Janjaweed
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 13,157
- 10,655
Wale wakubwa wenzangu mtanielewa vizuri! wakati wetu wasichana warembo walikuwa kwa hesabu. Nilipokuwa shule ya msingi miaka ya '70 nilisoma darasa moja na msichana ambaye kwangu alikuwa a woman of Dream.
Alikuwa msichana mrembo kwa viwango vya wakati ule ambapo maumbile ndio kigezo kikubwa. Aliumbika msichana na tuliomzunguka tulikubaliana kwa hilo. Nilimpenda kweli msichana huyo lakini sikuwa na nafasi ya kuonekana kwake kwa vile alipendwa na hata waliokuwa nje ya shule. Kusema kweli niliungulika sana na mapenzi kwake. Nasisitiza kuwa nilimpenda na nilikuwa na haja naye kiasi kuwa hata ndoto zangu, mipango yangu ya baadae na furaha yangu niliihusisha na yeye. Bahati mbaya sikuweza kumtamkia na nilipomuonyesha dalili alizidharau kwani hali duni was written all over me. Kuanzia kivazi na hata matumizi kwangu ilikuwa tabu. Hata hivyo nilikuwa na sababu moja kubwa ya kuonekana pale shule nayo ni kuwa nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi bora shuleni jambo ambalo lilisaidia kuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya wasichana. Hata hivyo nilikuwa na sifa nyengine nayo ni DOMO ZEGE hivyo sikuwa na uwezo wa kutengeneza uhusiano na msichana yeyote pale shuleni.
Tuliingia Sekondari nikiendelea na ndoto na njozi juu ya huyu msichana lakini hapa hali ya kutonitambua ilizidi kwani tulienda sehemu iliyohitaji hali nzuri zaidi ya maisha. Bahati nzuri nilifanikiwa kuendelea na masomo ya juu na my dream girl hakufanikiwa na wenye uwezo wakatangaza ndowa wakaondoka nae.
Tuliendelea na maisha yetu na Mungu akinijaalia kazi nzuri nami nikafunga ndowa. Ni miaka karibu 25 sasa na kwa nyakati tofauti nikikutana na yule msichana ambae amekuwa mama wa familia. Kwa kuthamini cheo cha ndowa tukikutana humsalimia kwa heshima lakini bado sijasahau niliyvompenda hapo nyuma.
Kipindi cha miezi 6 nyuma nimekutana nae na amenijuulisha kuwa ameachika kwenye ndowa yake na kuanzia hapo ameanza kunionyesha hamu ya kuwa na mimi. Ama kwa upande wangu bado namuona ananivutia na ninashawishika kutibu yale majeraha ya zamani lakini nikiifikiria ndowa yangu nabaki njia panda.
Kaka umeshaoa, na mashahidi wako wapo.... jitahidi asikuvunjie ndoa!!
Kumbuka kwamba si wewe tu unayekutwa ma masahibu hayo, yawezekana hata mkeo ana "a man of her dreams" lakini kwa kukuheshimu wewe, anamwomba nguvu Mungu amsaidie amshinde na kubaki na wewe
fikiria kabla ya kutenda, takwimu zisizo rasmi zinasema zaidi ya 80% ya wanandoa hawaoi au kuolewa na wale watu wa dreams zao
ni rare!!
Jiulize kwanini ameachika?