Unamkumbuka kwa yapi Abdul-Rahman BABU?

Companero,

Mkuu ni ukweli usiopingika kuwa Abrahman babu ndiye mwalimu wa Nyerere ktk Ujamaa..
Maelezo ya babu yote yanatangulia Muungano wetu kwa maana kwamba dhumuni la Muungano halikuwa kabisa kuihusisha nchi yetu na Ujamaa kutokana na shinikizo la nchi za magharibi. hata huo uwaziri wa nchi za nje kwa Zanzibar ulidumu tu kwa muda (four month to be exact) wakati ASP wakiwatafutia dawa Umma party kuwaondoa kabisa kwa sababu chama hicho kilijulikana kama ni chama cha Kikomunist..Ukweli ni kwamba ndio waliopindua utawala wa Sultan, yatasemwa mengi kupotosha.. but that is the fact.
Pamoja na kwamba dhumuni la Muungano lilikuwa kulinda Mapinduzi yale lakini swala la Ukomunist ndilo lilikuwa kichwa cha habari.. na Nyerere alikuwa very interested na kichwa hiki - Abraham Babu..
Ndio maana baada ya Muungano ASP walifikiria wameshinda kuwaondoa Umma Party lakini Nyerere alijua kwamba anamhitaji Abraham Babu na vichwa vingine toka visiwani akawavuta bara kama serikali ya Muungano kwa maslahi ya bara..
Kwa hiyo mkuu kuna ukweli ktk maelezo ya Myahudi wetu Netanyahu..na sioni tofauti zenu isipokuwa historia yenyewe mnachanganya wakati.

Sasa unapingana na maneno ya Babu mwenyewe anayekiri kuwa Mwalimu alikuwa anawapunguza makali wakomunisti? Yani unapingana na maneno ya Mwalimu mwenyewe kuhusu hofu yake kuhusu hawa Wakomunisti? Sasa kama unapingana na Babu na Mwalimu kuhusu tofauti zao za kiitikadi na kiutendaji sijui utakubaliana na nani kuhusu mgongano wa wanafikra hawa?

kwa ufupi, Mwalimu aliwaondoa kina Babu Zanzibar makusudi ili wasimsumbue Karume na ukomunisti wao. Aliwaleta Dar, akawapa uwaziri ila akahakikisha kuwa anazima mawazo yao kama dondoo ya Al Noor Kassum niliyoiweka hapo awali inavyoonesha. Alipoona amezidiwa kimawazo Mwalimu akaamua kumfukuza kazi Babu ili Usoshalisti wa Kisayansi wa Babu usivunje Imani ya 'Ujamaa - Msingi wa Usoshalisti wa Kiafrika'.
 
Kuhani,
Mkuu Nyerere alifanya mabadilisho wa wizara zote na sio kumwondoa Babu peke yake... tatizo ni kwamba Nyerere mwenyewe alikuwa msomi hivyo haiwezekani kabisa kuwa Babu ndiye alijua kila kitu kuhusiana na Ujamaa. Nyerere anajulikana, hata Uhuru wenyewe alikuwa introduced kisha akajenga kile alichokiona yeye kuwa bora zaidi hata kama kilitofautiana na mawazo ya wale waliomtangulia.. Ni hulka ya binadamu wote, unapokuwa intoduced ktk relation yeyote na mwanamke fulani haina maana huyo aliyekupa ntro ni lazima awepo ktk maisha yenu kila siku.
Ukimsoma vizuri Abraham babu utagundua kuwa Nyerere alikuwa na mtazamo tofauti wa ujenzi wa Ujamaa lakini sio zile principal..Pengine alitaka kufanikiwa haraka tofauti na vile alivyoshauriowa..nachofahamu mimi babu alimwambia swala la vijiji vya Ujamaa ni swala la utashi wa wananchi wenyewe isipokuwa weka miundombinu vijijini kuweza kuwavuta ktk kilimo na viwanda huko. Mwalimu ama watendaji kazi wake walishindwa kuvumilia mwendo wa kunyata kuhamia, wananchi ambao kwanza uhamiaji vijiji vingine haikuwa desturi yao. Uhuru bila mipaka ulikuwa bado somo jipya!...nakumbuka hata sisi miaka ya 70 ukiondoka kwenda Ulaya tulifikiria kabisa kuwa mtu huwezi ku survive nchi ya wageni kwanza utaanzia wapi!..

Zipo sababu nyingi saana kwa mwalimu mwenyewe kubadilisha baraza zima la mawaziri na sio kweli target alikuwa Abraham babu isipokuwa mwalimu alitaka watu wanaofuata azma yake. Na hakuna rais yeyote duniani ambaye anaweza kuweka baraza la mawaziri watu ambao wanapingana ktk utekelezaji...

Companero,
Mkuu sio kweli mwalimu aliwachukua hawa ili wasimsumbue Karume isipokuwa walitaka kuwaondoa kabisa ktk serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hawa jamaa hata walipokuwa bara bado walikuwa wanted Zanzibar na hofu ya kumuua Karume imetokana na hofu hiyo hiyo ya kile walichokifanya kina Karume kuwaondoa Umma party!
Tutakuwa tunajidanganya kusema kwamba Nyerere hakuwa mkomunist...isipokuwa kuna mambo mengi ya Kikommunist aliyaacha nje (maswala ya dini) na hakuchukua lolote la Ubebari!
 
Mwawado,
Haikuwa nia yangu kuwafananisha Babu na Kambona. Nilichotaka kufanya ni ku "contrast' hasa ukizingatia kwamba Babu aliendelea kumwaga cheche hata alipokuwa makimbizini Uingereza na Marekani wakati Kambona aliishia kwenye ulabu tu.

Mkuu kuna sababu nyingi zilizomfanya Kambona akae kimya. Na wahenga wanasema kimya kikuu kina mshindo mkuu. Huyu jamaa pamoja na ukimya wake aliandika masuala mengi kwenye shajara zake. Nasikia zitachapishwa hivi karibuni ili Ulimwengu wote ujue ukweli kuhusu Nyerere na besti mani wake Kambona! By the way, have you wondered why our conventional history has demonized Kambona the very man who saved Mwalimu in the 1994coup? Yaani toka utotoni tulikuwa tunaimba nyimbo za kejeli tu kuhusu Kambona!Why? Kuna jambo hapo limejificha au limefichwa!Think twice!
 
Tutakuwa tunajidanganya kusema kwamba Nyerere hakuwa mkomunist...isipokuwa kuna mambo mengi ya Kikommunist aliyaacha nje (maswala ya dini) na hakuchukua lolote la Ubebari!

Ukomunisti ni nini? Ni mambo gani ya Kikomunisti aliyaweka ndani? Yapi hasa?
 
Companero,

Mkuu nadhani sasa unafanya utani!...
Hata hivyo nitakujibu kwa ufupi pamoja na kwamba sielewi nia yako..
Ukomunist ni itikadi inayopinga Ubepari, ni mfumo wa kiuchumi ktk jamii unaolenga kuondoa tabaka za wananchi wake kati ya matajiri na maskini ambapo maskini ndio kiini cha uzalishaji huo. Haubebi chochote toka upande wa pili (Ubepari).

Ni mambo yapi ya Kikomunist, Nyerere alioyaweka?...
1.Uchumi wa nchi kuwa mikononi mwa serikali badala ya matajiri wachache!
2. Utumiaji maguvu ktk utekelezaji wa sera... Hapa nakuomba unielewe kuwa kama kitu ni RIGHT ya mwananchi basi right hiyo ni lazima uitumie utake usitake, usipopokea unavunja sheria. Mfano ndio hayo ya kuhamia vijijini.

hayo machache unasemaje mkuu! yametosha au kuna jipya!
 
Kuhani,
Mkuu Nyerere alifanya mabadilisho wa wizara zote na sio kumwondoa Babu peke yake... tatizo ni kwamba Nyerere mwenyewe alikuwa msomi hivyo haiwezekani kabisa kuwa Babu ndiye alijua kila kitu kuhusiana na Ujamaa.

Zipo sababu nyingi saana kwa mwalimu mwenyewe kubadilisha baraza zima la mawaziri na sio kweli target alikuwa Abraham babu isipokuwa mwalimu alitaka watu wanaofuata azma yake. Na hakuna rais yeyote duniani ambaye anaweza kuweka baraza la mawaziri watu ambao wanapingana ktk utekelezaji...

Mkandara, sawa. Ahsante.

Hivi tukisema Kikwete ametangaza baraza jipya la Mawaziri, na Zakia Meghji hayumo. Si sahihi nikisema Kikwete amem fire Meghji ? Whether na Chenge nae hayumo katika baraza jipya, na Mramba na Mwapachu na Ngasongwa na kwamba hakuwa anam " target" Meghji, ukweli uko pale pale kwamba Kikwete amem fire Meghji!

