A "missed" Golden Opportunity for JK's Legacy and Vision for the Next 50 Years?

Andrew

Member
Feb 14, 2007
6
0
Wana-JF, nilidhani Mkuu wa kaya angetupatia kitu cha maana sana watz kama vile kuelezea kwa kinaganaga juhudi zilizokwisha fanyika, kitu Muhimu ambacho kingebakia kama 'Legacy' yake wakati wa kutoa hotuba ya kuazimisha miaka 50 ya uhuru pale kiwanjani, na hata kutoa maono au dira 'VISION' kwa miaka mingine 50 inayokuja ambayo ingeweza kuwekwa kwenye kumbukumbu muhimu kwa mstakabali wa taifa.

Kwa mshangao mkubwa hatukuona ujasiri zaidi ya kuomba msamaha wa kutokutoa hotuba ndefu! je, tunaelekea wapi? Maana tunajua tulikotoka! Kumbukumbu gani itawekwa kwa ajili ya taifa letu, kwa faida ya vizazi vijavyo, kutoka kwa kiongozi wa awamu hii ambapo Taifa letu limefikisha miaka 50?
 
Back
Top Bottom