia nzima hakuna sehem nzuri kama pale, kama hutaki kula nyama kuna bufee pale ndani nenda kajisevie, au kama ulivyoonyesha una chuki binafsi panda mabasi mengine yanayosimama mombo uko ulikotumwa kama sumry,serengeti, skline, happy nation etc pale ni mahali kwa watu classic wa mabasi ya ukwli kama dar express, kilimanjaro, mtei na ma luxury yote ya njia ii

Heshima kwako Bona,

Nakubaliana na hoja zako bila shaka kuna mbinu za kuchafuana mwarabu kashindwa kabisa kutoa huduma nzuri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom