Abeid Amani Karume: Ni Shujaa wa Wazanzibari?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Je Wazanzibari wanakubaliana kuwa mzee Karume alikuwa ni shujaa wao? Anakumbukwa kwa yepi mazuri ambayo wananchi wa Zanzibar wanaweza kuona fahari kuwa aliwahi kuwa Rais wao? Yawezekana bado wapo watu ambao wanamuona kama alikuwa dikteta, muuaji na mtu ambaye ameviharibu visiwa hivyo?
 
Huyu si ndio alioingia kwenye muungano na wabara? Sasa wa-znz watamuona kama ndio shujaa?? Ngona nisubiri tanzania daima niisome story yako kwa undani.
 
Kuna mambo mengi mabaya na mazuri kutoka kwake. Inaaminika alikuwa na ukatili uliopitiliza, kitu ambacho hakikuwa kizuri. Ila huruma na kupenda kusaidia watu aliowaona sio threat kilikuwa kitu chema kwake.
Na ni mtu ambaye aliweza kuona mbali...alijua lazima na yeye angepinduliwa hivyo kuungana na Tanganyika lilikuwa jambo lisilokwepeka.
 
Nadhani alikuwa ni dikteta vinginevyo asingeuwa, na wazanzibar wengi kwa jinsi wanavyolalamika sasa hivi ni kuwa wako ktk muungano ambao aliwaingiza bila ridhaa yao.
 
Ni shujaa kwa kusimamia mapinduzi za znz, kusimamia aman na utulivu tofauti na watawala waliofuata
 
Back
Top Bottom