Aambiwa cheti chake cha degree akafungie samaki, hakuna alichosoma

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
Hii dunia kuna watu wana maneno unaweza ukakasirika mpaka ukawa mwekundu au mweusi kwa namna hasira, chuki na ghadhabu zilivyokujaa. Ninyi binadamu mnapokuwa na kazi msiwanyanyase wenzenu kiasi hiki.

Jamaa mmoja alisoma CBE alienda kuomba kazi Kampuni moja Binafsi inasemekana waliokuwa wanamhoji (interview) mmoja amesoma UK ,wawili UDSM miaka kama 8 iliyopita. Basi wakawa wanamhoji huyo jamaa ambaye kwa mujibu wa mleta habari anasema jamaa alikuwa na G.P.A ya 4.7 toka chuo cha CBE.

Waliomfanyia usaili walipoona cheti chake wakatamani sana kuweza kuongea naye wamuone huyo candidate kwa sababu walikuwa wanabishana uhusiano wa Lugha, GPA na akili au uelewa. Jamaa kweli akawa ameingia kwenye chumba akiwa mtanashati kabisa. Utata ukaanzia kwenye lugha kwanza, jamaa hajui kiingereza.

Wakaona suala lisiwe lugha basi watumie kiswahili. Jamaa nako akawa hajui kutofautisha matumizi ya r na l, ha na a, tha na za, za na dha na maneno mengine mengi akiyakosea. Kuja kwenye content ndo ikawa tatizo zaidi. Kuja kwenye mambo ya kawaida nayo hajui anajiuma uma na kutetemeka.

Jamaa mmoja akawambia "Wewe ni mtu wa 8 toka hicho chuo chenu, ni hovyo kabisa hivyo vyeti mnavyopata hapo chuoni ni bora mfungie tu samaki au maandazi". Jamaa mwomba kazi alijisikia vibaya sana na kusema ataenda kushtaki kwamba amedhalilishwa. Mhusika akamwambia awahi afanye haraka akashtaki maana naye atapata nafasi ya ku prove kuwa jamaa ni kilaza. Yule jamaa mpaka leo hajaenda kushtaki anabaki tu kulalamika kuwa chuo chake kimetukanwa.

Nikakumbuka mwaka flan pale mliman kuna mtu alivaa kituko akaambiwa aende huko CBE ndo kunamfaa. Akabisha kuwa yeye yupo huru, semister ile mwishoni jamaa aliliwa kichwa akadisco. Akaenda kuanza kitivo kingine na huko akawa analeta utozi na u much know na perfomance mbaya darasan, wakamshauri aende CBE maana kule kuna watu wa aina yake. Akakomaa wakamla kichwa tena, kweli akaamua kwenda CBE.

Akawa anatuma msg anasema kule maisha yako poa hamna stress kabisa ya kusoma na yeye ndo alikuwa anawaburuza sana darasani.

Kumekuwa na maneno maneno mengi kuwa kuna baadhi ya vyuo vipo mchekea sana kielimu na vinazalisha matango pori, yaani watu wasiofaa kuajiriwa kwa maana ya kuwa ni SL yaani slow learners hasa.

Mimi sijui lakini tusiwanyanyase kiasi hiki jaman.
 
Mlimani ndio chuo ila hata huku kwengine kama CBE kuna wahitimu wachache wazuri ila wengi wananunua vyeti kisanii ndio maana interview inabana kila kona
 
ila hawa ndugu zetu wa CBE watakuwa wanamatatizo kweli maana kila sehemu wanapigiwa kelele wao....!!!!

Na nyinyi ndugu zetu wa UDSM punguzeni majungu japo kidogo......!!!!
 
Kuna vilaza wengi tu wamesoma hapo UDSM... Msijisifie sana...
 
Hizo ni story tu, mbona mapungufu ya wengine wa UK na 2 wa udsm hawajayatoa katika interview siyo kweli kama wote walipata kazi
 
Kazi kweli kweli,nilitaka kwenda kusoma pale CBE ila kuna jamaa zangu wawili waliniambia niachane napo chuo gani hakijui kukataa watu hata kama hawana vigezo,nilicheka nikasema poa siendi tena,na sina mpango napo tena.
 
siku izi atuangalii chuo ulichosomea ,tunaangalia uelewa wako yani udsm,saut,tumaini,cbe etc kuna matango uchwara,
 
Back
Top Bottom