Aagiza azikwe na albamu la picha zake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
KIJANA Frank Raphael [18] amewaacha wazazi wake wakiwa na masikitiko makubwa baada ya kuamua kujinyonga kutokana kuwahurumia wazazi wake kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili na kuamua kujinyonga na kuacha ujumbe azikwe pamoja na picha zake alizopiga zilizopo kwenye album yake.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea huko katika Kata ya Isanga Mbeya mjini jana

Raphael alijinyonga kwa kutumia kamba aina ya katani kwa kile kilichodaiwa kuchoshwa na ugumu wa maisha unaowakabili wazazi wake kwa kumsomesha kwa shida ya hali ya juu na kuamua kufanya hivyo ili awaondolee mzigo wazazi wake hao

Kijana huyo mwaka jana alimaliza kidato cha nne na matokeo yake yalionyesha kuwa hakufanya vizuri na kipindi hiki alikuwa katika maandalizi ya kurudia mtihani huo

Hivyo kutokana na ugumu huo wa maisha unaowakabili wazazi wake ameamua kuwaondolea mzigo wazazi wake na kuacha ujumbe kwenye mfuko wake wa suruali aliyokuwa amevaa

"Naomba wazazi wangu wasituhumiwe kwa lolote.nimeamua kujinyonga mimi mwenyewe, naomba mnizike na picha zangu na madaftari niliyokuwa nikiyatumia shuleni" ulisema ujumbe huo wa kusikitisha

Frank ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia yao, ameacha majonzi makubwa kwa wazazi wake kwa kitendo kilichofanywa na mtoto wao huyo kwani walisema wangekabiliana na ugumu wa maisha hadi mtoto wao aweze kumaliza shule.
 
Mungu wangu, dah! huyo dogo what he went through kabla hajafariki na hatimae kufariki sijui niseme nini.... Maskini wazazi wake.. nashindwa kabisa kuelewa, kuchukua uamuzi huo?? I hope wazazi walikua hawalalami saana kwake kumplekea kufanya hivyo...

Mungu tunusuru na Ilaze roho ya Marehemu mahala pema...
 
Mungu karibu jamiiforum usome post hizi kisha usamehe yoote yaliyostahili hukumu kwa kijana huyu......mmmh watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

mix with yours
 
ari mpya na kasi zaidi matokeo yake ndio haya hakuna cha ari mpya watu wanajiua maisha magumu
 
Namshauri Mh.Sugu aanzishe mfuko wa kusomesha watoto wasio na uwezo wa kulipa ada katika jimbo lake kama alivyofanya Mh.wa Arusha mjini...
 
Mungu karibu jamiiforum usome post hizi kisha usamehe yoote yaliyostahili hukumu kwa kijana huyu......mmmh watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

mix with yours

Genuinely nimeshindwa la kujibu... assist me tafadhali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom