Sadly, we need to go to Kenya to learn this.
mimi nakujua sumbawanga kuliko wewe
uwanja wa ndege upo na unatosha,
kinachotakiwa ni barabara au reli..
Watanzania wangapi wanapanda ndege????
Mchungaji Kishoka,
Mbona unakuwa na roho ya korosho ndugu yangu? yaani uwanja wa Sumbawanga ukiimarishwa japo kwa ka-lami tu ndio inakuwa nongwa sasa unataka kila kitu kizuri kijengwe Arusha na Dom na Dar pekee?
Huo ulinganifu wa maendeleo utapatikana lini katika nchi hii? wana-Rukwa ni wachapakazi sana na wamekuwa wakiilisha Tanganyika miaka nenda rudi lakini hata barabara nzuri ya lami tu imekosekana. Saa zingine tuwe tunatoa hoja bila ya upendeleo na kuzingatia pia kuwa nchi yetu ni kubwa na kuna wananchi wengine ambao nao wanahitaji maendeleo.
Mwisho huyo Mheshimiwa Mizengo Pinda hatoki Sumbawanga ni mtu aliyezaliwa na kuishi/kusomea wilaya ya Mpanda.
Amani.
Kishoka mi nakupinga Sumbawanga kunahitaji airport nzuri yaani hizo hela ni sawa kwa kuangalia potentials za huko huo uwanja utatumika kwa faida zaidi kuliko huo wa Bagamoyo! Sumbawanga kuna ardhi nzuri ya kuruhusu kilimo cha maua na mbogamboga kama Arusha, Mbeya na Kilimanjaro! Pia tukumbuke kuna madini Sumbawanga na kuna mbuga za wanyama! nathani wanahitaji airport!
Geza hatupingi kwamba S'wanga hakuna potential ipo, ila kila kitu kinatakiwa kwenda ngazi kwa ngazi, na haina maana ya kuwa mahali pakiwa na airport ndio symbol ya maendeleo au kukua kwa uchumi.Kishoka mi nakupinga Sumbawanga kunahitaji airport nzuri yaani hizo hela ni sawa kwa kuangalia potentials za huko huo uwanja utatumika kwa faida zaidi kuliko huo wa Bagamoyo! Sumbawanga kuna ardhi nzuri ya kuruhusu kilimo cha maua na mbogamboga kama Arusha, Mbeya na Kilimanjaro! Pia tukumbuke kuna madini Sumbawanga na kuna mbuga za wanyama! nathani wanahitaji airport!
Is this a joke or prank news? We have Rubada folks matching all the way to South Korea to borrow 50 million Shillings to grow food and we are ready to sign of 43 billion to pave a tarmac for flying magic carpets of Rukwa? Kisa eti Waziri Mkuu awe na hadhi ya kushusha Gulf Stream?
Why not allocate that money to rebuild our Railway System or clean the JKNIA or KIA which are disgusting?
Yaani ukisikia Amani na Utulivu uliojaa upumbavu ni huu. Serikali ina deni kubwa kiasi haiwezi kulipa mishahara au kutoa huduma za jamii, lakini tunajenga Uwanja Rukwa?
Why not spend that money to buy 3 thermal generators that can produce a minimum total of 150mw?
When will people get angry and riot?
Geza hatupingi kwamba S'wanga hakuna potential ipo, ila kila kitu kinatakiwa kwenda ngazi kwa ngazi, na haina maana ya kuwa mahali pakiwa na airport ndio symbol ya maendeleo au kukua kwa uchumi.
Uwekezaji unaotakiwa kwa sasa katika nchi yetu hususana S'wanga na mikoa kama hiyo ni usafiri wa uhakika kwa watu wengi na vitu vya biashara navyo ni Reli na Barabara, umeme wa uhakika, elimu ndipo vitu vingine vitakuja automatically bila kelele au mikwaruzo, mfano leo hii ukitaka kujengaS'wanga utajiuliza cement utaipitishaje ili ujenge maghala, shule, nyumba bora za kuishi, hoteli nk nk, sasa huyo mwekezaji atakaye kuja kwa ndege ataka wapi atakula wapi? maana mimi s'wanga naijuia chakula au mghawa wenye hadhi ni mpaka kwa yule muhindi tu, upendo wapo wapo? au labda uende kwa masista/kwa mapadre.
nafikiri ndugu yangu utakuwa umenielewa.
kwa mimi mswahili ni rahisi saana kula kutokana na hali ninayo kuta lakini kwa mwekezaji mwingine atauliza hoteli ya kufikia ipoje? nyumba za kupanga zipoje, mazingira ya maisha ya poje, shule za watoto zipoje, ulinzi na usalama ipoje, Huduma za Afya na Umeme nk nk.
na kuongezea tu hapa Kibunguno kauliza Kilomita moja ya lami ni Shs ngapi? kwani kinacho takiwa kwa Sasa hapo S'wanga ni run way ambayo itaruhusu utuaji wa ndege bila matatizo na kuanzia ni hizi ndege zetu za abiria 50 kwenda chini, ambayo kwa kigezo changu zinaweza zisifike 43bn. kutengeneza hiyo run way kama tunataka Jengo kwa Ajili ya Waheshimiwa letu linaweza kujengwa kwa namna ya kwamba mambo yakiwa mazuri Jengo linaongezwa, lakini kwa sasa tunaweza Jengo la nafuu in Phases.
na viwanja vye kuhitaji run way za uhakika ni Kagera ambacho kwa sasa kina ndege nyingi au frequency kubwa ya kutua ndege kuliko S'wanga, lakini kweli hatuwezi kuiacha S'wanga, Mpanda, Tabora, Singida, Lindi Iringa , Songwe, Njombe, Ruvuma, wote tuna haki ni kupangilia tu ndipo kuna Gomba. haki nk nk
Ninavyo sema uwanja kuwekea lami atleast kwa ajili ya ndege ndogo, ni ili uwanja uwe reliable kutua ndege hata wakati wamasika na kuna hitaji hilo la ndege kusafiri.August,
Kwanza, je umeshapata jibu la kilometa moja ya lami ni kiasi gani?. Na hata kama una-suggest kuwa ka-uwanja kawekwe ka-lami kidogo mbona bado unajifunga kwa pointi yako kuwa huyo mwekezaji atakula na kulala wapi!. Mbona chakula kinachozalishwa na Mkoa wa Rukwa kwa msimu mmoja tu ni zaidi ya mara tatu ya hizo bln. 43!!!
Pili, kumbuka potential ya ka hako-ka uwanja sio tu Sumbawanga pekee ni kwa mkoa mzima wa Rukwa, unazungumzia wageni watalala wapi kwani watalii wanaokwenda mbuga za wanyama za KATAVI huwa wanalala wapi? pia usisahau mkoa una vivutio vingine vya kitalii ambavyo tumeshindwa kuviendeleza kutokana na miundo mbinu mibovu mfano mzuri ni KALAMBO FALLS (The second highest water falls in Africa). Potential nyinginezo ni za wafanyabiashara wa CONGO mashariki na ZAMBIA ambao wanakwenda kule kununua chakula kila kukicha.
Ndugu yangu Uwanja wa ndege una umuhimu wake na barabara, reli pia vina umuhimu na changamoto zake na sio vizuri kusema kwamba ni lazima kwanza barabara ijengwe ama reli ijengwe halafu uwanja wa ndege ufuate au vice versa!
Tunakumbuka kuwa wakati Mwalimu JKN anapewa taarifa ya kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika alikuwa ziarani Sumbawanga (Ufipa enzi hizo) ilibidi akimbizwe Zambia ili akachukue ndege ya kumuwahisha Dar kwa ajili ya shughuli hiyo sasa ebu niambie hata kama barabara ingekuwa na mkeka wa aina gani angewahi kufika kwa ajili ya maandalizi?.
Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa miaka ya mwishoni mwa themanini ATC walikuwa wanapeleka ndege zao Sumbawanga mara mbili kwa wiki na zilikuwa zinajaa abiria (asilimia kubwa ilikuwa ni WAFANYABIASHARA na sio WANASIASA) na hivyo kukuza biashara, wafanyabiashara walifikia hata kupeleka SANGARA wabichi kutoka Mwanza wa-kadhalika (utility).
Nimeona kuwa Mchungaji Kishoka anapendekeza pesa hiyo ingepelekwa Kigoma kuimarisha Reli na wewe nawe unapendekeza ingepelekwa Kagera kuimarisha Uwanja wa ndege! kwangu mimi naona mawazo yenu hayana tofauti na Mkuu wa Mkoa fulani aliyechukuwa/hamisha mapipa ya lami yaliyokusudiwa kujengea barabara za mji wa Sumbawanga enzi hizoo na kuyapeleka kwao!!
All in all, pesa hiyo bado ni ndogo sana na hata huo uwanja bado utakuwa hautoshi ningeomba wa-Tanganyika wenzangu tuachane na udogo-udogo; tuanze kuwa na fikra na mawazo makubwa zaidi kama ni viwanja basi tujenge vikubwa na kama ni barabara zijengwe pana zaidi, kama ni hospitali tujenge kubwa, kama ni masoko tujenge makubwa zaidi wa-kadhalika.
BTW:
Nimepata taarifa kuwa barabara ya kuunganisha Sumbawanga na Mbeya inajengwa kwa kiwango cha lami kupitia MCC.
Amani.
Ninavyo sema uwanja kuwekea lami atleast kwa ajili ya ndege ndogo, ni ili uwanja uwe reliable kutua ndege hata wakati wamasika na kuna hitaji hilo la ndege kusafiri.
Sasa ukija mambo ya kiuchumi na kibiashara, mahali pengi duniani hujijenga penye kutokana na economic activities, kama biashara inalipa hapo S'wanga leo hii ungekuta kuna Hoteli nyingi tu zimeisha jengwa, na ukiwa Tomaso wa suala hili angalia Mza kwa nini imejengeka? ni kutokana na kuweko kwa shughuli za kiuchumi ndio maana unaona leo hii PPf, NSSF na wengineo wanajenga Office Blocks, Nyumba za Kupangisha nk.
Na kama uwanja wa ndege ungekuwa unalipa ungeweza kukuta kampuni/mtu anaweza kuwaambia serikali kufanya mradi wa kujenga kiwanja toza kodi yako rudisha hela yako then baada ya kujilipa unarudi serikali au kwa mamlaka zinazo husika (Built own transfer).
Na kuongezea hata haya mashirika yetu ya ndege yangeweza kusema tujange uwanja ule maana ndipo tunapopatia faida yetu, lakini hilo hatulioni.
Jingine ambalo lilikuwa likiwezesha ndege kujaa wakati huo linaweza kuwa lilitokana na mashirika ya umma na wafanya kazi wa serikali kujaa huko kikazi, maana Barabara sio nzuri (NMC, NBC, RTC, CRDB, NIC na pia ilikuwa sera ya nchi chini ya CCM kwamba ile mikoa ambazo barabara sio nzuri basi serikali kupitia shirika lake ATC wafanye hivyo angalau fligt mbili kwa wiki nk nk )
Jingine unalotakiwa kulielewa na kuwa Potential za kiuchumi zinatakiwa kuwa Stimulated, sasa ukiangalia kwa sasa kinachotakiwa kwa sasa ni Barabara, pili Reli, na tatu Umeme, kumubuka Hata Muumba alianza na Siku ya kwanza ya pili na hata alipofika ya kupumzika na kuangalia nyuma aliridhika na kazi yake. na ukumbuke Muumba alimuumba Binadamu kwa mfano wake. Basi nasi tunatakiwa tufuate utaratibu huo huo,
nafikiri umenielewa ndugu yangu na mimi napenda saaana tu niomne S'wanga inayo ngara, lakini sioni kwamba inaweza kungara kwa kuwekewa uwanja wa ndege kwanza, bali barabara, na reli, na umeme wa hukika utakao wafikia wengi.
Sasa sijui wewe kwa fikra zako unaona tuanze na Uwanja wa Ndege au barabara, na nilipoweka mfano wa Kagera sio kwamba na wadharau watu wa S'wanga lakini nataka kukuonyesha kama tunapanga mipango yetu kutokana na activities basi Kagera umeonysha unazo hizo activities za ndege kuliko S'wanga, lakini kama tuna panga kutokana na kisiasa au utashi wa kibinafsi basi na huo uwanja waanzie S'wanga.