A New Call To Action: Tuchangie Chama cha Msalaba Mwekundu kusaidia Waathirika wa Mafuriko

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987

Japo natamani kusema maneno makali juu ya mafuriko ya Dar najikuta napatwa na mzigo mkubwa moyoni kwa mara nyingine tena. Mwaka Jana Januari tulianzisha Harambee ya kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania kukipa uwezo wa kukabiliana na janga la mafuriko la Kilosa. Kama nilivyosema wakati ule (na kuandika kwenye Gazeti la Tanzania Daima) kuchangia TRC (Tanzania Red Cross) ilikuwa ni kuwekeza kwa majanga ya baadaye kwani hakuna chombo nchini ambacho kina uwezo wa kusaidia wakati wa majanga kama Chama hiki cha Misaada ya dharura.

Niliandika hivi:

Tunakisaidia chama chetu hiki kwa sababu siku ya shida yetu na shida ya ndugu zetu kule kijijini ni hawa watakaokuwa wa kwanza kusaidia. Tumeyaona Haiti na Wamarekani kama walivyo Wahaiti wanaoishi Marekani hawakuchelewa mara moja kuanza kukisaidia Chama chao cha Msalaba Mwekundu. Ilikuwa hivi hivi wakati wa matukio ya Septemba 11 na hata wakati wa kimbunga cha Katrina kule New Orleans.

Hatuwezi kuitegemea serikali katika majanga. Karibu serikali zote duniani haijalishi ukubwa wake hazina uwezo wa kutoa misaada ya kiutu na kibinadamu kwa haraka na kwa ufanisi kama Chama cha Msalaba Mwekundu. Kwanza ni kwa sababu ukiritimba na pili kama serikali inanuka ufisadi itakuwa ni wazimu kutegemea kuwa wakipata mabilioni ya fedha yatawafikia walengwa au ndiyo yatakuwa ya kujengeana majumba ya kifahari kwa sababu "wanastahili".
Nina sababu nyingine ya kutoiachia serikali jukumu hilo au kuichangia kama wengine ambavyo wangeweza au wanafanya. Miaka miwili iliyopita niliandika makala iitwayo: "Taifa lisilojiandaa kwa majanga limejiandaa kwa maafa".

Nilianza makala ile kwa kusema, "Sisi kama taifa tunajaribu kuishi kwa kubahatisha na kuacha maisha yetu ya siku zijazo kuwa ya kubahatisha (kwamba tunaishi na mawazo ya ‘liwalo na liwe'), na pili, licha ya kujua uwezekano wa majanga mbalimbali yanayoweza kutokea, hatujajiandaa vya kutosha kuyakabili majanga hayo na hivyo pia kuweka maisha yetu katika sanduku la bahati nasibu!"
Sijui ni wangapi ambao wameshaamua kuishi kwa bahati na kusubiri majanga yatokee ndio waulize Chama cha Msalaba Mwekundu kiko wapi? Siku moja yatatokea majanga (ndiyo yatatokea siyo kwamba nawachuria), na kila mtu atatamani watu wa Msalaba Mwekundu wamfikie. Lakini tusipowasaidia mapema kabla ya majanga hayo tusishangae kama hawatakuwa na uwezo wa kufika huko kwa sababu watasubiri misaada kutoka Marekani na Uswisi!

Makala yote unaweza KUISOMA HAPA

Sasa matuko haya ya majanga ambayo yanaendelea nchini na kama nilivyoandika kwenye FIKRA PEVU kuwa mvua hii haiishi hadi Jumamosi (Mkesha wa Krismasi) ni wazi kuwa mnachoona kuwa ni madhara bado hayajafikia kikomo chake kwani Jiji letu litapigishwa magoti. Naweza kusema mengi ya kisiasa (Ningeweza kukumbushia mojawapo ya zile makala za "Taifa lisiliojiandaa kwa majanga, limejiandaa kwa maafa"). Lakini kwa sasa najizuia kulipuka (japo ni vigumu). NInatoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya Tanzania kuanza kampeni mara moja ya kuisaidia TRC kukabiliana na majanga haya.

Binafsi sipendi na siungi mkono sana kupeleka misaada kwa "mkuu wa wilaya" au vyombo vya "serikali". SIVIAMINI KWANI NI SEHEMU YA TATIZO ZIMA LA KUKUBILIANA NA MAJANGA. Tuungane kusaidia Chama cha Msalaba Mwekundu kiwezi kutoa misaada ya kiutu na kibinadamu kwa waathirika. Tusisubiri wapewe misaada kutoka nje ya nchi. Najaribu kuona jinsi gani kama sisi JF wenyewe tunaweza kuanzisha kitu chetu wenyewe kwa ajili ya kutoa misaada ya kiutu - inatosha kulumbana na kubishana lakini zinapotokea changamoto za Kitaifa tuwe pamoja.

Mimi mwenyewe naweza kuhisi kuwa haya marufiko yatagusa siyo chini ya watu milioni 1 na watu wasitegemee sana misaada mingi ya kigeni hasa kwa vile nchi nyingine nazo zimekumbwa na mafuriko na hali ya uchumi wa dunia ni mbaya sana - ni LAZIMA TUJITEGEMEE KWA KIASI KIKUBWA SISI WENYEWE.

