A.swali:kutekwa na kukamatwa sheikh farid na ponda kunatatua au kunazalisha matatizo

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
135
Wanajamvi hebu tutoe maoni, ushauri kwa Viongozi wetu kwa matukio hayo mawili ya kutekwa na kukamatwa kwa viongozi wa Imani. Je kunatatua tatizo au kunazalisha matatizo mengine. Imetokea kwa mataifa mengine wakizani kwa kufanya hivyo ni kuzima moto kumbe ni kuuchochea.
Nia ni kupata hekima na busara za kuwasaidia viongozi wetu kutatua tatizo kwa namna huzalishi lingine. Kamanda ametaja kwanini wamemkamata Sheik Ponda ni pamoja na uchochezi, maandamano ya kidongo chekundu, kutishia viongozi halali wa BAKWATA, Vurugu za mbagala wakati kutekwa kwa Sheik Farid ni shughuli za uamsho kutokana na matukio hayo Zanzibar wamevamia ofisi za ccm kuchoma moto wakati huku bara wafuasi wa Ponda wameandamana wamepigwa mabomu. Hivyo hatua zilizochukuliwa zimezalisha matatizo mengine.
Karibu kwa hoja za nini kifanyike tusizalishe matatizo juu ya matatizo bali tutatue hasa kutokana na Ma Sheik hawa kazi zao na hatua wanazochukuliwa.
 
kunazalisha matatizo.
Je kuchoma makanisa na kuiba laptop za kanisa na sadaka kuna solve ama kunaongeza matatizo?
 
One step ahead kama kuuwawa kwa osama bin laden! ila wawekwe mahabusu nzuri!
kesho asubuhi wapewe chai ya rangi na vitumbua,mchana wapewe ubwabwa nyama! ili nao wafurahi kama wako kwenye hitma au arobaini!
 
Naomba nikuulize mleta mada, je kwa mujibu wa sheria kuna mtu aliye juu ya sheria? Sheria lazima ichukuie mkondo wake, kama mtu anasikika hadharani akitukana, kukashifu na kuchochea vurugu kisha, ili kulinda heshima yake kwa jamii, akaitwa akataa na kuhadaa Polisi, je asikamatwe??
 
Ponda nae kazidi kujifanya yupo juu ya sheria kiongozi gani wa dini asiyekuwa na busara ya kuyazungumza mambo katika njia sahihi bila vurugu?
 
Polisi kazi yao ni kupambana na uharif na kuzuia uhalif kutokea, hawa mashehe wamekuwa ni source ya ya vurugu ikiwamo kuchoma makanisa na kuendesha mandamano bila kibali. Kwasababu hizo tunalilaumu jeshi la polisi kuchelewa kuchukua hatua mapema ila tunawapongeza kwa kuwa wameanza kuzichukua na hilo ni fundisho kuwa hakuna aliye juu ya sheria
 
Sheria haina haja ya kujua kuwa tatizo limeongezeka au la asha.
Ukivunja sheria hata kama una umma wa dunia nzima lazima upate adhabu.

Soma criminology in detail utagundua umuhimu wa punishment.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hawa ni wakuwaua tu kama yule mwenzao wa mombasa

Safari ni moja kuuliwa na risasi kwa hujuma. Mbona balo kafa kijinga kabisa au umeona anapona. bora kufa responsibly kuliko kufa kwa kukimbizia kidemu. Hata wewe utakufa tena kwa aibu, kumbuka huwezi kuzidisha hata sekunde kama umeandikiwa kufa utakufa tuu hesabu ishafungwa siku roho zimeumbwa kabla ya kuletwa duniani
 
Wanajamvi hebu tutoe maoni, ushauri kwa Viongozi wetu kwa matukio hayo mawili ya kutekwa na kukamatwa kwa viongozi wa Imani. ....

kukamata viongozi wa Imani kunachochea matatizo lakini kukamata viongozi wa UGAIDI kunatatua matatizo
 
Wanajamvi hebu tutoe maoni, ushauri kwa Viongozi wetu kwa matukio hayo mawili ya kutekwa na kukamatwa kwa viongozi wa Imani. Je kunatatua tatizo au kunazalisha matatizo mengine. Imetokea kwa mataifa mengine wakizani kwa kufanya hivyo ni kuzima moto kumbe ni kuuchochea.
Nia ni kupata hekima na busara za kuwasaidia viongozi wetu kutatua tatizo kwa namna huzalishi lingine. Kamanda ametaja kwanini wamemkamata Sheik Ponda ni pamoja na uchochezi, maandamano ya kidongo chekundu, kutishia viongozi halali wa BAKWATA, Vurugu za mbagala wakati kutekwa kwa Sheik Farid ni shughuli za uamsho kutokana na matukio hayo Zanzibar wamevamia ofisi za ccm kuchoma moto wakati huku bara wafuasi wa Ponda wameandamana wamepigwa mabomu. Hivyo hatua zilizochukuliwa zimezalisha matatizo mengine.
Karibu kwa hoja za nini kifanyike tusizalishe matatizo juu ya matatizo bali tutatue hasa kutokana na Ma Sheik hawa kazi zao na hatua wanazochukuliwa.
Kumbuka kuwa serikali haina dini so unavyosema wakikamatwa wanachochea zaidi si kweli hakuna aliye juu ya sheria na hata wasipokamatwa watazidi kuchochea mambo wanayoyachochea huko mitaani....sasa bora kipi wakamatwe ili watanzania waheshimu sheria au waachwe waendelee kuvunja sheria kwa kuchochea chuki na kuharibu imani za watu wengine kwa kuwachomea makanisa..FIKIRIA CHUKUA HATUA..
 
kuna ule msemo ya kwamba MTOTO WA NYOKA NI NYOKA. mta mfunga ponda lakini mtabakisha watoto (wafuasi) wake ! ithe only good solution nikuelimisha watu kupunguza jazba, kuheshimiana na kuvumiliana!:A S-coffee:
 
nazani hatua hii imechelewa sana na kumtetea ponda ni kutetea ugaidi kwani hata magaidi wanasababu ambazo huteka watu akili wakijua wanatetewa kumbe wao ni daraja. tumeharibu, tusizidi kuharibu, tutakimbilia wapi u-alshabab ukianza??
 
Hakuna ushauri mpya zaidi ya kusema wamewachelesha. Ilitakiwa sasa ibaki historia tu. Serikali ongezeni usalama waweze kutapakaa kila mahari na kubaini mambo kabla hayajatokea.

Kuna kipindi ujambazi ulishamili sana Tz tukahangaika sana kupambana nao bila mafanikio mpaka pale tulipojua kuwa mojawapo wa maafisa wa juu wa jeshi la polisi yuko kwenye mtandao. Hata hili la waislamu kuvimba kichwa si hivihivi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom