Che Kalizozele
JF-Expert Member
- Jul 20, 2008
- 777
- 49
Nimegundua ukiwa na uchungu na maisha ya watanzania wanaotaabika na hali zao duni,utakuwa umebeba mzigo mzito sana.Kila siku uwa najiuliza,kwa nini maisha yetu yanakuwa mabaya kila siku na sipendi kukubali kuwa ufisadi ndo sababu ya haya yote.Najua kuna sehemu ya umasikini wetu umechangiwa na ufisadi lakini nina imani haya hayakuanza leo na si tatizo la tanzania peke yake.kwa mfano,uwa najiuliza ni nini kilichosababisha mabadiliko makubwa ya ukali wa maisha toka kikwete ameingia madarakani na maisha yanapanda kila siku,amekosea wapi?
Siku moja nikiwa katika kufikiri,nikahisi tatizo tulilonalo ni uongozi.Hatuna viongozi mathubuti,viongozi wenye nia thabiti ya kuwatoa watanzania katika lindi hili la umasikini.Viongozi wanaojua wajibu wao na wanao heshimu na kujua uzito wa kazi aliyopewa.Kukosekana kwa uongozi mathubuti kumesababisha nchi yetu imekuwa ni nchi ya self service,hakuna nidhamu na wala hakuna anaeangalia na kufikiri kuwa kuna vizazi vinakuja na vinawategemea katika yale wanayotengeneza sasa.Kila mtu anajiudumia ili mradi tu kapewa nafasi,sasa tatizo linakuwa kwetu tunaosubiri tuudumiwe.
Nchi hii inahitaji kufanyiwa repair ya nguvu,na ili hili lifanikiwe linahitaji kiongozi,nikimaanisha kiongozi na si mbabaishaji.Nafikiri vita dhidi ya ufisadi isipokwenda bega kwa bega na kuangalia nani anaweza kutuongoza katika kuifanyia repair nchi yetu,vita hii itakuwa kama ile ya Israel na wapalestina.
Haya ni mawazo yangu.