Kwa wanaokumbuka mwaka jana kwenye janga kama hili tuliweza kutoa misaada ya vitu na mali mbalimbali kwa TRC vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi tukiongozwa na Kamanda Sanctus Mtsimbe na timu nzima ya TPN.

Wakati tunasubiri to set up a mechanism* napendekeza watu wachangie moja kwa moja kwa TRC - the best option.

MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
P.O. Box 1133 Dar es Salaam
Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843
logistics@raha.com

Nitawajulisha mpango wowote ambao JF tunaweza kuja nao kuweza kutoa misaada yetu. Japo wakati wa kuwakalia kooni na shingoni tena unakuja kuhusu uzembe uliokithiri kuhusu mafuriko haya kwa wakati huu tusaidiane kwanza kuwasaidia watu kwa sababu baadhi ya vitu ambavyo vitahitajika kwa haraka ni:

Maji ya Kunywa
Nguo
Dawa za maumivu (ambazo hazijaharibika)
Vitu vya Usafi kwa wanawake (female hygienic products)
Sabuni
Non-perishable food products (zaidi vyakula vya makopo)
Vitu kwa ajili ya watoto (nepi, n.k)
Vyandarua

* Nadhani kabla ya kesho tutakuwa tumekuja na mechanism ya kuratibu shughuli zetu kama JF kusaidia TRC kukabiliana na majanga haya. Kama kuna mtu ana suggestion ya jinsi gani tunaweza kufanya hivyo please I'm open to hear it.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji;
Tuelezeni namna ya kuchangia; pia ishauri serikali badala ya kutaka kukimbilia kuilipa Dowans; pesa hizo zitumike kwenye maafa yaliyotokea.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mwanakijiji;
Tuelezeni namna ya kuchangia; pia ishauri serikali badala ya kutaka kukimbilia kuilipa Dowans; pesa hizo zitumike kwenye maafa yaliyotokea.

Chama
Gongo la Mboto DSM

Wenye kuiangalia serikali kwa kweli imekula kwao.
Believe me.. hili la serikali nilishakata nao tamaa - wala kuwaambia kitu chochote sioni sababu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
mimi nilichangia wakati wa mafuriko ya kilosa lakini sijui kilipatikana kiasi gani na kilitumika vipi.halafu mchango ulikuwa wa mwezi mmoja lakini mimi nilikatwa zaidi ya mwezi husika,haya ni maeneo ya kuangaliwa kabla ya kutoa michango yetu kwa mara nyingine.halafu sijui ile kodi yangu ninayokatwa kwa mwezi ni kiasi gani kinatengwa kwa ajili ya majanga ya kimazingira au zote zinaishia kwenye sherehe za uhuru pekee!
 
Mbona taarifa zote zilikuwa zinawekwa hapa hadi tulipowasilisha mchango wa mwisho?
 
Tatizo la hiki chama cha msalaba mwekundu kikishachangiwa huwa hakileti mrejesho kuwa kimepata kiasi gani na zimetumikaje, sasa watu watakuwa wagumu kuchangia kwani hata kwenye makanisa kama kwa Kakobe watu wanataka kujua zinakusanywa ngapi ndio m,aana wamemburuta kortini.

Washauri watueleze za Kilosa zilipatiokana ngapi,
Za Gongola Mboto zilipatikana ngapi

Na zilitumikaje ili sasa wawe na uhalali wa kukusanya tena michango.
 
mi nawasiwasi na wale wenzangu wa siasa kali, ile alama ya msalaba ile tena mwekundu italeta tabu kidogo kwao, nawasiwasi kama hawataweka kunji juu ya uchangiaji... kwa walio nje ya tanganyika itakuwaje mzee mwanakijiji?
 
Tatizo la hiki chama cha msalaba mwekundu kikishachangiwa huwa hakileti mrejesho kuwa kimepata kiasi gani na zimetumikaje, sasa watu watakuwa wagumu kuchangia kwani hata kwenye makanisa kama kwa Kakobe watu wanataka kujua zinakusanywa ngapi ndio m,aana wamemburuta kortini.

Washauri watueleze za Kilosa zilipatiokana ngapi,
Za Gongola Mboto zilipatikana ngapi

Na zilitumikaje ili sasa wawe na uhalali wa kukusanya tena michango.

Unaweza kupata taarifa zaidi hapa za matumizi: Tanzania Red Cross National Society - IFRC
 
Tatizo la hiki chama cha msalaba mwekundu kikishachangiwa huwa hakileti mrejesho kuwa kimepata kiasi gani na zimetumikaje, sasa watu watakuwa wagumu kuchangia kwani hata kwenye makanisa kama kwa Kakobe watu wanataka kujua zinakusanywa ngapi ndio m,aana wamemburuta kortini.

Washauri watueleze za Kilosa zilipatiokana ngapi,
Za Gongola Mboto zilipatikana ngapi

Na zilitumikaje ili sasa wawe na uhalali wa kukusanya tena michango.

Wewe changia tu siyo lazima upate auditing report hata kwa issue ya misaada lol
 
Napenda kuchangia, lakini naogopa uchakachuzi kama ule wa Kilosa, michango itolewe na wana JF halafu presentation ya michango ifanyike kwa jina la Voda na Clouds. MØ@x!"#¤%&/
 
Back
Top Bottom