barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Akiongea na Azam Two...Abdul Kambaya anasema sio kweli kuwa Prof Lipumba amewafukuza Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi wa CUF.
Kambaya anasema kuwa kwa sasa Lipumba bado anasuka uongozi wake na leo alikutana na walinzi wa Chama Makao Makuu ya CUF ili kuona ni namna gani wanaimarisha ulinzi wa chama na viongozi waliorudishwa na msajili na pia kuhakikisha ulinziMakao Makuu ya Chama.
Abdul Kambaya anasema amekuja Azam Tv kukanusha habari hizo ambazo zimeanzia JAMII FORUM, huku akisema JF ni mtandao unaoongozwa na member wengi wa CHADEMA ambao nyuma ya mgogoro huu wa CUF wao wanafaidika.
Akihojiwa na Raymond Nyamwihula kama Prof Lipumba ataweza kufanya kazi na waliotofautiana naye? Kambaya anasema hilo linabaki kuwa suala la Lipumba mwenyewe, japo anakiri kuwa ni ngumu kuweza kufanya nao kazi pamoja kwani anaweza kuhitaji team mpya ya kukisuka chama kwa mikakati mipya
Kambaya anasema JF ndio inaeneza habari nyingi za CUF zisizo na ukweli na anasema kwa sasa mgogoro wa CUF umekuwa deal na biashara kwa vyombo vya habari vingi, akitolea mfano kuwa magazeti mengi ya leo yameandika kuwa "Prof Lipumba aingizwa makao makuu kwa Mtutu wa Bunduki". Kambaya anasema kuwa na si kweli kuwa Prof Lipumba anadhaminiwa na CCM.
Kuhusu kumuondoa Maalim Seif ktk nafasi yake,Kambaya anasema kwa sasa Lipumba ana mamlka ya kuwaondoa manaibu katibu mkuu wote isipokuwa Katibu Mkuu anayepatikana kwa mkutano kwa kuchaguliwa na mkutano Mkuu. Hivyo wao kama Wanachama wenye haki na walio madarakani kwa mujibu wa katiba,kesho wataenda kusikiliza walichoitiwa ktk Baraza la CUF makao Makuu ili wakajieleze na haki itendeke.
My Take:
Hii ya Abdul Kambaya kuhusisha JF na CHADEMA imekaaje? Ni kweli kuwa mpaka leo Kambaya anaamini JF ninaongozwa na member wengi wa CHADEMA?