Aaah Jk,! Teh teh teh

Julius Kaisari

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,176
675
Jamani huyu jamaa mkwere mi namshangaa..ni tabia ya mjinga kujichekesha chekesha wakati nchi inaomboleza na dhiki...huyu jamaa ni king'ang'anizi,ile mwaka 95 mwl alijua alikuwa hafai,akatumia kigezo cha ukomavu kisiasa,kumbe alimaanisha ni bogus..sasa watz hatukusoma maneno yale,au pengine ni kwa sababu tumekuwa tukichaguliwa na ccm......Sikupendi kikwete..hukustahili kuiongoza tz..rais gani asiye na mamlaka?asiyechukua hatua?kacheze ngoma na vimwana..ndicho uwezacho!
 
Nyerere alifanya makosa kutumia mafumbo wakati alipo mkataa 1995, heri angetuambia huyu jamaa ni kilaza hawezi kuongoza taifa sasa angalia tunavyoteseka. Huyu jamaa hata ukimpa shule ya chekechea sijui kama ataweza kuongo, lazima tubadilishe katiba ili tuweze kumfunga ndipo wengine watajifunza kutoka kwake.
 
Ukipenda usipende Mkwere amechakachua na anaendelea na kazi yake ya kutembeza kopo huko ulaya kama kawaida:) nasikia anaogonjwa wa kuchecheka ndio maana UVCCM wanafikiria kumpeleka Muhimbili sio mimi ni habari za Kiitelejensia:kev:
 
WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA UCHUNGUZI TANZANIA
TUTENDEENI HAKI KWA DOWANS HARAKA SANA!!!

Watanzania, inaelekea GUDUDU wa ajabu tena wa kutisha mno mpaka ikaifanya CCM, pamoja na hasira zetu hizi zote, ituone wa afadhali kidogo wa kukandamiza zaidi kuliko kusema kutokulipa GUDUDU Dowans.

Waandishi wetu wa habari za uchunguzi za uchunguzi wakatueleze kiundani zaidi kwamba ni kitu gani GUDUDU iliomo ndani ya huyu mdeni hewa Dowans inayomtisha saaana Dr Kikwete na bench zima ya CC ya CCM kiasi cha kuona ya kwamb wakiue Chama Cha Mapinduzi na au wananchi wa Tanzania wengi zaidi kusafirishwa kwenda kwenye umasikini wa kufa mtu kuliko kutokulipa Dowans??

Ndugu Said Kubenea, Ayub Rioba, Mbaraka Islam, Maggid Mjengwa na 'This Day' team, nyote hapo hamna haki ya kukalia na kutunyima haki yetu ya kujua GUDUDU kitu kinachotisha ajabu kiasi hicho ndani ya Dowans kwa CCM na serikali yake, kiasi kwamba hata kama ingelikua halali kulipwa, ni sharti malipo yake iwahishwe haraka hata kabla ya wadeni wetu wa zamani kama Wazee watumishi wa Afrika Mashariki.
 
Jamani huyu jamaa mkwere mi namshangaa..ni tabia ya mjinga kujichekesha chekesha wakati nchi inaomboleza na dhiki...huyu jamaa ni king'ang'anizi,ile mwaka 95 mwl alijua alikuwa hafai,akatumia kigezo cha ukomavu kisiasa,kumbe alimaanisha ni bogus..sasa watz hatukusoma maneno yale,au pengine ni kwa sababu tumekuwa tukichaguliwa na ccm......Sikupendi kikwete..hukustahili kuiongoza tz..rais gani asiye na mamlaka?asiyechukua hatua?kacheze ngoma na vimwana..ndicho uwezacho!

Mmhh, umetumia maneno makali. Siyo vizuri ndg yangu. Lakini naunga mkono hoja yako kwa asilimia 1,000.
 
Hivi huwa hasomi alama za nyakati huyu jamaa, kila sehemu watu wanamsema vibaya kwa jinsi nchi ilivyopoteza uelekeo!
 
Sijaona ukali wa maneno yake. Au naye ulitaka azungumze akichekacheka kama Kikwete? Nachojua hajazungumza chochote kuhusu Mzee Kikwete, kazungumza kuhusu Rais Kikwete. Unataka azungumze kauli laini kwa wanasiasa wetu na kwa mambo nyeti ya kitaifa? Je, ungekuwa umedhurika na kipigo cha Arusha ungeongea kirahisi hivi?

BTW, huu "ulaini laini" tunaouendekeza Watanzania ndiyo unaotuponza, mambo ya msingi hatuko serious, tunachoweza ni kimoja tu: Kushinikiza Marcio Maximo aondoke.
 
Anazijua vizuri alama za nyakati sema anataka kujifanya na yeye kama Laurent Gbagbo wa Ivory Coast
 
Sijaona ukali wa maneno yake. Au naye ulitaka azungumze akichekacheka kama Kikwete? Nachojua hajazungumza chochote kuhusu Mzee Kikwete, kazungumza kuhusu Rais Kikwete. Unataka azungumze kauli laini kwa wanasiasa wetu na kwa mambo nyeti ya kitaifa? Je, ungekuwa umedhurika na kipigo cha Arusha ungeongea kirahisi hivi?

BTW, huu "ulaini laini" tunaouendekeza Watanzania ndiyo unaotuponza, mambo ya msingi hatuko serious, tunachoweza ni kimoja tu: Kushinikiza Marcio Maximo aondoke.