Tukirudi kwenye ishu yetu, whether hakuwa anam target yeye kwenye cabinet reshuffle ya 1972 au hakum targert, the simple truth ni kwamba Nyerere alim fire Babu!

Kwa hiyo, huna budi kukubali, kama anavyosema Campanero, kwamba Babu na Nyerere walikuwa wana tofauti za Kiitikadi. Mwanzoni ulikuwa unaremba remba ndoa ya Nyerere na Babu kama soul mates fulani hivi wa kiitikadi. Ni "vichwa" vya Wazanzibar fulani aliowaleta Bara, umesema. Tena "Babu ndie alimfundisha Nyerere Ujamaa," unatuambia. Baadae, ulipoonyeshwa tofauti zake kiitikadi na Nyerere unasema Babu hakujua kila kitu kuhusu Ujamaa. Unamruka!

Babu na Nyerere walitofautiana kiitikadi ndio maana Nyerere akam fire kazi, February 1972.

Hatulazimishi Nyerere awe na baraza la Mawaziri wanaopingana nae kiitikadi. Ninachokataa hapa ni kupindisha kilichojiri, hili la wewe kubisha kwamba Nyerere hakum fire Babu. Na ni makosa pia kuchora picha ya uhusiano wa Bwana Babu na Bwana Nyerere kama vile ndoa ya kiitikadi ya Bwana na Bibi harusi ambayo iko kwenye honeymoon siku zote. Babu na Nyerere walitofautiana kiitikadi ndio maana akam fire!

Tena akam fire wakati Babu yuko Addis Ababa anawakilisha Tanzania kwenye Kikao cha Mawaziri wa O.A.U!!!!
 
Kuhani,
Hapana mkuu unachouliza hapa umeshindwa kukisherehesha vizuri.
Kikwete kubadilisha baraza la mawaziri na karamagi akiwepo haina maana Kikwete na karamagi wanapingana ktk Principal za Ubepari isipokuwa kuna jambo karamagi kalifanya nje ya kuaminiwa kwake pia kwa kuongezea tu yawezekana Karamagi hakuweza kuimudu wizara kiutekelezaji kama alivyotaka Kikwete.

Nikirudi ktk swala la Babu nachojaribu kusema hapa ni kwamba Abraham babu na Nyerere walikuwa njia moja ktk itikadi hiyo ya kujenga taifa la Kijamaa sipokuwa utekelezaji wa sera za chama ndipo Nyerere aliwaona viongozi wale hawafai...Kisha hakuna sehemu niliyodsema Nyerere hakum fire babu isipokuwa nimesema hakuwa target kama mlivyotaka kuonyesha mwanzo..kifupi naona kama kuna ujenzi wa chuki fulani kati ya Nyerere na Babu wakati sio kweli... kwa maana hii, Kikwete na Karamagi bado wanaweza kuwa na mawasiliano na wanabembea viwanjani pamoja hakuna chuki yao.

Sasa iwe makosa ni ya Nyerere ama Babu haina maana Nyerere na Babu hawakukubaliana kimsingi. Babu aliyaona makosa ya Nyerere na Nyerere aliyaona makosa ya Babu hivyo Nyerere kama rais aliweka watu ambao waliweza kutekeleza azma yake.
Na kama unakumbuka baada tu ya kuwaachisha kazi hawa jamaa na kuundwa kwa baraza jipya Tanzania tuli boom kiuchumi ile mbaya... kina Babu wote walionekana wachawi lakini uchumi huo haukuweza kudumu kwa sababu misingi aliyoijenga Nyerere haikuweza kuchukua uzito wa nyumba iliyojengwa.
Kwa hiyo inawezekana kabisa babu alimwambia Nyerere kuwa mkuu zege tunalol mwaga hapa lipe mwezi mzima limwagiwe maji liwe imara zaidi na ongeza nguzo zaidi kuweza kubeba jumba hili tunalotaka kulijenga. Nyerere akaona huyu mtu anamkawiza...Akainua kitu kikasimama watu tukahamia na sherehe zikafanywa... miaka mitano tu jengo chini!...Hii yote haina maana babu alikataa toka mwanzo ujenzi wa jengo hilo. Ukimsoma Babu bila kufikiria zaidi negative za mahusiano yao utamwelewa.
 
Thats very true sijawahi kuona hata kitabu kimoja kilichoandikwa na Kambona. Lakini Babu bwana tembelea duka lolote lile la vitabu watakwambia kama hakijaisha basi watakutolea order

Inatia kinyaa kuona nchi ambayo zamani tulikuwa tunatoa magwiji left and right tumebakiwa na ZERO!

Hebu soma hii article sijui iliandikwa lini from Time magazine

Tangibar - TIME

wewe wewe GT wewe unaogopesha sometimes...., i mean it dude!!! miye nasubiria vitabu vyako tu - am not a scholastic but if you've authored any i'll definitely order one right away be it via amazon at seeing the ISBN!!! lol

and somewhat this applies to akina Mwanakijiji (siyo riwaya zake), Masatu, Jasusi, Pundit (vilivyoandikwa kwa kiswahili), Rev. Kishoka (siyo vya mahubiri), Suki, Mkandara, FMES (siyo vya kibaharia), Bibi Ntilie, Kyoma (siyo vya kiutabibu), Nyani McCain (siyo vya hiphop), Kitila Mkumbo (siyo vya Chadema), Augustin Mosh (siyo vya mpango wa uzazi), Icadon (siyo vya upelelezi), YNIM (siyo vya utabibu) Dr. W .Slaa (siyo vya upadri), Zitto (siyo vya kikatiba), BAK (siyo vya kunakili), Mtanzania (siyo vya ki-liberal), Invisible (siyo vya mapenzi), Shy (siyo vya kiongoongo), Halisi, Phillemon Michael, MwK (siyo vya Chadema), NaimaOmar (siyo vya mapenzi), Ogah, Kichuguu, FairPlayer (siyo vya CCM), Kasheshe (siyo vya media), Fundi Mchundo (siyo vya mazingira), Kibunango (siyo vya picha za wanawake), na baadhi ya wengine wachache.

Thread hii imeenda shule na unajifunza mengi sana hapa, ahsanteni wakuu!
 
SteveD,
Duh.. mkuu changu - LIMBUKENI - hutaki kabisa kukiona!...

Mkulu, nilikuwa bado na update... umeniwahi miye limbukeni wa mtandao!! Nimeshakuweka kwenye orodha!!! ;)

Kama utaona, nimemwacha Mkulu Kuhani nje makusudi... maana najua atakapoandika chake (simaanishi ile thesis yake ya phd - maana ni bomba), kitakuwa na clauses kibao za kunifunga mimi msomaji!!....mithili ya kujisomea suicidal note yako mwenyewe..... !!!lol :)
 
Kama utaona, nimemwacha Mkulu Kuhani nje makusudi... maana najua atakapoandika chake (simaanishi ile thesis yake ya phd - maana ni bomba), kitakuwa na clauses kibao za kunifunga mimi msomaji!!....mithili ya kujisomea suicidal note yako mwenyewe..... !!!lol :)

Ujumbe kwa mtu hai anaewakilishwa na jina SteveD.

Unapoongelea "ubomba" wa thesis ya phd ambayo hujaiona, na hujui kama ipo, hiyo ni tasnifa (yaani dongo ) la kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa, hasa ukizingatia ulivyonichora kwenye kipicha cha njano cha kashfa.

Na uliposema "maana najua atakapoandika chake" bila kuongeza "kama bado hajaandika" maana hujui kama bado sijakiandika, au sijaviandika na inawezekana usije kujua, maana jina litakalotumika, au lililotumika, sio hilo unalolijua wewe, kitendo hicho ni cha kichochezi. Hilo linaweza kuchanganya wateja wasomaji wangu au wanaoweza kuja kuwa wateja wasomaji wangu, na hivyo kuharibu soko lililopo au linaloweza kuja kuwepo.

Tuma kwangu maombi ya radhi ndani ya masaa 48 kuanzia tundiko hili ambalo litakuwa tangazo rasmi la wazi (Constructive Notice ), ambalo halijalishi kama umepata ujumbe au hujapata, ili kuepuka kufikiriwa kuchukuliwa hatua kali.
 
Tuma kwangu maombi ya radhi ndani ya masaa 48 kuanzia tundiko hili ambalo litakuwa tangazo rasmi la wazi (Constructive Notice ), ambayo halijalishi kama umepata ujumbe au hujapata, ili kuepuka kufikiriwa kuchukuliwa hatua kali dhidi yako.

Acha kutishia hapa weka hoja, hakuna tangazo wala nonesense hapa weka hoja!

Mkuu Steve D, ubarikiwe kwa hoja nzito sana! Ujumbe ni kwamba hata uje vipi haogopwi mtu hapa ila ni hoja tu!
 
Kama utaona, nimemwacha Mkulu Kuhani nje makusudi... maana najua atakapoandika chake (simaanishi ile thesis yake ya phd - maana ni bomba), kitakuwa na clauses kibao za kunifunga mimi msomaji!!....mithili ya kujisomea suicidal note yako mwenyewe..... !!!lol

Mkuu Steve D, tupo ukurasa mmoja hapa.
 
Ujumbe kwa mtu hai anaewakilishwa na jina SteveD.

Unapoongelea "ubomba" wa thesis ya phd ambayo hujaiona, na hujui kama ipo, hiyo ni tasnifa (yaani dongo ) la kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa, hasa ukizingatia ulivyonichora kwenye kipicha cha njano cha kashfa.

Na uliposema "maana najua atakapoandika chake" bila kuongeza "kama bado hajaandika" maana hujui kama bado sijakiandika, au sijaviandika na inawezekana usijue maana jina litakalotumika, au lililotumika, sio hilo unalolijua wewe, kitendo hicho ni cha kichochezi. Hilo linaweza kuchanganya wateja wasomaji wangu au wanaoweza kuja kuwa wateja wasomaji wangu, na hivyo kuharibu soko lililopo au linaloweza kuja kuwepo.

Tuma kwangu maombi ya radhi ndani ya masaa 48 kuanzia tundiko hili ambalo litakuwa tangazo rasmi la wazi (Constructive Notice ), ambayo halijalishi kama umepata ujumbe au hujapata, ili kuepuka kufikiriwa kuchukuliwa hatua kali dhidi yako.

.....unaona sasa.... niliyataka mimi mwenyewe!!

sea0473l.jpg


Nisamehe Kuhani... Nisamehe kuhani mkuu!! Mimi ni mwenye dhambi!!

------------------------------------


OMBI: mnisamehe wakuu kwa kuondoka katika mjadala, let's take it as a break. Thanx.
 
Binafsi nilijua kuwa BABU alikuwa ni mzima sana na alikuwa ana command respect among the leftisthapa UK na London to be specific east end, enzi hizo Labour walikuwa wanachakaza mabenchi ya opposition, enzi za apartheid in SA na Cold war
Strange enough jamaa wa Caribbean ( wasomi) lakini wanamheshimu sana na michango yake aliyokuwa akiitoa, mind you hata KARL MARX Londion lilikuwa chimbo lake mpaka alipofariki the same applies to other prominent scholars.

Chavez alipokuja London of course the only chance ya kumuona ilikuwa kumingle na ma socialists wetu hapa ndipo Mbunge mmoja wa Labour ambaye ni leftist Jeremy Corbyn alipoanza kunipa story za Babu

Sasa why did i remeber him leo? few moments ago nilikuwa natazama BBC NEWS on BBC4 kulikuwa na story ya mwaandishi mwingine maarufu mwenye asili ya Caribbean anaitwa Dereck Walcott ambaye ni playright na poet na bila kusahau aliwahikushinda Nobel prize in Literature sometimes back

Jamaa anafanana sana na Marehemu BABU

derek-walcott-3-sized.jpg
man umenikuna! i never met with AMB ( babu ) but the guy was a socialist intellectual to the core. nakumbuka kuna wakati nikiwa ids -udsm nilikuwa namsaidia prof haroub othman kuandika kumbukumbu ya babu. thats when my respect for him grew a thousand times.

as luck would have it, in 2006 i met with dereck walcott in person, this time in trinidad during carifesta! kweli kabisa wanafanana! there was also another literary jiant - sir vid naipaul..huyu naye kiboko! mbali ya shafi adam shafi na shaaban robert tanzania tunaye nani wa ulinganisho na hawa? what happened after these two were done?

what a shame wanasiasa na wasomi wa tanzania sio waandishi. nyerere aliishia kutafsiri kazi za shakespeare ( julius kaizari ) na mabepari wa venice ( jamani hivi kweli tafsiri ya merchant = bepari? ). nothing original here!
 
man umenikuna! i never met with AMB ( babu ) but the guy was a socialist intellectual to the core. nakumbuka kuna wakati nikiwa ids -udsm nilikuwa namsaidia prof haroub othman kuandika kumbukumbu ya babu. thats when my respect for him grew a thousand times.

as luck would have it, in 2006 i met with dereck walcott in person, this time in trinidad during carifesta! kweli kabisa wanafanana! there was also another literary jiant - sir vid naipaul..huyu naye kiboko! mbali ya shafi adam shafi na shaaban robert tanzania tunaye nani wa ulinganisho na hawa? what happened after these two were done?

what a shame wanasiasa na wasomi wa tanzania sio waandishi. nyerere aliishia kutafsiri kazi za shakespeare ( julius kaizari ) na mabepari wa venice ( jamani hivi kweli tafsiri ya merchant = bepari? ). nothing original here!
Kaiyunrakuba,
Nothing original from Julius Nyerere? You may want to take that back.
 
Kaiyunrakuba,
Nothing original from Julius Nyerere? You may want to take that back.

---Jasusi, sina uhakika, lakini yaonekana wengi hapa wanaosema hamna kitu original kutoka kwa JKN wasema hivyo kunatokana na mrengo kuwa kitu kuwa original ni lazima kizae matunda positive. Bila kutupia mwangaza vitu original ambavyo - ni original lakini havikuweza kutekelezeka ipasavyo au vilikuwa havitekelezeki. Kwingi kunakoonekana hapa ni kule kuchanganya vinavyotekelezeka na ambavyo havikutekelezwa na kubamizwa kwenye rundo moja na credentials za originality. Hali halisi hapa twajua kuwa - hamna kisicho na mwanzo bila mwisho, hata katika ideology.
 
---Jasusi, sina uhakika, lakini yaonekana wengi hapa wanaosema hamna kitu original kutoka kwa JKN wasema hivyo kunatokana na mrengo kuwa kitu kuwa original ni lazima kizae matunda positive. Bila kutupia mwangaza vitu original ambavyo - ni original lakini havikuweza kutekelezeka ipasavyo au vilikuwa havitekelezeki. Kwingi kunakoonekana hapa ni kule kuchanganya vinavyotekelezeka na ambavyo havikutekelezwa na kubamizwa kwenye rundo moja na credentials za originality. Hali halisi hapa twajua kuwa - hamna kisicho na mwanzo bila mwisho, hata katika ideology.

Lakini mbona JKN ameandika vitabu vingi tu kuanzia Freedom and Unity, Freedom and Socialism, Freedom and Development...pamoja na articles nyingi tu zilizochapishwa. Can anything be more original than that? Au nyinyi vijana wa siku hizi hamkusoma hivyo vitabu?
 
Lakini mbona JKN ameandika vitabu vingi tu kuanzia Freedom and Unity, Freedom and Socialism, Freedom and Development...pamoja na articles nyingi tu zilizochapishwa. Can anything be more original than that? Au nyinyi vijana wa siku hizi hamkusoma hivyo vitabu?

Jasusi, ndipo hapo ninaposema kuwa sikubaliani na wengi wanaoonekana kuimply indirectly kwamba kitu kuwa original ni pale tu kitu hicho kitakapokuwa na tangible positive impact katika jamii. Wakiwa na reasonable argument ya failure za sera mbalimbali zilizotokana na falsafa na machapisho kama hayohayo uliyoyataja. Ilhali concurrently twakubaliana kuwa hamna kisicho na asili, basi vivo hivyo kwenye mambo ya ideology na mengine mengi tukubali kuwa kila kitu kina mwanzo/influence/inspiration na ni kawaida kuwa na traceable elements iwe kitu hicho kimezaa matunda au laa.

Kwangu mimi nakubali mengi ya JKN kuwa origin yake ni kwake yeye kwa misingi michache kwamba: moja, as long as aliweza kudigest na ku-synthesize yale yote aliyosoma na kukutana nayo maishani na kuya mold kama falsafa yake katika jamii aliyomo, basi origin ya hizo falsafa ni yeye mwenyewe. Mbili, kufanikiwa au kutofanikiwa kwa kitu kunatokana na sababu kuu mbili. Nazo ni: idea ya kitu hicho haitekelezeki (maana ni mbovu au iko beyond upeo wa kutekelezeka). Sababu nyingine ni kwamba idea hiyo inatekelezeka ila watekelezaji/wawajibikaji katika hilo wanashindwa kutokana na uzembe.

Sasa hitilafu katika mfano alioutoa Kaiyurankuba wa mabepari wa Venice na jinsi JKN alivyoutafsiri na kuonesha kukosekana kwa originality; kukubalika kwake ni pale tu ambapo atakapotaja mfano wa mwanafalsafa mwingine yeyoye yule ambaye hakupata inspiration kutoka pahala, bali anakuwa ame-conjure up a philosophy from thin air.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom