Abbas Mtemvu atalia tena?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Nina kumbukumbu na picha ya mbunge wa Temeke alivyotoka gazetini akilia baada ya wajumbe wa NCCR-Mageuzi kunyukana kule Tanga. Mtemvu alinukuliwa akisema alihuzunishwa sana na hali iliyotokea kwa chama alichokipenda sana na alichokuwa na mategemeo makubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi ya Tanzania.

Mtemvu aliendelea kulonga kuwa kama NCCR-Mageuzi itakufa, basi CCM itatawala milele. Baadaye kidogo, Abbas Mtemvu alijiunga na CCM na baadaye akapewa kijiwe cha kubangaiza kama Mkuu wa Wilaya, alianzia Kibaha, na baadaye kufanikiwa kumnunua kibaraka Tambwe Hiza mwaka 2005; akawa mbunge wa Temeke.

Hali inavyoendelea sasa, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa yatakayokipata CCM yatazidi yale yaliyokisibu chama cha NCCR-Mageuzi kule Tanga. Maswali mawili kwa Abbas Mtemvu:


1. CCM ikisambaratika kama NCCR ya wakati ule, Mh. Mtemvu atamwaga machozi tena?

2. Je ataamini kuwa chama kinachokiondoa CCM siyo NCCR-Mageuzi, kama ulivyokuwa utabiri wake wa awali, au atalazimisha CCM kitawale milele?
 
Back
Top Bottom