Naona siku hizi hata kuongeza hadharani simuoni zaidi ya siku ile anafungua bunge na hotuba ya mwaka mpya tokea siku amkeuwa ni mtu kama vile wa kujifichaficha utamsikia tu kwenye ufunguzi sijui wa kampuni ya mbolea na kufungua shule ya msingi huko kwao msoga zilizojengwa na wachina kama kumlipa vile fadhila
 
Rais wa nchi anafungua shule ya msingi..........bogus kabisa
 
Mmhh, umetumia maneno makali. Siyo vizuri ndg yangu. Lakini naunga mkono hoja yako kwa asilimia 1,000.

unajua mkuu,haiingii akilini,ni kichefuchefu.Hebu kumbuka,tangu aingie madarakan,ni uamuzi gani wa ki-amiri jeshi mkuu,kama ishara ya ukamanda,ambao kikwete kama rais amewahi kufanya?wevi wa mabilion unathubut kuropoka eti warudishe fedha zetu...basi..una-negotiate..then utegemee mahakama ifanye nini? Je unatoa ishara gani kwa wevi wengine?hatuna rais mzalendo..
 
hahaha!baba mwenye nyumba anatetereka wanaJF...jmoc c alikua mondul jeshini hko!yaan mtaani huko hata usiowategemea wanamponda huyu mtu na kufanya watu tustuke y mwalimu alimkataa ile 95 afu mbaya zaid HESHIMA YAKE INASHUKA hadi kwa vijana wadogo!
 
Naona siku hizi hata kuongeza hadharani simuoni zaidi ya siku ile anafungua bunge na hotuba ya mwaka mpya tokea siku amkeuwa ni mtu kama vile wa kujifichaficha utamsikia tu kwenye ufunguzi sijui wa kampuni ya mbolea na kufungua shule ya msingi huko kwao msoga zilizojengwa na wachina kama kumlipa vile fadhila

Unajua mkuu, wafanyabiashara na matapel wote wakubwa,kina Ra,el,&co wanachofanya sasa hivi ni tafiti za wapi kuna miradi ya mabilioni,then wanatia miguu yao. Ndio,wanajua hakuna mamlaka iliyo kinyume nao. Hata huo UWT wapo kama hawapo,au nao ni wevi kama Ra.. Nakubaliana na wanaJf kuwa hatuna Uwt! Nima-informer! Usalama gani wanautetea? Usalama wa matapeli? Siyo maisha na rasilimali za taifa? Dawa i jikoni..Wabunge wetu wapambanaji pelekeni moto bungeni ili tupate sababu zaidi,tunahitaji maandamano makubwa nchi nzima..
 
Naona siku hizi hata kuongeza hadharani simuoni zaidi ya siku ile anafungua bunge na hotuba ya mwaka mpya tokea siku amkeuwa ni mtu kama vile wa kujifichaficha utamsikia tu kwenye ufunguzi sijui wa kampuni ya mbolea na kufungua shule ya msingi huko kwao msoga zilizojengwa na wachina kama kumlipa vile fadhila

Ana ujasiri gani wa kuongea hadharani kwa sasa? Hofu yake ni kuwa watu wanategemea aongee mambo makubwa yanayoikabili nchi naye kwa sasa hana cha kujibu. Atakuja kuibuka na kuikaribisha timu ya mpira ikulu kwa ajili ya pongezi. Ni kweli kuwa kila binadamu au Rais ana mapungufu yake lakini kwa huyu jamaa du, imekuwa too much.
 
Naona siku hizi hata kuongeza hadharani simuoni zaidi ya siku ile anafungua bunge na hotuba ya mwaka mpya tokea siku amkeuwa ni mtu kama vile wa kujifichaficha utamsikia tu kwenye ufunguzi sijui wa kampuni ya mbolea na kufungua shule ya msingi huko kwao msoga zilizojengwa na wachina kama kumlipa vile fadhila

Raisi wa misiba na sherehe zisizo na tija huyo.

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Jamani huyu jamaa mkwere mi namshangaa..ni tabia ya mjinga kujichekesha chekesha wakati nchi inaomboleza na dhiki...huyu jamaa ni king'ang'anizi,ile mwaka 95 mwl alijua alikuwa hafai,akatumia kigezo cha ukomavu kisiasa,kumbe alimaanisha ni bogus..sasa watz hatukusoma maneno yale,au pengine ni kwa sababu tumekuwa tukichaguliwa na ccm......Sikupendi kikwete..hukustahili kuiongoza tz..rais gani asiye na mamlaka?asiyechukua hatua?kacheze ngoma na vimwana..ndicho uwezacho!

Alikuwepo Mwinyi mkasema Serikali inaendeshwa na mke wake, Mkapa mkamsema kazi kununanuna mara dictator mbambe kwahiyo wenye akili timamu hawawezi kushangaa huyu kusemwa na sio JK tu hata hao watakaokuja watasemwa hiyo ndio hulka ya raia especial wa kibongo.
 
the sky,the limit..hiyo ndo tafsiri yako..haya mautumbo anayofanya ya kunywa wine na matapel,warushaji,mafisadi kunegotiate urudishaji mali walizoiba,ndiko kunatufanya wenyeuchungu na tz kutokubaliana na msanii huyu. Mbona mwl alikuwa mcheshi?but in serious n delicate national issues,thubutu! Alikuwa anatema cheche...panua ukilaza wako..huwezi kuwa unajadili vikaon kumlipa tapeli huku uchumi unadolola,umeme shida tupu,huduma za jamii ni hisan,si haki tena,otherwise unataka kujilipa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom