A Parody of Presidential Eloquence - Kejeli ya Umahiri wa Rais katika Lugha

Mwanakijiji said:
Sijui kama itawezekana kuchapishwa kwenye mojawapo ya magazeti nyumbani..

Mwanakijiji,

..hiki kitu kizito. magazeti ya bongo yataogopa.
 
Hahahahahaha, this's one of the best posting MMM

Swali: Wewe kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unafikiri ni kwanini nchi yako ni maskini kupita kiasi? Unafanya jitihada gani kupunguza umaskini huu ni kuchochea maendeleo ya nchi?

Jibu:
Nasema mimi sijui, kama nchi ni maskini sijui
Umaskini umetoka wapi sijui, sababu gani sijui
Nifanye nini sijui, umaskini utapungua sijui
Nasema tena sijui, kamuulize nani sijui
 
Very interesting; yuko kama Pinokyo aliyekuwa anataka kusema uwongo huku akitaka asijulikane kuwa anasema uwongo lakini akajikuta anasema uwongo wa wazi kabisa, na hivyo pua yake ikazidi kurefuka.

Kama anasema hajui, na hili ni jambo linalohusu serikali yake, je amefanya nini ili kulijua kabla hajasimama kuhutubia taifa?
 
swali: rais wa tanzania ni nan?
J K: sijui
usishangae akijibu hivyo this is how our president behave!!
 
Tehe tehe teheee, mbona safari tunayo, dereva anahalisha na hakuna mwingine wa akiba, ndo kwanza tu tunaanza safari. Dereva hajui ni jinsi gani atawafikisha abiria wake, nao abiria pia hawajui ni nini kifanyike. Ngoja tusubiri tuone!
 
This is more than humorous. It is a real thought provoking master piece of leterature. Thank you Mzee Mwanakijiji. I suggest that you send this to a news paper like Mwanahalisi for publication or turn it into a minibook for Tanzanians to read and learn. Asante sana Mzee.
 
Ninawapongeza wale wote ambao wameiona hotuba hiyo kuwa ya kinafiki na ya uongo,Watanzania HATUDANGANYIKI!

Hicho kikao cha CC kilichoamua kuwa Dowans walipwe nani alikuwa Mwenyekiti wa hicho kikao?Au atwambie kama na CC haijui!Waziri wa nishati aliwataja hao wanaowasingizia kuwa ndo wamilika wa Dowans,leo hii Rais wake anasema HAWAJUI?Mahakama imesema,aliyepewa mamlaka ya kudai malipo hayo ni Rostam Aziz ambaye ni mjumbe mwezie wa CC,kwa nini hasimuulize ili amwambie hizo hela anazodai kwa niaba ya Dowans,zikishalipwa atawakabidhi akina nani?

KIUJUMLA HOTUBA INAKERA,INACHEFUA!

Inabidi yule shehe maarufu wa kumpa majini ya kumlinda aombwe amsaidie na majini ya kumpaushauri ni nini chakuongea maana yake akimuacha akiendelea kuongea kwa staili hii, yaani bila kutafakari nini aongee hatuto fika.
 
Ndo maana hata mie simjui huyo rais yenu, sijui hata alichaguliwa na kina nani..
 
Wow Wow! Did he really say all that? Kweli CCM inazaa mabuya...This is what CCM can do for you...I hope free minded CCM waliobaki watahama this time...Why remain as mwanachama wa CCM wakati mwenyekiti wako ni incompetent?

dont u c that this is satire?
 
Mzee MM,

Unaonanje hii single tuiamishie kule kwenye jukwaa la Burudani na Michezo...

Halafu fanya fasta uisajili hii kazi kule COSOTA kabla haijaibwa na vijana wa bongo fleva...:clap2:

Mwisho nasauri pia uwasiliane na Mh. SUGU ili ikiwezekana iwekwe kwenye Antivirus Mixtape Vol. 2....:coffee:

HAHAHAHAH...Hata taarab a.k.a Rusha-roho yafaa sana.
SHAROBARO RECORDS MPOOOO???
 
Kila mtu akiulizwa kitu ambacho anatakiwa awe na ujuzi nao au ambacho anaweza kujua akitaka aanze kusema "na mimi sijui".. tuone kama nchi itakwenda!
"sijui" mara nyingi ni utetezi mwepesi wa kukwepa maswali mgumu au maswali zaidi.

Mtu akishajibu " sijui" mara mbili au zaidi wewe muuliza swali unafanyaje?........jazia mwenyewe
 
"sijui" mara nyingi ni utetezi mwepesi wa kukwepa maswali mgumu au maswali zaidi.

Mtu akishajibu " sijui" mara mbili au zaidi wewe muuliza swali unafanyaje?........jazia mwenyewe

Ni jibu ambalo wazazi linawaudhi na watoto linawakera; walimu linawatibua na wanafunzi linawaumbua. Mtu anaposema "sijui" kwa kweli anakuweka mahali pa kushindwa kuendelea kumuuliza. Wenzetu huwa wanasema "I can not recall that"... akibanwa kizimbani.
 
Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


Jibu:
Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?


Jibu:
Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?


Jibu:
Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?


Jibu:


Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?


Jibu:


Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?


Jibu:


Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?


Jibu:
Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


Jibu:


Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
Kama najua sijui, kama sijui sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

SASA WANAJAMII TUNAFIKA KWELI NA TANZANIA YETU HII??

 
Nimecheka sana hapo mwisho kwamba hata yeye kama ni Rais wa JMT hajui... ni kweli inafikirika, kwa madudu anayoyaafanya hajui nafasi yake katika nchi........ Poor JK......
 
Back
Top Bottom