A VISITING HUSBAND: Mungu angenipa wa hivi nisingezeeka kamwe

@arusha,baba mngoni,mama mchagga

Nawasalim wana JF

Nina wivu sana wa mapenzi na nampenda sana laazizi wangu na siko tayari kutengana naye labda asiwepo duniani.Kuishi pamoja bila ugomvi as mme na mke ndiyo matakwa yangu ila kila aliye kwenye ndoa ananitisha kwamba ndoa ndoano.

Sasa ili kuepusha misuguano nataka nimweleze haya:
1.awe anakuja napoishi at my home place mara nne na kulala mara tatu hivi kwa wiki
2.Niwe na uhuru wa kwenda (mimi na watoto wetu) na kulala kwake as long as I want
3.Mwezi wa sita na wa kumi na mbili ahamie/nihamie tuwe pamoja mwezi mzima

My take:Hakika naamini akikubaliana na mimi kwa haya matatu haitatokea kununiana hata siku mmoja as long as every second we will be missing each other
Mtaani/kazini /kanisani wote wawe wanajua mimi ni mke wa flani na yeye ajulikane kuwa ni mme wa marytina



Ndugu yangu pole sana,

ninajua kuwa unampenda sana sana. na mara nyingi umekuwa ukimzungumza sana hapa. ulisha lalamika juu ya binti yule wa kimasai alivyokuwa ana mnyemelea, baadae ukasema Mungu gani anataka wewe uibiwe mtu wako, ukataka ushauri wa namna ya kumdhuru huyo binti. lakini ulizidi kukosa matumaini ukafikia kusema kipato chako hadharani na ulipenda upate mwanaume ambaye utammiliki wewe tu, yaani akae na wewe umlee kwa kipato chako.

leo unataka "visiting husband". kwa lugha halisi either unamwambia yeye akufanye uwe nyumba ndogo, au yeye awe na nyumba ndogo. hiyo itakuwa ni hatari sana! sana. hakuna kitu mbaya kama visiting husband.

usiishi maisha ya kufikirika. ishi maisha halisi. mkiishi pamoja tofauti ni lazima zitokee, aidha mkiwa mbali tofauti hazitokei sana , lakini kamwe hamwezi kuwa kitu kimoja. unatakiwa kupambana na hizo tofauti. wote unawaona mtaabni wanafuraha nao huwa wanatofautiana, hii ni kwa wanawake na wanaume pia. ukienda kwenye magenge ya wanaume utasikia wanasema " mwanamke wangu msumbufu , matatizo", ukienda kwa wanawake nao ndo yale ya " ndoa ndoano". sasa tunachoona hapa ni matatizo ambayo wanadamu wote wanayo , hatuwezi kukwepa- ni Adamu na Hawa walituambukiza haya, yatakwisha tukirudi kule nchi ya ahadi
 
Duuh hii ngumu hyseee yani akuoe then muishi mbali mbali?! Mmmh hii ngumu labda kama ndoa ya wake wawili yani utakua unamkosa ule muda atakapokua kwa mwenzio.
 
Kwenye ile uliyojifanya pedeshjee kwamba fweza za kumwaga zipo nilikushauri hukunisikia, hapa unasema huwa unaweka hisia zako za kweli!!!!!, kama ni kweli, basi we utachiz very soon!, una ukame wa mapenzi ya kweli ambao unakupeleka pabaya!
 
hapa Dar mi naifahamu couple moja ya namna hii.Wao walikutana utu uzima kila mmoja akiwa divorcee,wakapendana,wakaoana,hadi leo hii kila mmoja anaishi kwake wakiamua kukutana ni kwa miadi aidha kwa mr au kwa mrs,mi nawaonaga wana raha,kwenye sherehe/misiba wanakuja pamoja.
 
hakuna mwanaume atakubali hiyo ki2 labda mume wa m2 aliechokana mke wake awe anakuja kujiliwaza, kama ni kijana tu basi hzo siku atakazokuwa alon atapata mwingine wa kumjali yaan kumpikia, kumuogesha, kumfunga tai wakat we uko kwako unalea watoto... sikushaur isee
 
hili ulitakalo ni rahisi tafuta kazi mkoani ili muwe mnaonana kwa manati na hapo na hapo majibu ya ukitakacho utakipata kama hutajaziwa watoto wa nje au kukuta unasaidiwa na wa karibu ...
 
Usimweleze hiyo ndoto yako. Haitakaa iwezekane. Ila kama shughuli za kumridhisha mume zimekuchosha, mwambie akutafutie msaidizi
 
Huyo mume unaemtaka hayuko kwenye mpango wa Mungu ni kidunia zaidi ..omba Mungu aondoe mawivu yakupitiliza ingawa uliumbwa hali ya kumtamani (kuwa na wivu juu ya mumeo)
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.Waefeso (ephes)5:31
All the best
 
Unataka siku usipokuwa naye uwe unajivinjari na wengine, kudadeki nayeye anawivu wakutaka kukuona kila wakati.hapo ngoma drooooo. Unalo, hutaki kukosana?? Wagombanao ndo wapatanao best
 
Maryjina 1st umesema aje kwako mara 3 au 4 kwa wk bt ww kwena kwake as long as u want, huo ni ubinafsi.
2nd, unamuomba Mungu kitu ambcho hta yy anakipnga, huujui mpango wa Mungu kuhsu ndoa ww ''..atawaacha wazazi wake na KUAMBATANA na mwnzake na kuwa MWILI mmoja." huwez fankiwa labda kama humuombi Mungu..
 
@arusha,baba mngoni,mama mchagga

Nawasalim wana JF

Nina wivu sana wa mapenzi na nampenda sana laazizi wangu na siko tayari kutengana naye labda asiwepo duniani.Kuishi pamoja bila ugomvi as mme na mke ndiyo matakwa yangu ila kila aliye kwenye ndoa ananitisha kwamba ndoa ndoano.

Sasa ili kuepusha misuguano nataka nimweleze haya:
1.awe anakuja napoishi at my home place mara nne na kulala mara tatu hivi kwa wiki
2.Niwe na uhuru wa kwenda (mimi na watoto wetu) na kulala kwake as long as I want
3.Mwezi wa sita na wa kumi na mbili ahamie/nihamie tuwe pamoja mwezi mzima

My take:Hakika naamini akikubaliana na mimi kwa haya matatu haitatokea kununiana hata siku mmoja as long as every second we will be missing each other
Mtaani/kazini /kanisani wote wawe wanajua mimi ni mke wa flani na yeye ajulikane kuwa ni mme wa marytina


Hii tamthiliya inaitwa jina gani vilee?
 
Back
Top Bottom